Mkiwatawala waume zenu mtazaa mashoga…………………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkiwatawala waume zenu mtazaa mashoga…………………!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Apr 17, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kuna wanawake ambao kwa lugha ya mazoea tunasema wamewatawala waume zao. Yaani wao ndio wenye kauli ya mwisho katika nyumba na pia hutumia vibaya madaraka hayo kwa kuwanyanyasa waume zao. Akina mama wa aina hii ni rahisi sana kwao kusababisha baadhi ya watoto wao kuja kuwa mashoga.

  Inakuwaje?

  Baadhi ya watoto hawa ni wale wa kiume hujikuta wakimtazama baba yao kama mwanaume aliyeshindwa na hutafsiri kushindwa kwake kama kasoro ya uanaume. Katika mkabala huo watoto hawa hujikuta wakiatamani kuwa kama mama zao, kwani mama zao ni mashujaa wao na kwao kuwa mwanamke kuna maana ya madaraka, kutoa amri na kuheshimiwa zaidi. Mtoto hujenga na kuamini mambo hayo ndani ya fikra zinazofahamika kama Subconscious Mind, ambazo ni fikra au mawazo yasiyopumzika na yanayotunza kumbukumbu zote kwa matumizi ya baadae ya binadamu. Kwa kawaida watoto huwa hawajui kwamba ndivyo fikra zinavyoamini kwani Subconscious Mind hufanya kazi bila mhusika kujua.

  Kwa kuwa ndivyo mtoto anavyoamini ndani ya fikra zake, mtoto hujikuta akiwa karibu zaidi na mama na kujaribu kumuiga mama yake kuliko baba yake ambaye anamuona kama mnyonge. Kwa hiyo mtoto huyu wa kiume ataanza kufanya mambo yote ya kike kwani kwake uke ni ushujaa. Hata wenzake anaoshirikiana nao mambo ya kufichaiansiri watakuwa ni wanawake. Kujibainisha kijinsia itakuwa vigumu sana kwake. Hii ni kwa sababu kwa nje atakuwa anajiona kuwa ni mwanaume, ingawa kwa ndani anajihisi kuwa ni mwanamke na atakuwa anapendelea kuwa hivyo.

  Mwanasaikolojia mkongwe na maarufu duniani, Dennis Coon, ambaye katika kitabu chake , Introduction to Psychology amekusanya na kuzikagua nadharia mbalimbali kuhusu chanzo cha ushoga, anakiri kwamba nadharia ya malezi inaonekana kuwa na mashiko zaidi. Anasema mama "Mbabe" na mwenye kumwendesha mwanaume na kuutweza utu wake na heshima ya uanaume wake anaweza kabisa akujikuta akiwa na watoto wa kiume wanaojibainisha naye na kuukimbia uanaume wa baba yao. Watoto kama hawa sio ajabu wakiwa mashoga………………….!
   
 2. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Ninakubaliana nawe Mtambuzi wa tabia kuwa kwa sehemu kubwa, malezi ya wazazi kwa watoto yanaweza kwa sehemu kubwa kuchangia mtoto kuwa shoga. Pia hata the way watoto wanavyokuwa exposed kwenye mazingira mabovu yasiyo na maadili yanaweza kumuathiri mtoto na kujikuta amechukua tabia hizo chafu.

  Ila sina uhakika na suala la tabia ya mama kuwa mbabe ndani ya nyumba kama ni sababu pia ya kuwafanya watoto wawe na tabia hizi mbaya .... Inawezkana lakini ngoja tuachie na wengine wataalam wa saikolojia na malezi wachangie tuwasikie ...
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi mwanamme hatawaliwi na mwanamke kama hana mapungufu ya kiume au kama si shoga. Mwanamke hakutawali kama hauna "weakness" za urijali.

  Kwa mtazamo wangu, mwanamme ambae hana maamuzi ya mwisho nyumbani kwake huyo ni shoga amma ana uhanisi fulani. Amma uhanisi wa kiume amma uhanisi wa kimapato. Bila kasoro za uhanisi huwezi kuwa ndondocha wa mwanamke. Wanawake hutaka vitu viwili tu kwa mwanamme, urijali wake ndio kwanza, akikosa hilo basi mapato ya mwanamme. Akikosa yote hayo hakai hata kidogo. Mwanamme mwenye uhanisi wa kimoja kati ya hivyo vitatu ni lazima atawaliwe na mwanamke.

  1. Shoga
  2. Urijali usiokidhi viwango (uhanisi)
  3. Uhanisi wa kipato.
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  na nchi ikitawaliwa na mwanamke wananchi watakuwa nini?
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Lakini na nyie kwa nini mkubali kutawaliwa ...
  Unatakiwa uwe kama dume la simba likinguruma mmmmh..am kidding.
   
 6. N

  Nyakwaratony JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 575
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  hilo nalo neno!
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  haijawahi tokea ila kuongozwa sawa lakini kutawaliwa nope...
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  lakini sio kwamba mashoga walio wengi huwa wanasababishiwa hiyo hali na marafiki, ndugu na sio wazazi zaidi maana sidhani kama kuna mzazi anaependa mwanae awe bwabwa basi huyo itabidi akimbiwe na jamii...
   
 9. n

  ngokowalwa Senior Member

  #9
  Apr 17, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  FL1 kwani wewe hupendi utawala -lol
   
 10. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hi kali aisay, na aliye uongea hio point...inabidi tumrudishe shule.
   
 11. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,852
  Trophy Points: 280
  nionavyo mim mwanaume huwa anatawaliwa na mwanamke kwasababu ya mapungufu yake. ila kuna wamama wengine wamezaliwa wababe by nature hivyo mwanaume anatakiwa ajue silka za anayetaka kumuoa, ndio maana huwa wataalam wanashauri basi uchumbe uwe mwaka na aid ili kumpa kila mtu nafsi ya kumjua mwenzie japo kidogo.

  lakii ushoga wa watoto unaweza ukachangiwa na mambo mengi sana, alilosema mtoa mada ni moja tu ya yanayoweza kusababisha but ukweli ni kwamba hata environment hasa mtaani, au watu walioko pale nda ukiacha wazazi au hata shuleni hasa boarding. pia pana ishu ya kupenda vya bure. hizi ni tamaa za hela na maisha ambapo mtu binafsi anajichangulia ambazo hazihisiani kabisa na malezi aliyo yapata nyumbani.
  m
  mambo yanayoweza kuzuia ushoga miongoni mwa wanaume ni haya
  a) kujikubali na kupenda uanaume wao.
  b)kupenda kufanya kazi na si kupenda vya bure
  c)kuepuka makundi mabaya
  d) kuwa wacha mungu.
  e)kuthamini nafasi waliyonayo kama baba na kukumbuka wajibu wao kwa familia.

  wajue kabisa kupenda kuingiliwa kainayuame na maumbile ni dhambi na wanachokiomba wasijaribu kabisa kwani wangepewa kuwa wanawake halafu waingie mp kama wanawake na wazae kwa uchungu basi wangejua uwa me ni raha kuliko kuwa ke
   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe kwa 100% na ndio maana kama nilivyonukuu utafiti wa mwanasaikolojia Dennis Coon kwamba suala la ubabe wa wanawake kwa waume zao huchangia pia watoto wao wa kiume kuwa mashoga, kwa hiyo sababu ulizozitaja ni moja kati ya vyanzo vinavyo-infuency watoto wakiume kuwa mashoga. Nimeamua kulizungumzia jambo hili kwa sababu wanawake wengi siku hizi huona ufahari kuwatawala waume zao na ndio maana vitu kama LIMBWATA vinatajwa sana na wanawake kama njia rahisi ya kuwa juu ya vichwa vya wanume zao.
   
 13. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Siamini...ubabe sio hobby ya mwanamke bali mama inabidi avae pants ikiwa baba hajaweza. Sidhani kama kuna mama atataka family isambaratike kutokana na udhaifu wa baba. Ikiwa huyo mtoto wa kiume ni mwenye akili timamu anawezajua kama mama yao is doing the best for them, not a lousy father.

  Ukiwa wanaume wanatafanya wajibu wao hakuna mtu atakaetawaliwa. Regardless the situation, you should also know that Husbad is the head and the wife is neck, she turn it the way she want na sio lazima utawaliwe usijidanganye lol
   
 14. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Kuna ukweli kwenye hii thread kwani nimeshuhudia wanawake wababe wengi wakiwa karibu zaidi na watoto wao wa kiume na baba zao hawasikilizwi kabisa na wengine wakaamua kujitoa kabisa katika masuala ya kuisupport familia na kuishi kivyao. mitoto ya kiume utaikuta ikiwa karibu na mama hata wakati wakitafuta mchumba lazima mama aweke tick
   
 15. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #15
  Apr 17, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Wanaofficial name hao....mtoto wa mama!
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Wewe wasema...........Lakini kaa ukijua kwamba wapo wanawake aidha kwa malezi au kutokana na kujifunza tabia hizo ukubwani hujisikia fahari kuwatawala waume zao, wanaume wanaokubali kuwa chini ya amri za wake zao nao wameathiriwa na malezi pia...........kama alivyosema mchangiaji mmoja kwamba mwanaume anayekubali kutawaliwa na mkewe atakuwa ana udhaifu wa urijali wake au kipato na hafanyi juhudi zozote kujikwamua na badala yake anamuacha mkewe awe mtafutaji na mbeba majukumu ya hapo nyumbani kwa sababu yeye ameshindwa.
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Na mara nyingi hawadumu na wake zao kwenye ndoa,kwani waliwaolea mama zao na si wao waliooa...............Mama ndiye anayekuwa mhimili wa ndoa za watoto wao......... wawe ni wa kike au wa kiume.
   
 18. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #18
  Apr 17, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Siku hizi unajitahidi aisay, unakumbuka zamani tulipo kuwa kule ulikuwa hujui hata kuongea kiswahili.
   
 19. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #19
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,176
  Likes Received: 1,895
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa nasema Mengi humu kuhusu Ubeijing!.. Wanawake wakaja Juu.

  Sasa thread za Negative Effects zinakuja kwa Kasi..
   
 20. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280

  wananchi wenye jinsia ya kiume watakua nini? hihihiii
   
Loading...