Mkono akubali kufukuzwa CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkono akubali kufukuzwa CCM!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwitongo, Jun 5, 2012.

 1. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wana JF, nimekutana na hii katika Gazeti Jamhuri la leo katika website yao. Inaonekana Mkono anajiandaa kuvaa Gwanda!!!! Peopleeeeeeeeees!!!!


  Mkono akubali kufukuzwa CCM

  *Apata wasiwasi kuwa Nyerere aliuawa wakubwa waharibu mambo
  *Filikunjombe asema wabunge ni wanafiki, yuko tayari kufukuzwa
  *Nape asema vikao vipo, NEC yawatwisha mzigo wabunge wa CCM

  Na Waandishi Wetu

  Hali ya mambo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inazidi kuwa mbaya, baada ya mmoja wa makada na wafadhili wake maarufu, Nimrod Mkono, kusema yupo tayari kufukuzwa uanachama.

  Hatua hiyo ya Mkono imekuja baada ya kuwapo tetesi kwamba wabunge watatu wa CCM - Mkono (Musoma Vijijini), Deo Filikunjombe (Ludewa) na Alphaxard Lugola (Mwibara), kuweka saini kwenye fomu yenye kusudio la kutaka kumng'oa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

  Mkono ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, ameiambia JAMHURI kwamba yupo tayari kwa lolote, ikiwa ni pamoja na kuvuliwa gamba kama itaonekana kuwa uamuzi wake wa kusaini ulikiuka misingi.

  "Siwezi kubadili msimamo, heri nife kuliko kuunga mkono Serikali inayoiba, maana pale katika Mgodi wa Buhemba iliyoiba ni Serikali… imeondoa kila kitu na kuacha mashimo," alisema kwa hisia kali na kuongeza:

  "Kwangu mimi haina faida kuwa mbunge kama kuna mambo ya kuwaumiza wananchi. Mimi ni mbunge wa wananchi wa Musoma Vijijini, natetea masilahi yao, sasa kama wanataka kunifukuza kwa kuwatetea wananchi, wanifukuze, nipo tayari. Chochote waamue, nipo tayari kabisa."

  Amesema yeye na wabunge wenzake waliosaini fomu ya kumng'oa Waziri Mkuu walifanya hivyo kwa nia njema ya kuleta uwajibikaji serikalini, na kwamba huo ndiyo uliokuwa msimamo wa wabunge wengi kwenye kikao cha Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (party caucus).

  "Watuvue magamba, mimi nipo tayari kuvuliwa gamba, hatuwezi kwenda hivyo. Katika party caucus tulikubaliana tuiwajibishe serikali. Mimi kila mahali naongea Buhemba, Buhemba, Buhemba. Kwenye vikao vya chama nazungumzia Buhemba, Kyarano, lakini hawasikii. Sasa kama hawanisaidii kumaliza hizi kero za wananchi, nikae kwenye chama kinisaidie nini?" Amehoji.

  Kyarano ni bwawa lililochimbwa kwa maelekezo ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwanzoni mwa miaka ya 1980 kwa ajili ya shughuli za kilimo cha umwagiliaji. Lipo katika mpaka wa vijiji vya Butiama, Bisarye na Rwamkoma.

  Mkono amesema; "Kila mara nazungumzia Buhemba kuwa dhahabu imechukuliwa, majengo na mitambo vimeibwa kwa usimamizi wa polisi na maofisa wa serikali. Kyarano imekufa. Vitu vya Mwalimu vimeharibiwa, nina faida gani?"

  Mbunge huyo amekwenda mbali zaidi kwa kusema huenda ikawa kweli kwamba Mwalimu aliuawa kama alivyodai Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere, kwa sababu mambo mengi aliyoyasimamia Mwalimu yameachwa yafe.

  "Nawaeleza hawaendi Buhemba, hawaendi Kyarano, maji Butiama hakuna, hawaendi…ndiyo kauli yangu hiyo kwamba kama wanataka kunifukuza, basi wanifukuze. Mimi ni mbunge, nimeyazungumza haya mara zote kama mbunge na si kama mhuni. Huo ndiyo msimamo wangu na sijawahi kuyumba. Kama wanataka kunifukuza, sawa!" amesema.

  Kauli ya Nape kuhusu Mkono

  Kauli ya Mkono ya kutamka wazi kwamba yupo tayari kufukuzwa kutoka CCM imemshitua Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye.

  Alipoulizwa kama chama hicho kipo tayari kumpoteza mwanachama na mfadhili mahiri kama Mkono, Nape alianza kwa kukosoa taarifa zilizoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema zinalenga kuibua mjadala usiokuwapo.

  "Nani kasema watahojiwa? Hoja hii ni kweli iliibuliwa kwenye kikao cha NEC kwa baadhi ya wajumbe kuhoji kwamba ilikuwaje wabunge wa CCM wakasaini kumng'oa madarakani Waziri Mkuu! Lakini tukaona kuwa hii ni hoja ya bungeni, na huko kuna party caucus. Uongozi wa Kamati ya Wabunge wa CCM upo, na haujatupatia taarifa rasmi kama kuna watu wamevunja kanuni.

  "Tukasema kama wanaona kuna uvunjaji kanuni watujulishe. Nasema hii hoja inatengenezwa makusudi. Kama kulikuwa na tatizo, basi party caucus watatujulisha, lakini hadi sasa hatujapata taarifa rasmi. Wale wana kanuni zao za wabunge, kama wanaona kuna jambo linahitaji kufikishwa ngazi za juu wanalileta," amesema.

  Alipoulizwa kama chama kinaweza kumwadhibu Mkono na wenzake, alisema, "Sipendi kuzungumzia mtu, hapa tunajadili kanuni na sheria. Tunaendesha chama kwa kanuni, sheria na taratibu, kama sheria zinasema Nape kakosea pamoja na umuhimu wake, sheria zitafuatwa. Nakuhakikishia katika hili hatujapata taarifa."

  Nape: Maige si saizi yangu

  Katika siku za karibuni, Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM), amenukuliwa akisema kwamba Nape ni gamba ndani ya CCM na anapaswa kuwajibishwa. Kwa upande wake, Nape amejibu mapigo kwa kusema, "Maige si saizi yangu, ni mbunge, atajibiwa na (CCM) wilaya yake. Nadhani wameshaanza kumjibu."


  Filikunjombe: Wabunge hawafai

  Kwa upande wake, Filikunjombe alipowasiliana na JAMHURI alisema yeye yuko tayari kufukuzwa kutoka CCM kama chama hicho kitamhukumu kuwa alifanya kosa kwa kutia saini azimio la kumg'oa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ila akasema uamuzi wa aina hiyo utamshangaza mno na unathibitisha unafiki wa wabunge wa CCM.

  "Nimesikia walijadili suala hili kwenye NEC na Rais Kikwete akasema vikao vipo vingi, suala hili lipelekeni kwenye vikao husika kama party caucus bungeni.
  "Mimi nasema sijutii uamuzi wangu. Tena nasema kama wapo wa kufukuzwa kutoka CCM ni wale waliokataa kusaini ndiyo waadhibiwe, kwa sababu huo ndiyo uliokuwa msimamo wa chama. Asilimia 90 au 95 ya wabunge walikuwa wanalalamika na tukakubaliana hivyo.

  "Ajabu; ilipofika wakati wa kusaini daftari wengine wakawa wanalipita kama hawalioni. Wabunge wengi ni wanafiki sana. Ndiyo; tunapaswa kuwa na nidhamu lakini nidhamu ya woga haifai. Dhamira yangu iko safi kabisa, kwa hili nipo tayari kufukuzwa katika chama.

  "Pamoja na kwamba ninaheshimu uamuzi wa vikao, ukweli utabaki pale pale kwamba nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko.

  "Hawa waliokataa kusaini ndiyo wa kufukuzwa maana walikuwa wanataka chama kianguke na serikali yake. Sasa itakuwa ajabu sisi tulioitetea serikali isiangushwe - tena serikali ya chama chetu - ndiyo tufukuzwe sitaelewa ila nipo tayari hata leo," amesema Filikunjombe.

  Wabunge hao watatu waliungana na wabunge wa vyama vya upinzani vya Chadema, CUF, TLP na UDP kusaini azimio la kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lililoandaliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

  Baada ya hatua hiyo, Serikali ililazimika kufanya mabadiliko makubwa kwenye Baraza la Mawaziri na mawaziri wanane na manaibu wawili kutupwa nje ya ulingo.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,383
  Trophy Points: 280
  Mkapa anayo kesi ya kujibu kuhusu kifo cha mwalimu
   
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  movie bado linaendelea
  mda sio mrefu yataibuka mengi yatakayopelekea wabunge wa CCM kupigana hadharani live
  na kuanika uozo wa kila mmoja wao.
   
 4. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mpaka 2015 tutakuwa tumeshudia mengi makubwa,lets wait and see!
   
 5. T

  Topetope JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 273
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Tulisema nyerere ali thulumiwa nafsi watu wapo walio husika
   
 6. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Unajua ukitaka kuwagombanisha wanafiki, basi mwonjeshe mmoja wao utamu wa ukweli. Awamu hii haitapita kabla utabiri wako haujatimia
   
 7. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Serikali itoe tamko juu ya kifo cha mwalim kama ambavyo mh. Vicent alivyosema kwa niaba ya familia ya mwalimu... utata umezidi kutanda Pro Mwakyusa anaweza kutusaidia juu ya hili
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sasa kama walianya makosa kusign mbona JK alifanya reshuffle ya cabinet?
  Huu ni unafiki wa wabunge wa CCM kama 90% walisupport kimoyo moyo bila kusign si ndo unafiki na woga wa kitoto.
  Big up Mkono na Deo aluta continuaaaaaaaaaaaaa
   
 9. c

  cicy Member

  #9
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  watu wa musoma wameamuka sasa wanataka kujua nini kimemua nyerere mhhhh
   
 10. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Mwitongo taarifa yako ni nzuri, asante. Umesema Mb. Mkono anajindaa kuvaa gwanda binafsi sijaona ni wapi amesema kuvaa gwanda zaidi yakusema yuko tayari kufuzwa ama kuvua gamba. Hii ni siasa mpaka 2015 tutashuhudia na kusikia mengi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. samstevie

  samstevie JF-Expert Member

  #11
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Nani kasema watahojiwa? Hoja hii ni kweli iliibuliwa kwenye kikao cha NEC kwa baadhi ya wajumbe kuhoji kwamba ilikuwaje wabunge wa CCM wakasaini kumng'oa madarakani Waziri Mkuu! Lakini tukaona kuwa hii ni hoja ya bungeni, na huko kuna party caucus. Uongozi wa Kamati ya Wabunge wa CCM upo, na haujatupatia taarifa rasmi kama kuna watu wamevunja kanuni.


  Kumbe wabunge wa CCM huwa na maamuzi na msimamo wa pamoja hata kwa taratibu zinazoangamiza nchi. wanapaswa kuwajibishwa wote BTW Filikunjombe, Mkono na Lugola wameona mahali penye mwangaza bora wa kisiasa (si CCM) mbele ya maisha yao.
   
 12. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,672
  Trophy Points: 280
  Wafa maji hawaachi kutapatapa.
   
 13. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,943
  Likes Received: 1,268
  Trophy Points: 280
  Mkwapa kaua
   
 14. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Tumewasikia na tunasubiri kama kweli wana nia njema basi na waipige ccm chini
   
 15. B

  Babuu Rogger JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 80
  Kaaazi kwelikweli.
   
 16. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wewe unadhani mwana ccm akivuliwa gamba kuna sare gani inayomfaa zaidi ya gwanda? kumbuka ilishasemwa kwamba Mkono alimsaidi Vincent Nyerere kuitwaa Musoma kutoka kwa Manyinyi!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. M

  MZALAMO JF-Expert Member

  #17
  Jun 5, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 471
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 60

  Huwa mwepesi wa kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake lakini katika hili la kifo cha mwalimu sijasikia kauli yake tunamuomba sasa ajibu hizi tuhuma. Waandishi wa habari tusaidieni kumuuliza mheshimiwa sisi wananchi tuko njia panda.
   
 18. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #18
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Siwezi kuzungumza/andika kwa kudhani Mkono ama yeyote wa siasa si lazima atoke chama kimoja kwenda kingine mwingine aweza kuamua kufanya shughuli zake binafsi, maadamu hajasema kuvaa gwanda basi tusimlishe maneno kwa taarifa za ukanjanja.
   
 19. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  " ugomvi ni dhahabu ktk nyumba ya wapumbavu"
   
 20. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #20
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Wito kwa wabunge wa CCM wanao ambao wamechosgwa na mfumo mbovu wa CCM. Muda wa kuondoka kishujaa ni sasa. Msingoje 2015. Ninaamini kabisa uchaguzi ukirudiwa mtachaguliwa kupitia chama makini cha upinzani. Ninajua kuna gharama ya uchaguzi lakini tujue kila kilicho kizuri kina gharama zake. Badala ya kungojea ufukuzwe ni bora kujiuzulu.
   
Loading...