Mkinga: Barrick walikodi kampuni kutoka SA kuibua makontena ya mchanga

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
30,861
2,000
Namsikiliza mzee Mkinga akiongelea mada kuhusu hatua za Rais Magufuli kudhibiti wizi wa madini katika kipindi cha je tutafika Kinachoendeshwa na Makwahia wa Kuhenga Channel Ten

Mkinga anasema kuwa Barrick waliwahi kudondosha makontena ya mchanga pale bandari ya Tanga na kulazimika kukodi kampuni kutoka South Africa kwa dola milioni mbili ili kuja kuyaopoa.
 
mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,158
2,000
Hata wenyewe hawajakataa kama yanathamani kubwa . Tena pamoja na sisi kugundua zaidi, wao yanawaingizia zaidi ya 50% ya kipato Chao cha mwezi.

Kuzuia makontena ya acacia mining company Plc ni Sawa na kuziba pua isipumue kampuni hiyo yenye migodi tanzania tu. Kila kiumbe wa acacia anahisi maumivu makali ndio maana wamekuwa wapole.

Hapo ndio unamshangaa mtanzania anapoyaita Makinikia au Copper/Gold concentrate takataka au magwangala ili kuhamisha magoli watu waache kujadili vitu vya msingi.
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
10,739
2,000
Wanajua yana hela ndefu ndio sababu lkn mwanasheria msomi Lissu ambaye hajui hata symbol ya copper kuwa ni Cu anasema ripoti ni rubbish
mkuu...Lissu yupo sahihi kabisa kwa 100%. opinion yake imetokana na a well informed briefing kutoka kwa watu wanaoyajua haya mambo in depth and breadth.

Binafsi mchakato pamoja na ufundi wa kupima viwango vya madini ndani ya mchanga navijua kwa undani sana.

Tunaojua tunashindwa kuelewa ile kamati hata sijui ilipata wapi/vipi yale majibu yake na sijui kama walikuwa anticipative kwenye implications za walichokuwa wanakifanya.

Msomi yeyote anayejitambua huwa anajiongeza - ile kamati hata haikujiongeza. kwa nini - wanajua wao wenyewe!
 
tryphone005

JF-Expert Member
Jan 30, 2017
459
500
Hata wenyewe hawajakataa kama yanathamani kubwa.
Hapo ndio unamshangaa mtanzania anapoyaita takataka au magwangala
Mkuu ss watu weusi ni wataalam wa uchawi na ushirikina tu, mgombea ubunge , mgombea udiwani, mgombea chochote kile, maofisini, mashuleni, kwenye burudani wote wanapishana kwa kalumanzila na pale ukienda unaambiwa geuka uingie kinyumenyume, sasa matokeo yake watu wanakuja wanafikiria kwa kutumia makalio, ndio mawazo yanakuwa hivyo, mali zinaitwa takataka!
 
RedDevil

JF-Expert Member
Apr 30, 2009
2,377
2,000
mkuu...Lissu yupo sahihi kabisa kwa 100%. opinion yake imetokana na a well informed briefing kutoka kwa watu wanaoyajua haya mambo in depth and breadth.

binafsi mchakato pamoja na ufundi wa kupima viwango vya madini ndani ya mchanga navijua kwa undani sana.
tunaojua tunashindwa kuelewa ile kamati hata sijui ilipata wapi/vipi yale majibu yake na sijui kama walikuwa anticipative kwenye implications za walichokuwa wanakifanya.
msomi yeyote anayejitambua huwa anajiongeza - ile kamati hata haikujiongeza. kwa nini - wanajua wao wenyewe!
Huenda walipewa ToRs kuanzia kufanya analysis na cha kuandika kwa malengo fulani. Ushaambiwa Mkuu anatafuta hela ya kujenga reli ya kisasa maana aliahidi katika kampeni zake za uraisi. Sasa akishindwa kuijenga mmm anaona atakuwa kashindwa na ujue hakubali kushindwa kitu!!
 
mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,158
2,000
mkuu...Lissu yupo sahihi kabisa kwa 100%. opinion yake imetokana na a well informed briefing kutoka kwa watu wanaoyajua haya mambo in depth and breadth.

binafsi mchakato pamoja na ufundi wa kupima viwango vya madini ndani ya mchanga navijua kwa undani sana.
tunaojua tunashindwa kuelewa ile kamati hata sijui ilipata wapi/vipi yale majibu yake na sijui kama walikuwa anticipative kwenye implications za walichokuwa wanakifanya.
msomi yeyote anayejitambua huwa anajiongeza - ile kamati hata haikujiongeza. kwa nini - wanajua wao wenyewe!
Anadanganya anaposema makinikia Yana thamani Sawa na 5% ya kipato Chao chote.
Kuhusu kiwango ni controversial lkn kuhusu thamani ya kilichomo hata kwa kiwango Chao wenyewe wawekezaji kinawaingizia mabillions. Ngoja tusubiri vita vyakitaalam Kati ya kamati na Acacia tuone nini ni nini...
 
kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,845
2,000
Watanzania wote wanaompinga TL hawawezi kuzungumzia ile 95% ya dhahabu yanayosafirishwa moja kwa moja. Huwezi kuwakuta wakizungumza haya , wanazunguka tu kwenye mambo ya makanikia.

Mwanaume TL kasema tunaibiwa kwenye dhahabu ambako 95% huondoka moja kwa moja, lakini maccm mtandao wameambiwa huko msiguse, TL anawaambia letenk sheria zote bungeni tuyajadili na kuyarekebisha ila maccm mtandoa hawataki kuzungumzia hapo.

Wamepewa hadidu za rejea na waajiri wao kuanzisha uzi kumshambulia lisu kila siku kwa sharti la kutokugusia dhahabu pure, mikataba na wale viongozi na wabunge wao waliopitisha hizo sheria kwa ndioooooo. CCM ndiyo tatizo katika hii nchi
 
Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
8,424
2,000
Namsikiliza mzee Mkinga akiongelea mada kuhusu hatua za Rais Magufuli kudhibiti wizi wa madini katika kipindi cha JE TUTAFIKA? Kinachoendeshwa na Makwahia wa Kuhenga.Chanel ten

Mkinga anasema kuwa barrick waliwahi kudondosha makontena ya mchanga pale bandari ya Tanga na kulazimika kukodi kampuni kutoka South Africa kwa dola milioni mbili ili kuja kuyaopoa.
Ni kweli, contena ilionesha ina thamani ya sh milion 40 na baada bandari kushindwa kuopoa walikubali kuilipa Barrick thamani ya mchanga ambazo ni Tshs 40 ml, Barrick wakataa wakakodi mitambo wakalipa karibia Tshs bilion 4.5 kuopoa contena yenye thamani ya Tshs 40ml.
Halafu serikali ikaona ni sawa hilo kontena lilikuwa na thamani ya 40ml na likaachwa liendelee na safari.
 
Fundisi Muhapa

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
4,433
2,000
Hata wenyewe hawajakataa kama yanathamani kubwa . Tena pamoja na sisi kugundua zaidi, wao yanawaingizia zaidi ya 50% ya kipato Chao cha mwezi. Kuzuia makontena ya acacia mining company Plc ni Sawa na kuziba pua isipumue kampuni hiyo yenye migodi tanzania tu. Kila kiumbe wa acacia anahisi maumivu makali ndio maana wamekuwa wapole...
Hapo ndio unamshangaa mtanzania anapoyaita takataka au magwangala ili kuhamisha magoli watu waache kujadili vitu vya msingi
Ni MASHAPO
 
Sophist

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
4,085
2,000
mkuu...Lissu yupo sahihi kabisa kwa 100%. opinion yake imetokana na a well informed briefing kutoka kwa watu wanaoyajua haya mambo in depth and breadth.

binafsi mchakato pamoja na ufundi wa kupima viwango vya madini ndani ya mchanga navijua kwa undani sana.
tunaojua tunashindwa kuelewa ile kamati hata sijui ilipata wapi/vipi yale majibu yake na sijui kama walikuwa anticipative kwenye implications za walichokuwa wanakifanya.
msomi yeyote anayejitambua huwa anajiongeza - ile kamati hata haikujiongeza. kwa nini - wanajua wao wenyewe!
Wakala! A jungle scientist? Lissu got intl from sources privy to the issue, who? Acacia?
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,520
2,000
mkuu...Lissu yupo sahihi kabisa kwa 100%. opinion yake imetokana na a well informed briefing kutoka kwa watu wanaoyajua haya mambo in depth and breadth.

binafsi mchakato pamoja na ufundi wa kupima viwango vya madini ndani ya mchanga navijua kwa undani sana.
tunaojua tunashindwa kuelewa ile kamati hata sijui ilipata wapi/vipi yale majibu yake na sijui kama walikuwa anticipative kwenye implications za walichokuwa wanakifanya.
msomi yeyote anayejitambua huwa anajiongeza - ile kamati hata haikujiongeza. kwa nini - wanajua wao wenyewe!
Theory from primary school to university..
 
Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,171
2,000
Wanajua yana hela ndefu ndio sababu lkn mwanasheria msomi Lissu ambaye hajui hata symbol ya copper kuwa ni Cu anasema ripoti ni rubbish
Watu wengi hawajamuelewa Lisu, siku zote tumekua tukijisaidia vichakani kwasasa tumekiona choo kipo wapi, anachokipigania Lisu ni kwamba tuendapo huko chooni tusiende peku twaweza pata magonjwa.
 
Mr.Junior

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
10,284
2,000
Wasomi wetu wa Kitanzania ndio mlioingia mikataba mibovu, ndio mnaowasaidia Wazungu kutuibia mali zetu hakuna la maana mnalofanya lenye manufaa kwa nchi hii.

Mmebaki kujisifia tu kwenye mitandao ya kijamii na vijiwe vya kahawa kuwa nyinyi ni wasomi ila usomi wenu haujaleta matokeo yeyote kwa nchi hii.

mkuu...Lissu yupo sahihi kabisa kwa 100%. opinion yake imetokana na a well informed briefing kutoka kwa watu wanaoyajua haya mambo in depth and breadth.

binafsi mchakato pamoja na ufundi wa kupima viwango vya madini ndani ya mchanga navijua kwa undani sana.
tunaojua tunashindwa kuelewa ile kamati hata sijui ilipata wapi/vipi yale majibu yake na sijui kama walikuwa anticipative kwenye implications za walichokuwa wanakifanya.
msomi yeyote anayejitambua huwa anajiongeza - ile kamati hata haikujiongeza. kwa nini - wanajua wao wenyewe!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom