Mkoa wa Ruvuma: CCM bado ina nguvu kubwa; CHADEMA yaimarika, CUF yafifia; ACT-Wazalendo yachomoza

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Ni matumaini yangu kuwa kichwa cha habari hii kinatoa tahmini ya jumla juu ya mkoa huu wa Ruvuma. Niko hapa kwa takribani juma moja katika kufanya tathmini binafsi ya kisiasa kuelekea Oktoba mwaka huu. Nimepita Songea na Mbinga; Nikaenda Tunduru na Namtumbo; nikasonga hadi Peramiho na sasa niko Nyasa. Hiyo ndiyo hali halisi.

Mkoa huu bado unadhibitiwa kwa kiasi kikubwa na CCM. CHADEMA, katika hali ya kushangaza na katika mazingira ya kisiasa ya kati ya 2015 hadi mwaka huu, kimeimarika na kuogofya. Katika Majimbo ya Peramiho kwa Jenista Mhagama na Songea Mjini kwa Ndumbaro, mchuano kati ya CCM na CHADEMA utakuwa ni wa kihistoria.

CUF ambayo ilikuwa na nguvu ya kutosha na kutisha Tunduru na Namtumbo, kwasasa imefifia na hata sehemu nyingine kujifia. Wanachama wa CUF wamejitoa chama hicho na kujiunga na ACT, CCM au CHADEMA. Huku nilipo, CHADEMA imeendelea kuimarika na kujipenyeza hadi kwenye fukwe za Ziwa Nyasa. Inashangaza!

Majimbo yaliyobakia ya Mbinga na Songea Vijijini, mtifuano utakuwa kati ya CCM na CHADEMA ingawa hautakuwa mkubwa. Hata hivyo, Uchaguzi huja na maajabu yake. Huja na misuguano yake ndani ya vyama na kuzalisha ushindi kwenye vyama vingine. Tusubiri tuone. Naelekea mkoani Mbeya keshokutwa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Nyasa, Ruvuma)
 
Chadema ni kama mbegu ilishaoteshwa ardhini zamani sana, leo ukikata mti wake hapa, ujue mwingine utaota pale, msijidanganye haitakaa ife, ndio inazidi kustawi tu.
 
Back
Top Bottom