Mkono asalimu amri baada ya kukatwa wazazi CCM

Mkono kawaona Mwakyembe, Mwandosya, Ulimboka na Mwangosi walivyofanywa. Its not wealth, karudisha majeshi
 
'Bado tu nitakuwa muaminifu kwenye chama', yanatoka moyoni kweli?
 
MKONO, ulikuwa unamtishia nani? Ulidhani wewe mbabe kiasi cha ulivyokuwa unasema? Unaanzisha vita ya mawe na hali unaishi kwenye nyumba ya vioo? Unaanzisha vita bila ya kujua uimara wa jeshi na bunduki na risasi zako? Hongera sana Mr Chairman of Ccm mabwepande kwa kukata ngebe za wanaokutishia katika kiti chako kitukufu.
 
Sina hakika hawa jamaa wa ccm wanakibilia vyeo na madaraka kwa nia ya kumkomboa mtz wa kawaida!!!!
 
Dogo hamjui Mkono si unajua tena JF ni bahari inasomba kila kitu.

Ameshirikishwa dili nyingi sana zilizopangwa kisheria na kukwapua mapesa chungu nzima! Hajanywea bure, dhamira yake inamsuta!

Msiniulize ni dili gani, mkopi kisha mpesti kwenye medulla.
 
Ni kweli hamjui. Alitakiwa aseme kwamba Atulie tu Atalindwa. Akithubutu kufanya fyoko tu ataozea Segerea kwani Ufisadi alioufanya pale BOT wanaumezea kwa sasa kwa kuwa tu ni mwenzao.
 
Maneno ya mkosaji aliongea mwenyewe hatakubali kama jina lake litaondolewa sasa anajikana mwenyewe,tapatapa za sisiemu,
 
Ule ulikuwa ni mkwara tu, akileta kujua naye anaweza kuozea jela kutokana na ufisadi.
 
mkono ndio tunasema wazee waliopata laana ndani ya ccm lakini hawajui kama wananchi walisha walaani. Busara za mzee kama mkono ni janga kwa taifa maana hana maamzi kama yeye bali anafuata nini ccm inasema niuoga wakutokutumia akili yake bali ya kundi fulani.
 
Vigeugeu, ndumilakuwili ndiyo kina mkono!!! Kwanza taaluma yake ilikuwa inampa heshima sana!!! Sijui kwa makidai yake kama ataweza tena kutamba maana nyodo zilimzidi baada ya kupata mihela ya kesi za BOT na zile za TANESCO!!!!! Amekula hii nchi sana. Rudi Mkono Advocates mzee ili uzeeke salama.
 
Kuhusu kauli yake ya hapatatosha/hapatatchimbika siwezi kuisemea, lakini ninamuunga mkono Mkono kwa kubakia ndani ya chama chake.

Nyerere aliwahi kusema kuwa upinzani mzuri ndani ya CCM utatoka ndani ya CCM, tatizo letu ni kuwa demokrasia yetu haijakua kiasi cha kuwavumilia "wapinzani" [wa vyama vyetu] ndani ya vyama vyetu. Hawa lengo lao sio kukiua chama bali kukijenga na kukirejesha katika mstari pale kinapotokea kupotoka, kama walivyo wapinzani wa nje kwa serikali.

Mkono anaweza kuwa mpinzani wa chama ndani ya chama chake, na hii ni faida hata kwa vyama vya upinzani. Akiondoka au wakiondoka wale ambao wanauthubutu wa kuikemea CCM, itazidi kiburi na kuendeleza madudu.
 
Back
Top Bottom