Mkoa wa Lindi: Historia na Taarifa Muhimu

Mkoa wa Lindi: Historia na Taarifa Muhimu

Peter Madukwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2012
Posts
3,140
Reaction score
2,499
Nimezaliwa na kukua Lindi, Nikasoma katika mkoa huu mpaka Kidato cha Nne, karibuni kwa swali lolote linalohusu mkoa huu mkongwe.

NB:
Mji wa Lindi zamani sana ulikuwa unaitwa kwa jina la utani la Paris kutokana na kuwa mji mashuhuri nchini tangu enzi za Waarabu kulinganisha na mji wowote Tanzania.

=========================

=========================


attachment.php


Tovuti ya Serikali ya Mkoa: Lindi | Lindi Region

Eneo la Mkoa wa Lindi

Mkoa wa Lindi umepakana na mikoa ya Pwani, Mtwara, Ruvuma na Morogoro. Upande wa Mashariki hupakana na Bahari Hindi. Mkoa huu umeanzishwa mwaka 1971 una eneo la 67,000 km². Karibu robo ya eneo lake au 18,000 km² ni sehemu ya hifadhi ya wanyama ya Selous.

Mkoa una wilaya sita za Lindi Mjini na Lindi Vijijini, Kilwa, Nachingwea, Liwale na Ruangwa.

Mito mikubwa ndiyo Lukuledi, Matando na Mavuji, yote yaelekea Bahari ya Hindi. Mwinuko huanza mwambaoni ukipanda hadi mita 500, hakuna milima mirefu sana.

attachment.php


Wakazi

Mwaka 2002 idadi ya wakazi ilikuwa 791,306. Karibu asilimia 90 kati hao ndio wakulima. Makabila makubwa zaidi ni hasa Wamwera ambao wanapatikana hasa wilaya ya nachingwea na lindi vijijini katika kata za Rondo halafu Wamachinga ,Wamalaba ambao wako zaidi lindi mjini Wamatumbi na Wangindo huko Kilwa.

Idadi ya wakazi wa wilaya ni (idadi katika mabano): Kilwa (171,850), Lindi Mjini (41,549), Lindi Vijijini (215,764), Liwale (75,546), Nachingwea (162,081), Ruangwa (124,516),

Hali ya hewa

Hali ya hewa ya Lindi ni ya joto mwaka wote ikiwa na wastani kati ya sentigredi 24,5 na 27. Mkoa hupokea kati ya 980 mm na 1200 mm za mvua kwa mwaka, hasa kati ya miezi ya Novemba na Mei.

attachment.php


Miundombinu ya Mawasiliano

Kuna barabara chache katika hali nzuri. Ndizo 155 km za barabara ya lami na 3567 km barabara za udongo, mara nyingi katika hali mbaya. Wakati wa mvua mara kwa mara njia ya kwenda Daressalaam imefungwa. Kuna matumaini ya kuboreka kwa mawasiliano na mji mkuu wa Dar es Salaam tangu kumalizika kwa daraja la Rufiji. Kwa sasa barabara ya kutoka Mingoyo mpaka Dar es Salaam imekamilika kwa kiwango cha lami.

Pana kiwanja cha ndege Lindi, Nachingwea na Kilwa Masoko. Lindi na Kilwa Masoko kuna pia bandari. Huduma za simu zipata maendeleo kiasi tangu kuanzishwa kwa simu za mkononi.

Utalii haujafikia umuhimu sana kutokana na matatizo ya mawasiliano magumu ingawa Lindi ina sehemu mbalimbali zenye uwezo wa kuwavuta watalii: Kilwa Kisiwani ndicho mji wa kihistoria wa pwani la Afrika ya Mashariki pamoja na magofu ya miji mingine ya Waswahili, Selous ni hifadhi kubwa kabisa katika Afrika, ufukoni wa mchanga ni wa kuvutia sana, nafasi za zamia majini ni tele.

Gesi imepatikana baharini karibu na kisiwa cha Songosongo imeleta matumaini ya maendeleo.

Kilimo na Biashara

Mkoa wa lindi wakazi wake wengi ni wakulima hasa maeneo ya vijijini wengi wanalima mazao mchanganyiko yaani ya biashara na chakula mazao ya biashara hasa ni Korosho ambazo zinapatika kwa wingi katika wilaya ya Ruangwa,Lindi Vijijini,na Nachingwea ,pia kuna zao la Ufuta na ndizi kama zao la biashara na chakula pia Mazao ya chakula kuna mahindi,mpunga,muhogo,nyanya,vitunguu hizi pia ulimwa sana wakati wa masika kutegemea na mvua za vuli. Biashara wakazi wengi wa mkoa walindi wanafanya biashara hasa biashara ndogondogo zijulikanaza kama machinga trade wanauza mazao wakati wa mavuno na uchukua bidhaa nyingi kutoka Dar-es-salaam na kupeleka vijijini hasa kwenye kata.

Elimu

Mkoa wa lindi huko nyuma kielimu kwani idadi ya shule za sekondari mpaka sasa si nyingi sana na shule hizo hazina walimu wa kutosha kutokana na miundombinu ya barabara na shule zenye kidato cha tano na sita mpaka sasa ni Lindi Sekondari, Mahiwa na Namupa Seminari, pia kuna Chuo cha Uwalimu Nachingwea katika wilaya ya Nachingwea
.


..................................................
..................................................
TANGAZO
Habari njema kwa wakulima wenye ndoto za kuingia kwenye kilimo cha korosho.

Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi anawaalika watanzania wote wenye nia ya kulima korosho kuja katika halmashauri yake na kuunga mkono jitihada hizo.

Mpaka sasa Halmashauri imetenga heka 45,000 kwa ajili hiyo mnaweza kuwa mnajiuliza inakuwaje mjini kukawa na mashamba naomba muelewe kuwa manispa ya lindi ndiyo manispaa inayoongoza kwa ukubwa tanzania jiji la mwanza lenye halmashari mbili linaingia zaidi ya mara mbili jiji la dar es salaam lenye manispaa tatu limeizidi kidogo sana manispaa hii.

Kilichofanyika manispaa iliongezewa maeneo ambayo yalikuwa ni Land bank mashamba ya korosho yaliyotelekezwa hifadhi ya misitu n.k ili ikidhi vigezo vya kuwa manispaa kutoka halmashauri ya mji.

Hivyo pamoja na ukubwa wake wote huu eneo linalotumika ni dogo sana eneo kubwa lililobaki ni pori au mashamba yasiyoendelezwa. Sasa manispaa imeamua kufanya mambo yafuatayo kwanza kutumia sheria za ardhi na mazingira misitu n.k kuanzisha program hii mashamba haya yamepimwa sasa tutaondoa mapori yasiyo na faida na kuanzisha misitu ya miti ya korosho hapo tutakuwa tumehifadhi mazingira lakini tumeendeleza ardhi.

Taratibu za kupata mashamba haya unatakiwa kuandika barua kwa mkurugenzi wa manispaa kuomba shamba kulingana na heka unazoona utawez kuzihudumia pia uelewe kuwa kazi ya kuendeleza mashamba haya inaanza mwezi wa pili mwaka huu hakuna kulala.

Manispaa itakupa shamba itakupatia miche ya korosho bure kwani mpaka sasa miche 1,000,000 imeoteshwa na ipo tayari kwa ajili hiyo. Miche hii itasafirishwa na manispaa mpaka eneo la shamba kazi yako ni kusafisha shamba na kupanda.

Shamba hili litamilikishwa kwako baada ya kuendeleza na kuhudumia.

Unatakiwa uelewe kuwa hawatoi mashamba kwa ajili ya kuhodhi bali kwa ajili ya kilimo katika mashamba.

Manispaa itakuletea umeme na maji shambani na njia baada ya kuendeleza.

Heka moja ya shamba inapatikana kwa tsh 10,000 kwa mzawa wa Lindi na 50,000 nje ya Lindi hakuna dalali wa hii kazi msije kuibiwa bure na fedha hii inalipwa katika akaunt ya deposit ya manispaa

Mkija huku mje na mawazo ya kulima na baada ya hapo ku process korosho viwandani na si kupeleka minadani lengo la manispaa ni kuwa na uchumi mkubwa wa kilimo cha korosho wenye viwanda vyenye kuchakata malighafi za korosho.

Hii ni plan B baada ya serikali kuchukua kodi za majengo minara ardhi sasa manispaa inataka kupata mapato yake kwenye fursa hii.

Ukipanda korosho mwaka 2018 mwezi wa 2 unauhakika wa kuanza kuvuna mwaka 2020.

Msiseme hatujawaambia karibuni kusini kwa maelezo ya ziada njooni inbox.

Pamoja tunaweza
Korosho Dhahabu ya kijani

Mawasiliano
Mkurugenzi wa manispaa
Halmashauri ya manispaa Lindi
S. L. P 1070
Lindi
 

Attachments

  • HEADER.jpg
    HEADER.jpg
    43.2 KB · Views: 805
  • lindi.jpg
    lindi.jpg
    116.5 KB · Views: 998
  • lindi1.jpg
    lindi1.jpg
    64.6 KB · Views: 815
Mazao gani ya biashara na chakula hulimwa kwa wingi Lindi?
 
Salma Kikwete anataka kugombea ubunge jimbo gani Lindi?
 
Mkoa wa lindi una vijiji vingapi? Kipi kipi kina wakazi wengi, na shughuli yao kuu ya kuwaingiza kipato ni ipi?
 
hizo ni tetesi tu.. Ambazo hata mi nimewahi kuzisikia kwamba first lady anataka kugombea jimbo la lindi mjini ambalo kwa sasa limashikiliwa na mbunge wa CUF.. Barwani
Kwa hiyo familia ya Kikwete inataka kuweka rekodi mjengoni!
 
Asante
mkoa wa lindi ni moja kati ya mikoa ya pwani.. Samaki wanavuliwa na kuliwa kwa wingi hasa ktk wilaya ya kilwa na wilaya ya lindi. Hata hivyo ktk wilaya ya kilwa ndiko samaki huvuliwa kwa wingi na hupatikana kwa bei nafuu kulinganisha na wilaya ya lindi ambapo samaki huuzwa ghari kutokana na kutopewa kipaumbele sana ktk uvuvi

Umeulizwa bado mnakula chamaki nchanga na ming'oko? We unajibu mambo ya uvuvi, toa jibu la chamaki nchanga.
 
Nataka kutangaza ndoa na mke wa Lindi lkn nasikia wanawake wa huko hawamnyimi ntu kitu alichopewa bure. Yaani hawajui neno NO. maneno haya yana ukweli wowote ?
mahari huko ni bei gani ?
 
Asante
mkoa wa lindi ni moja kati ya mikoa ya pwani.. Samaki wanavuliwa na kuliwa kwa wingi hasa ktk wilaya ya kilwa na wilaya ya lindi. Hata hivyo ktk wilaya ya kilwa ndiko samaki huvuliwa kwa wingi na hupatikana kwa bei nafuu kulinganisha na wilaya ya lindi ambapo samaki huuzwa ghari kutokana na kutopewa kipaumbele sana ktk uvuvi

Umeulizwa kuhusu samaki nchanga, Hebu jibu sasa.
 
Kinachoniuma mimi ni ile bandari pale?? Kwa nini mmeifanya ya maonyesho na si kufanyia kazi ili ilete maendeleo ya mkoa!!??
 
Kwa nino Lindi haikuwa kwenye harakati za pamoja na Mtwara kudai gesi inufaishe mikoa ya kusini kwanza?? Mkiitwa wasaliti, je mna hoja ya maana ya kujitetea kuwa Lindi hawakuwa wasaliti wa harakati??
 
Record aliyoiweka NDESAMBURO haitakaa ivunjwe karne hhii. Mdesamburo ni mbunge. binti yake ni mbunge na mkwe wake ni mbunge. mshkaji wake wa karibu ni mbunge.

duh kweli hiyo ni wolrd record
 
Mna mpango gani kuhusu suala la gas naona mtwara wako kasi kudai haki zao vipi lindi songosongo kimyaa wananchi hawalalamiki
 
Back
Top Bottom