Mkopo wamkosanisha na mpenzi

Kuna Jamaa ana mpenzi wake, wanakaa tofauti lakini wapo karibu sana. Jamaa anafunguo za nyumba ya mpenzi wake kwa hiyo asipomkuta hufungua na kukaa akimsubiria halikadharika na demu hivyohivyo. Sasa kasheshe imejitokeza kumbe jamaa alichukua kadi ya gari ya demu bila kumwambia kaenda kuchukulia mkopo yapata mwaka sasa. Na jamaa hali mbaya sasa ameshindwa kumalizia deni, watoa mikopo wamekuja juu wanataka gari tu. Hapo demu ndio amejua kumbe kadi yake ilitumika kukopa huo mkopo nae kaja juu ile mbaya na hamtaki tena huyo jamaa.

katika hali hiyo wa JF mnashauri nini?

Mwana dada yupo sahihi kabisa maana jamaa hajafanya jambo jema na wala si la kistaarabu kabisa na jamaa anawajibu wa kuadhibiwa kabisa
 
Mke wangu umesemaje eti?

uwiiii......... Asprin cheza na mimi upendavyo ila usicheze na pesa wala mali yangu. uwiiiii hapa watahitimisha lile ambalo wengi husema juu ya upalestina. kiruuu eleri hainaga umume wala umke aisee.

ila ndio tatizo la vijana wa siku hizi ambao wao ni opputunistic msemo wa Kongosho. kwanza hadi uwe huru kuja kwangu inamaana lazima nikuamin na hata kama nakuamin funguo za droo zangu za ndani ama safe hutakaa uzione wala ujue password.
 
Last edited by a moderator:
ni story ya kweli , huyo demu ana jina la kilugha, kama Bumi, Gwantwa huwezi kujua kama demu au mwanaume. alitumia jina la demu kama jina lake

Yaani huyo mwanaume ni zaidi ya mwizi! Pia atakuwa hampendi huyo demu wake vinginevyo angemshirikisha. Angekuwa kanifanyia mie ningehakikisha anakunywa mvua za kutosha segerea.
 
Kuna Jamaa ana mpenzi wake,
wanakaa tofauti lakini wapo karibu sana. Jamaa anafunguo za nyumba ya
mpenzi wake kwa hiyo asipomkuta hufungua na kukaa akimsubiria
halikadharika na demu hivyohivyo. Sasa kasheshe imejitokeza kumbe jamaa
alichukua kadi ya gari ya demu bila kumwambia kaenda kuchukulia mkopo
yapata mwaka sasa. Na jamaa hali mbaya sasa ameshindwa kumalizia deni,
watoa mikopo wamekuja juu wanataka gari tu. Hapo demu ndio amejua kumbe
kadi yake ilitumika kukopa huo mkopo nae kaja juu ile mbaya na hamtaki
tena huyo jamaa.

katika hali hiyo wa JF mnashauri nini?

duh?kazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom