Jamani mie nashangaa sana kuhusu hii serikali yetu ya Tanzania, nakumbuka hapo nyuma walitutangazia wananchi kwamba mkongo wa taifa ukikamilika gharama za mawasiliano ya kiilektroniki zitashuka. Sasa nashangaa kuona gharama za matumizi ya vifaa hivyo yanazidi kuongezeka zaidi kuliko hapo nyuma. Au mkongo huo uliishia wapi? Naombeni ufafanuzi wa jambo hili kwa anaelifahamu kwa kina zaidi.