Mkono wa birika umeigharimu chadema chaguzi hii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkono wa birika umeigharimu chadema chaguzi hii?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Nov 2, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,979
  Trophy Points: 280
  Kwa vituo takribani 52, 000 Chadema ilipaswa kutumia bilioni tatu kuwalipa mawakala kwa vituo vyote nchi nzima na kwa shilingi elfu hamsini kwa kila wakala.................kwa kutofanya hivyo na kuwategemea wagombea udiwani na ubunge kuwagharimia mawakala ulikuwa ni mkono wa birika ambao sasa machungu yake wote tunayaona..........

  Pale ambapo NEC iliyoteuliwa na CCM ilipoamua kutowalipa mawakala Chadema ilipaswa kushtuka kuwa ni mkakati mzito wa CCM wa kuwarubuni mawakala kusaini matokeo ambayo yawezekana siyo sahihi....................Taarifa nilizonazo Chadema wanadai wanazo takwimu ambazo zaonyesha Dr. Slaa kashinda Uraisi.....kama hizo taarifa ni kweli basi mkakati wao ulikuwa ni sahihi.............lakini kama siyo ni kweli basi kurudia kuhesabu kura katika chaguzi zote zenye utata ni jambo la muhimu kwa minajili ya kuwatoa hofu wapigakura kama kweli sauti yao haikudhulumiwa na ufisadi wa CCM...........................

  Hili ni la muhimu hata kwa CCM yenyewe katika kuweza kupata uhalali wa kuongoza nchi bila ya zengwe na mashaka kuwa ni dhuluma tu ndiyo inawaweka madarakani..........na aliyeingia madarakani kwa dhuluma ataendeleza dhuluma kubaki madarakani na katika kuwatumikia raia....

  Huko tuendako Chadema iwe na mkakati wa kuweka fungu mapema la kuwalipa mawakala nchi nzima kuondokana na wasi wasi kuwa mawakala wana ukata mkubwa kiasi kuwa waweza kununuliwa........uwakala ni kazi yenye kustahili kuheshimiwa kwa malipo pamoja na kuwepo punje punje za kujitolea................
   
 2. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hivi Ruta umesha-ongea na wakala yeyote wa CHADEMA na aka-sema hakulipwa????
   
 3. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mimi sitahitaji shilingi hata moja kusimamia mahala popote chadema watanihitaji. Fedha isiwe kigezo cha ukombozi wa nchi yetu. Tunahitaji kujitoa zaidi kuliko kutegemea tulipwe. Kutegema chama kuwalipa ni kukubali kuwa mawakala wetu wetu walikuwa kwa maslahi binafsi zaidi kuliko wananchi wa Tanzania.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Rutashuba---nanihii

  regardless of what you think, opposition will have a smooth ride on 2015. because chadenma have paved the way for their progress

  we roll tings'/...........
   
 5. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Kudos Aeka Mangi.

  The issue of money for service to your party is the CCM way. I dont think we should go the same way to build CHADEMA, CUF, or any other political party in that matter. This will set a bad precedent that money is the issue. I believe that the ideology and the urge to serve is the building block for a strong and cohesive party. Members will have to understand that party politics is not about individuals gains but community service whose dividends have public interests. Tusianze mambo ya wajumbe wa kikao kujilipa madonge manono kuliko manufaa ya kikao chenyewe.

  It will be hard to a society and leadership used to benefit from these clandestine payments, however, we need to be principled otherwise five to 10 years to come, we will find ourselves in the CCM mess today!!!
   
 6. K

  Kashishi JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2010
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 1,101
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe mia kwa mia ndugu yangu. Ukombombozi wa kweli ni lazima uanzie kwenye nafsi ya mtu mwenyewe kwani unaweza kuwalipa mawakala hata laki moja na kama bado ni mtu asiyena maono na dhamira ya kweli basi wakala huyo akihongwa millioni moja atahujumu ushindi wa chama tu.
  Maana tafsini kwake amekosa maono na utashi. Hivyo fedha isiwe kigezo bali pengine staili ya kupata mawala pengine ingeweza kufanywa kwa umakini wa ziada badala ya hii kamata kamata ya last minutes ili kukamilisha number ya mawakala. Wawe ni watu wenye quality na dhamira dhabiti.
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  You should not have said this buddy, but i do not only respect you but also i respect your analysis. As for me dude money should never ever be the hurdle against our political and economic struggles against the fisadis!
   
 8. Nkoboiboi

  Nkoboiboi JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ruta.. CHADEMA (Tanzania ya kweli ) haihitaji malipo ya kifisadi kama haya!!! Hivi kura kama ni kwa ajili ya Maendeleo Yetu inahitajikulindwa na mwanadamu!!!! Wacha wajitwike laana ya kuiba haki za watu watakaa utumwani miaka 430 (Naona prof yako ina Bible) nafikiri unaelewa maanayake - WANA WA YAKOBO NA FARAO
   
 9. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kulikuwa na post hapa isemayo 'Ushindi wa JK ni shubiri kwa CCM'. Ambaye anaweza kuipata ai repost tena tafadhali.
   
 10. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Pamoja na ukweli kwamba watu kadhoo si wanachama wa CCM, taratibu na mazoea yaliyojengwa na Mfumo wa serikaliya CCM katika maisha yetu ya kila siku umetuathiri kwa kiwango kikubwa sana.
  Bado tunatamani kutajirika kwa wizi uuaji uongo na unafiki.
  Wako walioingia ndani ya mageuzi kwa sababu wamepanga foleni ya ulaji ndani ya CCM kwa muda mrefu walihisi zamu yao isingeweza kufika hivi karibuni kwa hiyo wameamua kujiunga na upinzani ili kufupisha urefu wa foleni ya ulaji.
  Wasicho jua ni hiki. Safari hii ndani ya upinzani kutakuwa kuna kula na kupiga Tindo ili kujenga kesho na keshokutwa. Kujilimbikizia mali kutategemeana na nguvu ya kubuni mikakati ya kuzarisha zaidi na si ufisadi

  Kuendelea kuongelea utendaji kwa mtindo wa kiCCM
  Ni sawa kabisa na mtu ajiitaye mlokole,aliyekata shauri kumfuta Yesu na kukataa kila aina ya dhambi, kisha kila apitapo demu Bomba na Sketi fupi hukata jicho kali la tamaa kisha kwa unafiki hugeuza shingo yake upande mwingine kujifanya hakuyatamania mapaja yale na baadaye kugeuka na kukodolea mimacho kwa nyuma huku amelegea kwa mtindo wa mbweha aliye likosa windo wazi wazi. Mlokole Mwngine aonapo bango lenye Glass ya Serengeti ikiwa na Jasho la ubaridi hujificha uso wake kwa kiganja kwani moyoni na kooni bado yu atamani radha ya Bia.

  Uadilifu siku zote ni aghali sana. Watu waadilifu ni watu wanaojitolea kwa sababu tu wanaamini uadilifu una thamani kuliko maburungutu yote ya fedha, pia wanaamini kwamba uadilifu hujenga jamii yenye utajiri katika kila sekta.

  Kwanza jiulize,CHADEMA wakifuata nyayo za CCM kutanguliza fedha mbele tofauti yao na CCM itakuwa nini??
  Pili Jiulize, Fedha ya kulipa mawakala wote wa CCM, CCM wameitoa wapi?? Bunge likitaka kujua source za fedha yao wako tayari kuiweka wazi??

  Hisia Machale na Pekuapekua yetu inadhihirisha hivi;

  CCM wakiingiza mikono yao mirefu, ya KIJITUJITU, katika mifuko ya kaptula zao kutoa fedha, mifuko yao ina mahandaki marefu yanayopitiliza mpaka kwenye Hazina Kuu ya Taifa. Kifupi wanaiba sehemu kubwa ya makusanyo ya kodi ya wananchi wote Tanzania kufinance shughuli binafsi za Chama chao bila ridhaa ya Watanzania na pia kwenda kinyume na sheria ya vyama juu ya fedha.
   
 11. R

  Rugemeleza Verified User

  #11
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni kweli tunahitaji watu wanaojitolea zaidi ya kulipwa pesa. Hapa Marekani wanaolipwa ni wafanyakazi wa ndani ya kampeni na ndio gharama za uchaguzi huhesabika. Lakini kiukweli kazi kubwa inafanywa na wanaojitolea ambao hata mgombea hataweza kuwafahamu. Hivyo ni jukumu la Chadema kujenga vikundi vya wajitoleao ili kuweza kujenga chama madhubuti cha kila mtaa, kitongoji, kijiji, mkoa na Taifa. Historia ya nchi yetu katu kamwe haitakuwa kama ya miaka 25 iliyopita.
   
 12. GFM

  GFM JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Can not agree more ..............
   
 13. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #13
  Nov 2, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280

  hizo bilioni TATU CHADEMA kingezizaa wapi ......mkuu kama sio ndoto !!! ni pesa nyingi hizo....CHADEMA Walitegemea mawakala wengi wakiwa ni wanafunzi wa vyuo vikuu waliojitolea ....baadhi kwa mapenzi tu tena bila senti....CCM iliwalipa kila wakala wao laki moja!!

  kama sio mawakala wa chadema hata hivyo viti 30 walivyopata wasingepata..watu jifunzeni kuwa na shukrani kwa walio jitolea...chukulia mtu kama sugu ....alikuwa na pesa gani ya kumlipa mawakala kumshinda mpesya.....vijana wamejitolea tu!
   
 14. GFM

  GFM JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Smell like CCM shit ............ kama ni kujitafutia kipato basi CHADEMA ingeshindwa kote, kwa kuanzia ingekuwa Arusha ambako EL alitaka
  kupenyeza rupia lakini ikakataliwa ............
   
 15. kijanamakini

  kijanamakini Senior Member

  #15
  Nov 2, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  i am with u pal. Pesa si zaidi ya uhuru wa nchi hii....!!!! Mimi ni kijana, nimeshakata tamaa na nchi hii, but am not giving up yet....CCM ni wizi wizi mtupu//!!!!
   
 16. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #16
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Suala la ukombozi especially kwetu sisi watanzania hatuhitaji kulipwa. This is for the sake of our next generation. Sihitaji hata senti moja for CHADEMA or chama kingine chenye mwelekeo wa kumpunguzia mtanzania mizigo na ukali wa maisha. Ndiyo maana hapo awali wakati wa kampeni nilitoa mchango wangu katika kuhakikisha tunamuumbua aliyekuwa anasambaza SMS za kumchafua Dr. Slaa. Sikuomba pesa wala udiwani na ninajivunia kwa kile nilichokifanya. Hata usalama wa Taifa wanaelewa hilo upinzani nao wana wataalamu wazuri wa IT lakini wapenda AMANI kuliko hao akina Miraji na genge lake.
   
 17. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,993
  Likes Received: 1,001
  Trophy Points: 280
  Mkuu umegonga penyewe.

  "Mkono wa birika umeigharimu Chadema chaguzi hii" unaamanisha chadema walikuwa na pesa wakakataa kuzitumia,sasa wewe tueleze chadema wanakiasi gani wakabania kuzitumia kwenye uchaguzi, kwa sababu mimi ninavyojua chadema ilikuwa na hali mbaya kifedha ndio maana wakaomba watu wachangie katika ya kampeni.

  Inabidi tukubaliane na hali ilivyokuwa,kwenye fedha tusiwalaumu chadema kabisa.Chadema hawawezi kujilinganisha na ccm,hatujui hizo pesa wanachota wapi. Hata kama Chadema ingeweza kuwalipa mawakala wake kila mmoja laki, ccm ingeweza kuongeza kuwalipa mawakala wake laki tano iliwaweze kuwarubuni wa upinzani na bado tungelalamika kwanini Chadema wamewalipa mawakala wake pesa kidogo.Mimi naona uwakala bado ibakie ni kitu cha kujitolea.
   
 18. Madago

  Madago Senior Member

  #18
  Nov 3, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama ingekua kwa sababu ya pesa wala tusingepoteza muda wetu huku. Huu ushenzi wa kudai posho Tena umeanzia serikalini hasa wakati wa mkapa. Idara nyingi za serikalini zilipata mafungu wakawa wanashindwa lkuzitumia ipasavyo ndio watu wakaanza kujilipa mara imtindo ukasambaa, ilhali watu mishahara wanapewa. Ugonjwa na tabia hii ukijumlisha na umaskini wa watu ukashika kasi mpaka vijijini. Maendeleo ni pamoja na siasa safi, Kama mchonga alivyoiweka huko zamani.
   
 19. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #19
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nasikia harufu ya "michango" mingi halafu watu kula kona! Hivi zile hela zote za ma-Conservatives wa Uingereza mlizopewa zimetumika wapi vile?
   
 20. Bob_Dash

  Bob_Dash Member

  #20
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 91
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Du! mlisha anza kuleta habari za vijiweni hapa, sioni kama kuna ukweli wowote kuhusiana na hilo.
   
Loading...