Shirika la afya duniani inaeleza kutokana na uwepo wa tiba mbadala ambayo hutumika kwa wingi zaidi nchini Saudi Arabia ambapo moja ya desturi za kawaida ni matumizi ya mkojo wa ngamia peke yake au kuchanganywa na maziwa ya ngamia kwa ajili ya kutibu saratani, jambo ambalo mara nyingi huungwa mkono na imani za kidini.
Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa na
WHO "Use of camel urine is of no benefit to cancer patients: observational study and literature review" Mkojo wa ngamia haukuonesha faida yoyote ya kitabibu kwa wagonjwa wowote wa saratani, na huenda hata ulisababisha maambukizi ya magonjwa ya kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu. Uhamasishaji wa mkojo wa ngamia kama tiba ya jadi unapaswa kusitishwa kwa sababu hakuna ushahidi wa kisayansi unaounga mkono matumizi yake.
Wagonjwa wote waliofanyiwa uchunguzi wa radiolojia kabla na baada ya matibabu yao kwa kutumia mkojo wa ngamia. Wote walitumia mchanganyiko wa mkojo wa ngamia na maziwa ya ngamia, na muda wa matibabu ulianzia siku chache hadi miezi 6. Walitumia wastani wa mililita 60 za mchanganyiko wa mkojo/maziwa kwa siku. Hakukuonekana faida yoyote ya kitabibu baada ya matibabu; wagonjwa 2 walipata brucellosis, maambukizi ya bakteria yanayotoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kupitia matumizi ya maziwa yasiyochemshwa, nyama isiyopikwa vizuri, au kwa kugusana na majimaji ya wanyama walioambukizwa.
Wagonjwa kumi na mmoja walibadilisha mawazo na kukubali matibabu ya kawaida ya kupambana na saratani, na wagonjwa 7 walikuwa dhaifu sana kupokea matibabu zaidi; walifariki kutokana na ugonjwa huo.
Lakini baadhi ya
tafiti (
Is camel’s urine friend or enemy? Review of its role in humanhealth or diseases)zinaeleza kuwa msingi wa kidini wa matumizi ya mkojo wa ngamia katika matibabu unatokana na imani kwamba kuna ushahidi unaoaminika kuwa Mtume Muhammad (SAW) alishauri kutumia mkojo wa ngamia kutibu maumivu ya tumbo wakati huo. Mkojo wa ngamia unasemekana kuwa na sifa za kupambana na kisukari, saratani, bakteria, virusi na fangasi. Pia unasemekana kuwa na athari za kulinda ini (hepato-protective) na kuboresha afya ya mfumo wa moyo na mishipa ya damu.