Mko wapi tujuane

Mko wapi tujuane

FURY BORN

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2020
Posts
637
Reaction score
1,152
Wale wooote tuliopitia elimu ya sekondari Enzi za Professor Sarungi akiwa waziri wa elimu, wale tuliobadilishiwa mtaala tukiwa kidato cha tatu na kutakiwa kufanya mtihani wa somo la siasa lilobadilishwa na kuitwa civics ndani ya miezi michache.

Wale tuliosoma shule za jumuiya ya wazazi unasoma kuanzia kidato cha Kwanza mpaka nne bila kusoma physics na hesabu.

Wale tuliomaliza form bila hata kujua kusolve hesabu ndogo kama simultaneous.

Wale ambao mwanao wa kidato cha pili akirudi na home work ya hesabu na akahitaji msaada wako ndo siku ambayo utaingia bedroom mapema ukijifanya kuchoka Sana.

Wale ambao tulifanya mtihani wa kidato cha pili alama ya mwisho ya ufaulu ikiwa ni 21, lakini matokeo Tanzania nzima yakawa mabovu mpka Sarungi akaamue wanafunzi wote waliokuwa na alama mpka 18 kama sikosei waendelee kidato cha nne,

Wale ambao baada ya hapo tulianza kuunga unga na Leo hii tuna digrii na tunapiga hela kuliko hela kuliko waliopiga one za Saba na one ya tatu A levels, lakini Leo hii wako chini yetu tukiwafanyia tathmini za kiutendaji.
 
Mkuu mimi ni mdogo wako au kaka yako? Waziri wangu wa Elimu aliitwa JACKSON MAKWETA...vuta kumbukumbu kati ya Sarungi na Makweta nani alianza...kkkkk
Sarungi aliukwaa uwaziri kipindi Cha AHM Wakati Makweta alianza uwaziri enzi za Mwalimu mwaka 1981.
Sisi wengine tulisoma enzi za yule mpare mkware Mgonja na baadaye mama Tabitha Siwale wakati ule Tanzania nzima shule za sec zilikua 189.
Lindi kulikua na shule moja
Kigoma moja
Pwani zilikua 6
Dar zilikua kumi na moja tu.
Kinondoni
Mzizima
Shaaban Robert
Zanaki
Kisutu
Jangwani
Azania
Tambaza
Kibasila
Pugu
Forodhani
Mgulani ilikua ya wanajeshi
Sasa hivi nasikia Dar Kuna zaidi ya shule Mia mbili za sekondari.
Tumeendelea.........
 
Dah mkuu unakumbukumbu sana. Hapo Pwani kulikuwa na shule kadhaa maarufu Kibaha, Minaki, Bagamoyo, Ruvu n.k
 
Aisee humu kuna ma komredi wamekula chumvi balaaa
 
Dah mkuu unakumbukumbu sana. Hapo Pwani kulikuwa na shule kadhaa maarufu Kibaha, Minaki, Bagamoyo, Ruvu n.k
Pwani zilikua
Minaki
Bagamoyo
Kibaha
Ruvu
Ikwiriri Ile shule iliyojengwa na wa Cuba Kama Ruvu na moja iko mkoa wa Moro.
Mkoa uliokua unaongoza kwa shule ilikua Kilimanjaro. Kulikua na shule 81. Ndio ujue sio kwa ukabila kwamba wachagga wako kila sekta katika nji hii.
TANGA zilikua shule 9 tu
Galanos aka Nguvumali
Usagara
TANGA school
Popatlal
Jumuiya
Hegongo Muheza
Korogwe girls
Boza technical
Magamba Lushoto
Wilaya ya Handeni ilikua haina shule ya sekondari ndio maana hakuna wazigua wasomi. Nadhani mpaka sasa hakuna profesa wa kizigua.
 
Wazigua hawana profesa had leo?

Wahadzabe watawapita hao maana kuna vijana wako wanaitafuta PhD kutoka kabila hilo
 
Wazigua hawana profesa had leo?

Wahadzabe watawapita hao maana kuna vijana wako wanaitafuta PhD kutoka kabila hilo
Peramiho yetu kwenu Ruvuma ilikua si hapa
Kulikua na
Kigonsera
Songea boys
Songea girls hii shule ilikua na wasichana wakware sana.
Nadhani Hadi Sasa Ruvuma hakuna chuo kikuu hata kimoja. Hii inaonyesha Ni kiasi gani wakunyumba wanawekeza kwenye pombe na ngono. Shauri yenu
 
Hahaha haha Wangoni wanapenda Ngono na Pombe na Masherehe yenye minuso
 
Peramiho yetu kwenu Ruvuma ilikua si hapa
Kulikua na
Kigonsera
Songea boys
Songea girls hii shule ilikua na wasichana wakware sana.
Nadhani Hadi Sasa Ruvuma hakuna chuo kikuu hata kimoja. Hii inaonyesha Ni kiasi gani wakunyumba wanawekeza kwenye pombe na ngono. Shauri yenu
Kabisa mkuu kilikuwepo kile cha wakatoliki sjui Kama Bado kpo Kuna kipind kilizuiliwa kudahi

Kipo chuo kikuu cha madaktar hapa peramiho sjui kinaitwa St James vjana wanasoma ila kimezuiliwa kudahil wengine had marekebisho yafanyike
 
Mkuu mimi ni mdogo wako au kaka yako? Waziri wangu wa Elimu aliitwa JACKSON MAKWETA...vuta kumbukumbu kati ya Sarungi na Makweta nani alianza...kkkkk
Walipishana kama sikosei makweta ndo alimwachia Sarungi, ikiwa form four ulifanya mtihani wa siasa wewe ni Kaka, lakini kama umefanya civics na ukiwa umeisoma civics wewe ni mdogo wangu. Mimi ndo tuliofanya mtihani wa Kwanza wa civics
 
Back
Top Bottom