Mkoa gani unafaa kwa kilimo 100%

kiben10

JF-Expert Member
Apr 28, 2018
616
789
Napenda kuwashirikisha vijana wenzangu kwa hili, naomba kujua mkoa gani naweza kufanya kilimo cha Mahindi na Maharage nikafanikiwa kwa 100%???
Kwani ile biashara yangu ya mkaa naona LOSI imeshaingia na mtaji umeliwa kwa 45% sasa kabla sijaadhirika naombeni mnijuze kwa jambo hili nalowashirikisha ili nisije nikawa CHIZI kwa sababu GHOFU langu nimeuza na PESA inakwisha, nataka kuamia huku je niende MKOA GANI UNAFAA KWA KILIMO??

PS: Mtaji wangu ni 1.4M
 
Jitahidi na hiyo 1.4 isije ikaisha maaana uliuza nyumba ukafanye biashara ya mkaa!!!! Nakushauri nenda Doma ukalime nyanya miezi 3 tu unaingia sokoni.
 
Ndugu,kilimo ni sayansi. Kabla ya kuchagua ni Mkoa gani unafaa yakupasa ujue lengo LA KULIMA mazao hayo Ni nini? Wateja wako ni akina Nani? Miundo mbinu ikoje? Gharama za uzalishaji ziko vipi? Mahitaji ya kilimo eg mbegu,mbolea,viuadudu,ardhi,utaalamu nk.
 
Alafu kingine anatakiwa ajue ya kwamba sehemu yenye rutuba hakuna Soko la mazao. Labda kama ana target ya kupeleka mjini DSM, Mwanza, Zanzibar, arusha na sehemu ya majiji na sio uku kwy rutuba hakuna wanunuzi na wanunuzi ni choka mbaya
 
Back
Top Bottom