Mkono akubali kufukuzwa CCM!

Siwezi kuzungumza/andika kwa kudhani Mkono ama yeyote wa siasa si lazima atoke chama kimoja kwenda kingine mwingine aweza kuamua kufanya shughuli zake binafsi, maadamu hajasema kuvaa gwanda basi tusimlishe maneno kwa taarifa za ukanjanja.

Toa mfano wa aliyejivua gamba akabaki akifanya shughuli zake! Ukishaingia katika siasa ni kama umeshaingia kwenye wanga!! Huwezi kuacha kuwanga eti kwa sababu uko ugenini! Mkono ni peopleeeees!
 
Serikali itoe tamko juu ya kifo cha mwalim kama ambavyo mh. Vicent alivyosema kwa niaba ya familia ya mwalimu... utata umezidi kutanda Pro Mwakyusa anaweza kutusaidia juu ya hili

Kaka haitatusaidia sana hii je tukijua walimwua ndio tutamfufua yule mzee wa busara??? To me this is nonsense
 
Toa mfano wa aliyejivua gamba akabaki akifanya shughuli zake! Ukishaingia katika siasa ni kama umeshaingia kwenye wanga!! Huwezi kuacha kuwanga eti kwa sababu uko ugenini! Mkono ni peopleeeees!

Hapo ndo napotofautiana nawe wa Mwitongo tusidhani kwa mazoea tu maadamu hajasema kwanini tusivute subira? kuliko kumpandisha imani?
 
Last edited by a moderator:
Nafikiri suala la unafiki wa wabunge wa CCM, Nape kaongea vizuri.

Wabunge hawa wame nymazia vitu vingapi vya kijinga bungeni na kuwaacha wabunge wa Chadema wakihangaika peke yao!

Hizi zisije kuwa njama za kutafuta nafasi za kazi chadema baada ya kuona CCM 2015 HASHINDI!
 

Wabunge hao watatu waliungana na wabunge wa vyama vya upinzani vya Chadema, CUF, TLP na
UDP kusaini azimio la kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lililoandaliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

Baada ya hatua hiyo, Serikali ililazimika kufanya mabadiliko makubwa kwenye Baraza la Mawaziri na mawaziri wanane na manaibu wawili kutupwa nje ya ulingo.
Ni mbunge gani wa UDP aliyesaini azimio hilo?

Anyway, Mkono atuunge mkono Zitto atakapowasilisha azimio hilo kikao kijacho cha bajeti. Sababu za kuing'oa serikali bado zipo nyingi. Wezi wa EPA hawajafikishwa mahakamani, wezi wa dhahabu ya Buhemba (MEREMETA) Pinda kagoma kuwataja kwa madai kuwa ni siri ya serikali, waliotutia hasara kwenye ukodishaji ndege za ATC hatujaambiwa wamechukuliwa hatua gani nk. Tuunge mkono mheshimiwa Mkono.
 
Naiona Tanzania Mpya siku chache zijazo. Na bado itabidi Mkapa na Mwakyusa watueleze ukweli wote kwenye hili hakuna haja ya kubebana na kuficha uweli kwenye hili.
 
Wito kwa wabunge wa CCM ambao wamechowa na mfumo mbovu wa CCM: Muda wa kuondoka kishujaa ni sasa. Msingoje 2015. Ninaamini kabisa uchaguzi ukirudiwa mtachaguliwa kupitia chama makini cha upinzani. Ninajua kuna gharama ya uchaguzi lakini tujue kila kilicho kizuri kina gharama zake. Badala ya kungojea ufukuzwe ni bora kujiuzulu.
 
Hapo ndo napotofautiana nawe wa Mwitongo tusidhani kwa mazoea tu maadamu hajasema kwanini tusivute subira? kuliko kumpandisha imani?

Kuna ubaya gani nikiwa msemaji wa Mkono? Mbona Salva Rweyemamu anamsema JK! Dalili ya mvua ni mawingu. Mkono atavaa gwanda muda si mrefu! stay tune!!!
 
Last edited by a moderator:
Hata hao akina Mkono na Fulikunjombe nao ni wanafiki tu,yamesemwa mengi juu yao, hata Nape amekiri kuwa hiyo hoja iliibuka katika NEC, wanataka ushaidi gani tena, kama wan nia ya dhati kweli na kupambana na ufisadi, jitoeeni kwenye hicho chama cha mafisadi sio eti mnasubiri wawafukuze!

Ajabu kweli ni jinsi gani Mkono na Fulikunjombe mnaweza kusukuma gari wakati mko ndani ya gari hilo hilo? Shukeni chini, lisukume, nawahakikishia linasukumikika, liko nyanganyanga wakati huu,gear na breki zote kwishineri!
 
movie bado linaendelea
mda sio mrefu yataibuka mengi yatakayopelekea wabunge wa CCM kupigana hadharani live
na kuanika uozo wa kila mmoja wao.

Nimesoma blog ya Shigongo wanasema Freemason wataichukua dunia mwaka huu mwishoni.
Natamani iwe kweli ili nisiione hii aibu ya CCM kutiana visu vya migongo mchana kweupe.

Mkono ana siri nyingi za CCM na Serikali maana amekuwa anafanya nao kazi mda mrefu. Sasa kama na yeye amechoka!!!! Ngoja bunge la bajeti lianze nahisi CCM watawafunika CHADEMA kwa kuipiga mawe serikali hasa ukizingatia mawaziri wengine watakuwa wanatetea wizara zao wakati hata kiapo cha ubunge hawajakitafuna.

Tutakuwa tunafaidi ngumi mchana Bungeni na usiku tunakula football ya EURO. Raha TUpuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Mpaka 2015 tutakuwa tumeshudia mengi makubwa,lets wait and see!

wataumbuana sana tusubiri tuone makubwa yaja.......... mkuu mimi naona ndo muda muafaka wa laana za BABA yetu wa taifa zinaanza kufanya kazi....OOOOH JESUS ahsante mungu wezi waanze kuumbuana
 
Hapo patamu tunasubili ukombozi na watatafuta nafasi wakati tumeshajaa njooni mapema mliowasafi.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom