Asante Mungu,Bwana wetu kwa muda huu. Ninasogea mbele zako kwa unyenyekevu. Mungu nisamehe dhambi zangu zote. Mungu nisafishe kwa damu ya Mwano Yesu Kristo. Mungu Baba naomba kibali chako kukomesha uongo na ila zote za shetani na matendo yake na yeye mwenyewe. Asante Mungu kwa kunipa kibali. Uongo, ila zote za shetani na matendo yake na yeye mwenyewe shetani vyote ni magugu, tena magugu makavu sana. Magugu haya nayafunga pamoja. Kwa jina la Yesu Kristo, Mungu wetu aliyeziumba mbingu na dunia tena kwa kupitia Roho Mtakatifu ninawasha moto magugu haya. Nina hakikisha magugu yote yamepata moto. Kwa msaada wa Roho Mtakatifu magugu haya yote yaliyoshika moto nayatumbukiza kwenye ziwa la moto lilo chini sana kuzimu. Na joto la ziwa hilo lisipate tena kuifikia Dunia tunamoishi. Na huo ndiyo mwisho wa magugu haya. Asante Mungu kwani unaenda kudhibitisha maombi yangu kama ulivyonielekeza kuwa kwa kila aombaye atapewa na abishaye hodi atafunguliwa. Ni katika Jina la Yesu Kristo nina Amini utatenda. Amen.