Mkopo na dhamana ya cheti

Wazabanga kuku

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
264
379
Wadau,

Nina wazo la kuanzisha chuo cha hotel na utalii au kufungua mgahawa na bar kubwa but sina mtaji, je kuna bank ambayo inaweza kunikopesha angalau 20 milioni kwa kuweka dhamana vyeti vyangu vya shule kuanzia darasa la kwanza hadi PGDE. Manake sina kitu kingine cha kuweka dhamana sina ardhi, sina nyumba sina chochote zaidi ya kumiliki hivi vyeti.

Nijuzeni bank gani inawezanisaidia.
 
Inahuzunisha sana, msomi kama wewe ambaye umesoma mpaka PGD huelewi jinsi mkopo unavyotolewa.

Kimsingi, taasisi za kibenki zinatoa mkopo kwa kuweka rehani kitu chenye thamani sawa na mkopo uliouchukua. Yaani, kama unataka mkopo wa 20m uhakikishe kuwa una mali (ardhi, nyumba) yenye thamani zaidi ya 20m. Hii ni ili endapo utashindwa kurudisha fedha zao basi wauze hicho kitu na hela yao irejee kwenye system.

Vyeti vyako sawa, vinaweza kuwa vimetumia fedha nyingi na akili pamoja na muda kupatikana. Lakini taasisi husika haiwezi kuviuza baadae na kurudisha hela yao. Potelea mbali, uuzwaji wa cheti ni marufuku na hauruhusiwi kisheria.

Na baadhi ya taasisi tu zinazotoa mkopo mdpgo sana bila kuweka kitu rehani. Na mara nyingi haizidi 500,000. Namaanisha M-PAWA , L-MICROFINANCE na nyinginezo. Hao watakufatilia wanavyojua wao. Benki hazina huo utaratibu. Hata kama umesomea Harvard, hawataki vyeti vyako.

Pole sana Mkuu ila usikate tamaa. Mungu atakuwezesha.
 
Back
Top Bottom