Mkono wa Sheria ni kwa CDM tuu na Wanyonge??!! Tujikumbushe ya Lusinde | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkono wa Sheria ni kwa CDM tuu na Wanyonge??!! Tujikumbushe ya Lusinde

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eumb, Jul 17, 2012.

 1. eumb

  eumb Senior Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jana Ndg Mwita Mwikabwe (Chadema) amepandishwa kizimbani huko Singida akikabiliwa na tuhuma za kumtukana Mwigulu Nchemba (CCM).

  Nikakumbuka kisa cha Lusinde aliyesimama hadharani na ikawa recorded akimwaga matusi mazito, lakini huyu alionekana ameteleza tena akakaribishwa na kwenye media mbalimbali kama clouds radio ili aweze kusahihisha kile alichosema japo hakuweza kwenda kufuta kwenye youtube Mh. Livingstone Lusinde akimwaga Sera za CCM Arumeru - YouTube Sasa najiuliza japo Mwita atapewa nafasi ya kujitetea mahakamani lakini huyu wa CCM yeye hakustahili kupandishwa kwa Pilato naye??

  Au CCM wako juu ya sheria? Tumesikia jinsi Chadema walivyoeleza hali ilivyokuwa tete siku ya mkutano, na wametaja na RB No baada ya kutoa taarifa polisi, hivi hawakustahili kusikilizwa? Au CCM ndio chama kinachostahili kwa kila kitu?
   
 2. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,377
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Ccm ni wanafiki sana!haya yote wana fanya kwa kuwa police,mahakama na jeshi ni vyao sababu haiingii akilini taarifa ilishaa tolewa halafu police wapo eneo la tukio wakikodoa mimacho tu!sasa kweli naamini Tanzania hakuna chombo huru!
   
 3. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwisho wa yote ilikuwa hivi, huko Zambia UNIP, Kenya KANU na maeneo mengine vyama hivyo vimekuwa pinzani vinalalamikia sheria mbaya wakati vyama hivyo vilipitisha hizo sheria vikiwa madarakani.

  Hapa Tanzania yatatokea hayo CCM watakuwa wapinzani watalia kwa sheria hizi kandamizi, wakati huu wanacheka mpaka magego yanaonekana.

  Mwanasheria mkuu wa Serikali naye kawa Mwanasiasa wa CCM kama tulivyomuona jana jioni.
  2015 Mungu tupe uhai tufike salama tupige kura, tusimamie kura, tuhesabu kura na kupata matokeo.
   
 4. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mtuhumiwa No moja ni Nchemba.
   
 5. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mh kwani lusinde hakushitakiwa?
   
 6. D

  Dopas JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni watanzania wengi tuna akili ngumu ya kuelewa, vinginevyo CCM leo isingekuwa inaendelea kufanya inayoyafanya, chaajabu pamoja na udhaifu wa ccm na uongozi wake, bado wapo watu wanaikumbatia huku wakilia.... hali ngumu.. maisha magumu.. nk
  Kwa hali hiyo safari ya ukombozi ni ndefu kuliko tunavyodhania...
   
 7. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Yani anakera kama si learned one?
  Ana iangusha sheria kwa kulalia upande mmoja
  Yuko kimaslahi zaidi
   
 8. K

  Kizotaka JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bandugu watanzania wengi aslimia 95 leo hii ni kama wamepigwa bumbuazi, mambo tunayaona kabisa lakini wala hatuna habari, na viongozi wa ccm wanajua kuwa rais wa tanzania ni kazi rahisi sana, ndo maana wanagombania, watz bado wengi wajinga
   
 9. andate

  andate JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 2,655
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  CCM sio wanafiki. Serikali ya CCM inaendesha nchi ki-dictator. wananchi wengi hawalioni hilo. Watu hawaruhusiwi kuonyesha misimamo yao dhidi ya ufedhuli wa serikali, na ikitokea mtu akathubutu anaadhibiwa vikali.

  Na sasa hivi imefikia hatua hadi mbunge anaambiwa aripoti polisi kisa tu hoja zake zinapingana na serikali. Sasa hata maana ya bunge inakuwa haieleweki.

  Watetezi tuliowatuma bungeni wanalazimishwa kuto-kututetea.
   
 10. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Yan ccm wanachekesha sana!
   
 11. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Somalia ilianza hivi hivi. Bunge kiroja, Mahakama kiroja, polisi kiroja Serikali kiroja. Ni nani kawaloga? Hawakulagwa ila kwa sababu wajiangamize. Kilichobaki kwa umma ni kwamba hatuna tumaini tena ila kujihami kwa kuchukua sheria mkononi. Kila mtu ajue namna ya kujilinda mwenyewe. (things fall apart!!!)
  .
   
 12. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Mimi bado nawatetea Polisi hawana jinsi inabidi wafuate matakwa ya aliyewapa hizo nafasi, ilimradi tuu wasije wakafa njaa naamini hata wao hawapendi kutumika kama condom kiasi hicho lakini hawana jinsi. Ndiyo maana namshukuru Mungu kwa kukataa enzi hizo kwenda kusomea Upolisi kule CCP.
   
 13. m

  manucho JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tamati ndiyo hiyo, tunaelekea makaburini sasa
   
 14. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #14
  Jul 17, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,949
  Likes Received: 6,706
  Trophy Points: 280
  Jeshi letu la polisi lipo so biased, hakuna ubishi matusi aliyoporomosha Lusinde kule Arumeru yamepitiliza kwa mbali sana ukilinganisha na yale yanayodaiwa kutolewa na Mwita huko Ndago, hata hivyo Mwita kakamatwa, wakati Lusinde anaendelea kupeta mitaani!

  Hebu tujiulize hivi wale waliowacharanga mapanga wabunge wetu kule Mwanza weshafikishwa mahakamani?

  Jeshi la polisi ingawa linaona raha sana kuwatesa wapinzani, lakini watambue mwisho wa CCM kutawala unakaribia sana mwisho wake, hivi sura zao hao manjago, wataziweka wapi, wakati huo utakapowadia, ambapo CDM itakuwa madarakani na CCM kuwa chama cha upinzani?
   
Loading...