Mkopo wa dola milioni 500 wenye riba ya dola milioni 400? Huu ni unyama na ufisadi!

Tunakoenda kutakuja kuwa na anguko la kiuchumi Tanzania kwa mwendo huu hakukuwa na ulazima wa kukopa pesa zote hizo kwa wakati huu hiyo riba ya 80% ni kubwa sana yaani kama atuna watu wa kushauri vitu
 
Nimeona kwamba Taifa limepata mkopo wa dola milioni 500,lakini riba yake ni dola milioni 400,na unalipwa ndani ya miaka mitano

Hii ni wastani wa malipo ya dola milioni 100 kwa kila dola milioni 100,yaani shilingi inazaa shilingi,dola milioni mia inazaa dola milioni mia.

Huu ni wizi wa mchana kweupe,utapeli,unyama,ufisadi ,ambao utalitesa taifa na wananchi masikini

Najiuliza tu,ni nani walikuwa kwenye majadiliano haya yaliyoliuza taifa?maana haya ni mauaji kabisa

Na huyo anayetamba kuwa ni rais wa masikini na wanyonge,hizi ndio riba za kuwatwika watu masikini kweli? Hizi ndio riba za kumbebesha masikini wa taifa hili? Mikopo hii ndio itaondoa umasikini?

Bahati mbaya hata matumizi ya pesa hizi hayajulikani yatakuwa nini

Najumuisha kuwa huu ni unyama kwa taifa
No wonder Zitto amekamatwa ...............................!!
 
Umeona wapi?hebu na mie nioneshe huo mkataba wa mkopo nione hiyo riba ya dola milioni 400!hakuna kitu kama hicho duniani na ukinionesha huo mkataba nipigwe ban ya maisha humu JF
Mlizoea kusihi kwa ghilba na uchonganishi tu,kawadanganye Tanapa wenzako ndio wanaweza kuchukua uongo huu
Na mimi pia ntaomba ban niungane na wewe...
 
Nilipoandika kuwa JPM hachukii ufisadi ila anachukia ufisadi kuanikwa kwa wananchi niliambiwa nimeandika rubbish

Narudia TENA, JPM hachukii ufisadi, anachukia wananchi tukijua kuwa kuna ufisadi
 
Nimeona kwamba Taifa limepata mkopo wa dola milioni 500,lakini riba yake ni dola milioni 400,na unalipwa ndani ya miaka mitano

Hii ni wastani wa malipo ya dola milioni 100 kwa kila dola milioni 100,yaani shilingi inazaa shilingi,dola milioni mia inazaa dola milioni mia.

Huu ni wizi wa mchana kweupe,utapeli,unyama,ufisadi ,ambao utalitesa taifa na wananchi masikini

Najiuliza tu,ni nani walikuwa kwenye majadiliano haya yaliyoliuza taifa?maana haya ni mauaji kabisa

Na huyo anayetamba kuwa ni rais wa masikini na wanyonge,hizi ndio riba za kuwatwika watu masikini kweli? Hizi ndio riba za kumbebesha masikini wa taifa hili? Mikopo hii ndio itaondoa umasikini?

Bahati mbaya hata matumizi ya pesa hizi hayajulikani yatakuwa nini

Najumuisha kuwa huu ni unyama kwa taifa
Mkuu kwani una uhakika hiyo riba yote wanachukua wenye Mkopo??
Pengine riba ingine inabaki hapa hapa nchini kaka,
Ila sasa Riba hiyo inabaki kwa nani na inabaki kivipi hapo ndio sielewi Mkuu wangu
 
they want to eliminate political parties or to mute/silence political leaders in order to fulfil the rule of law!!?is the type of power monger?
 
Huo mkopo kama ni kweli ulichukuliwa kwa "hali ya dharura" kusherehekea mpango mzima wa kigaidi wa kumuondoa Mh.Lissu kwenye uso wa dunia.
 
Mkuu Papaa Musofe, Naomba nikurekebishe kidogo katika mahesabu,
Ukikopa 500, kalipa 900, maana yake riba ni asilimia 80%, ingekuwa umekopa 500, na kulipa dola 100 kwa dola 100, then riba ni asilimia 100%.

Huu ni mkopo ambao hauna dhamana, hivyo ni very risk naunakuwa na interest kubwa, kama hawa loan-sharks, unaitwa syndicated loan, ambao unatolewe kwa muungano wa mabenki ili kupunguza risk ya kutolipwa.

Kwangu kitu muhimu sio kwa nini tunakopa kwa interest kubwa hivyo, bali issue kwangu ni tunakopa kwa interest kubwa hivyo kwa dharura gani?, nikimaanisha mkopo wa aina hiyo inaweza kuchukuliwa kwa ajili ya dharura tuu!, kama tunauwezo wa kupata dola milioni 900 ndani ya miaka 5!, then, badala ya kukopa hizo dola milioni 500 na kulipa kulipa dola milioni 400 ndani ya miaka 5, then serikali makini yenye uwezo huo, ingezitumia hizo dola milioni 900 kwa maendeleo, na sio ka nchi masikini kama Tanzania kanatumia dola milioni 400 kulipia riba kwa benki tajiri ya Uswisi, kiukweli kwa somo langu la uchumi nililofundishwa kwenye makaratasi, huu ni uendawazimu!, ila uchumi wa makaratasi na uchumi halisi ni vitu viwili tofauti!.

Kama ule mkopo wa dola bilioni 1.2 wa Exim bank ya China kujengea bomba la gesi, ulikuwa na riba ya asilimia 01% kwa mwaka na watu tulilalamika humu,
Bomba la Gesi Mtwara:A "20 -Year Grace Period" ya Mkopo wa Exim ...

huu mkopo wa sasa wa riba asilimia 80%, kiukweli tumebaki speechless

Paskali
Mkuu ata wewe unachangia kwa mihemko?!! Ivi unakubaliana nae vipi mtoa mada kwamba serikali imetozwa 80% ya riba kuna mkataba wa mkopo ame attach kwenye uzi wake au data yoyote iliyojitosheleza ku support anachoongea?

Jf GT imepotea kabisa.
 
Back
Top Bottom