Mkoko huu unalipa si mchezo

Cassava

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
282
36
Wadau za leo, katika kuhangaika nimebahatika kukusanya kiasi na sasa nataka na mimi nipumzike kutembea kwa miguu safari ndefu za mjini. Kwa ufupi nataka kununua mkoko. Nimetembelea website za kuuza mikoko nikakutana na mkoko aina ya [h=1]"Toyota Voxy" wa mwaka 2002, Unauzwa TShs. 6,500,000/- DUTY NOT PAID, Umetembea kilometa 98000, Unatumia petrol na ingine size ni 2000cc, Wauzaji wanasema uko ready to be imported.

Sasa wadau mwenye kujua MIKOKO na uagizaji kwa ujumla, naomba kujua kama huo mkoko unauzwa hiyo bei (6.5M), je, ili niuweke barabarani kabisa natakiwa kuwa na shilingi ngapi?

Mimi siyo mzoefu naomba mnipe ushauri na pia naomba mwenye kujuwa waagizaji waaminifu ambao sitazungushwa zungushwa sana.

Naomba pia kujuwa lipi jema kuagiza kutoka Japan au kwenda show room na kutungua? Je ukienda show room maswala ya TRA na malipo mengine inakuwa nafuu?
[/h]
Naomba mwenye kuelewa anisaidie.

Wenu Mdau.
 
Kama gari liko nje ya nchi na inabidi liletwe hapa nchini, roughly, ongeza kama robo tatu ya hiyo bei, itacover mazagazaga mengine yote including bima na road licence, registration etc na mkoko utakuwa wako
 
Ni vizuri pia kujua kama bei uliyoitaja ni FOB or CIF. Kama ni FOB, tafuta kujua CIF yake ndiyo ufanye makisio kamili.
 
Wadau za leo, katika kuhangaika nimebahatika kukusanya kiasi na sasa nataka na mimi nipumzike kutembea kwa miguu safari ndefu za mjini. Kwa ufupi nataka kununua mkoko. Nimetembelea website za kuuza mikoko nikakutana na mkoko aina ya [h=1]"Toyota Voxy" wa mwaka 2002, Unauzwa TShs. 6,500,000/- DUTY NOT PAID, Umetembea kilometa 98000, Unatumia petrol na ingine size ni 2000cc, Wauzaji wanasema uko ready to be imported.

Sasa wadau mwenye kujua MIKOKO na uagizaji kwa ujumla, naomba kujua kama huo mkoko unauzwa hiyo bei (6.5M), je, ili niuweke barabarani kabisa natakiwa kuwa na shilingi ngapi?

Mimi siyo mzoefu naomba mnipe ushauri na pia naomba mwenye kujuwa waagizaji waaminifu ambao sitazungushwa zungushwa sana.

Naomba pia kujuwa lipi jema kuagiza kutoka Japan au kwenda show room na kutungua? Je ukienda show room maswala ya TRA na malipo mengine inakuwa nafuu?
[/h]
Naomba mwenye kuelewa anisaidie.

Wenu Mdau.

hiyo bei ni cif or fbo? Hebu angalia web ya chekicheki.google toyota voxy.chekicheki.tanzania kuna mikoko ya bei rahisi kabisa kwa kwa tz money nabei yao wanakuwa wameiweka kwa cif. .
 
Cha muhimu tafuta kama wanayo option ya inquiry maana mitandao mingi wanayo hiyo,
Then utatakiwa kujaza jina lako, bandari utakayotumia, email n.k.
Then watakutumia estimated price/cost mpaka ifike bandarini including inspection.
Sasa mkuu TRA ni kama ramli flani hivi ambapo kodi yao hua haiko specific kivile. Sometimes wanaangalia Invoice na vilevile wanazo bei zao kwa kila gari.
Nishwahi kuagiza gari 2 zilizofanana katika vipindi tofauti nikachajiwa kodi tofauti.
 
Utakuwa poa tu ILA angalia kampuni inayokuuzia ucje ingia kwa wanigeria wakakuingiza mjini, above all km ni kama nyingi vile but usijali weka barabarani. Hakuna tax exemption so unaweza kutakiwa kukusanya cha juu kingine kwa ajili ya ushuru ili uuingize town.
 
By the time unaingiza hiyo gari nchini itakuwa imefikia miaka 10 tangu manufacture date yake. Ongezea na kodi hiyo pia.

Halafu 2000 cc engine size ikiwa unakaa bunju na unakwenda mjini kazini basi jitayarishe kwa bajeti nzuri ya petroli.
 
BF32459
TOYOTA
VOXY
2002/101,990ccRightAutomatic113,329 $3,600
$3,334

¥270,000
¥250,000

hii ipo BEFORWARD JAPAN NI KAMPUNI AMBAYO MIMI NIKIAGIZA GARI NALALA USINGIZI SAFI SINA WASIWASI WA KUTAPELIWA AMA KULETEWA GARI AMBAYO HUKUICHAGUA
 
Bei mpaka Dar es salaam (CIF) ni us d 5133
kazi kwako MHOGO
 
Bei mpaka Dar es salaam (CIF) ni us d 5133
kazi kwako MHOGO

WAdau wote nawashukuru kwa michango yenu, ndiyo maana naipenda JF, ila huwa napata shida sana nikisoma habari za siasa. Kuna siku huwa zinaumiza sana.
 
Back
Top Bottom