Mkikimkiki: Mdahalo wa elimu na afya kwa vyama vya siasa

Jul 2, 2015
20
23
Habari wakuu,

Leo Jumapili Septemba 13, 2015 tunawaletea midahalo ya Mkikimkiki na leo utajikita kwenye elimu na afya, wawakilishi wa vyama kwa leo ni;

1. Khamis Kigwangalla akiwakilisha Chama Cha Mapinduzi
2. Samson Mwigamba atawakilisha ACT wazalendo
3. Ndelakindo Kessy atawakilisha NCCR-Mageuzi
4. Jacob Samuel atawakilisha ADC na Rajab Hozza atawakilisha UPDP

Mdahalo huu pia utarushwa na kituo cha televisheni cha Star TV na kusikika radio free Africa. Tuwe sote pamoja kujuzana yatakayojadiliwa.
========

View attachment 286443

Swali: Chama chako kina mkakati gani kuhakikisha watoto wote wanapata lishe bora?

Rajab UPDP: Tukipata madaraka kutakuwa na utaratibu wa kotoa lishe bora mahospitalini ili mama ajenge afya yake, sasa hivi imekuwa ni afya ya kutoa ushauri, mtoto anapozaliwa anatakiwa kupota huduma bora kijamii, lishe bora zote zitakuwa mahospitalini na kina mama watapewa lishe bora wakienda nyumbani. Huduma za afya zimekuwa mbovu kwa makusudi kwa sababu madaktari wana hospitali binafsi, kama una hospitali binafsi marufuku kufanya kazi serikalini.

Kigangwala CCM: Jibu sio la oja kwa moja kwa sababu linahusisha vitu vingi sana, sera ya CCM mpaka sasa hivi inatoa madini ya chuma na iodin pia kwa kina mama wajawazito bure, baada ya kujifungua pia ni bure na kwa watoto chini ya miaka mitano, pia kuwapa mama wajawazito kinga ya Malaria.

Ndelakindo NCCR: Natoa rai kwa wagomba wote, mama Tanzania ametuhidhadhi kwa miaka 50, tuhakikishe amani yetu inatawala, NCCR mageuzi na UKAWA tumekubaliana kuwa na ilani moja ya uchaguzi.
Tumewek sera, mama wajawazito wana wajibu wa kufika vituo vya afya, mgombea Urais kupitia UKAWA pia wamesisitiza afya kwa mama wajawazito. Tutaweka msisitizo zaii kwa mama mjamzito kuondoa tatizo la watoto kudumaa chini ya miaka mitano.

Mwigamba ACT: Tatizo linaanzia kwenye uchumi wetu, suluhisho la kwanza ni kuhakikisha tunajenga uchumi shirikishi, kuimarisha uchumi ni hatua ya muda mrefu, hatua ya jaraka ni kuunda jopo la wachumi na afya kuona ni huduma gan za msingi kwa mama mjamzito na afya kwa ujumla na zitakua bora kwa shule zote za serikali na binafsi. Kuna huduma serikli itakuwa ni wajibu wake ili kuimarisha afya za watoto wetu.

Jacob ADC: Kuhakikisha wananchi wanapata chakula miili yao kuhimili magonjwa na watoto kukuza na kuimarisha miili yao, ADC katika sera itahahakisha inawapatia wananchi wote chakula kwa kuchangia. Kuhahakikisha shule zote zinapata chakula kwa wanafunzi pamoja na walimu wao.

Rajab: UPDP hili tatizo lipo sehemu tatu, itafuta mtihani wa darasa saba, mtoto ataanza shule akiwa miaka sita mpaka darasa la kumi, pia kupiga marufuku tuisheni, tuisheni ya sasa ni pango la unyang'anyi.
Fredy Chacha: Kulinga na sera za vyama, baadhi wametangaza kutoa elimu bure, J e inawzekanaje kwa upande mmoja na mwengine ishindikane.
Ndelakindo: Takwimu zinaonyesha Afrika ndio wakopeshaji wa dunia, sisi ndio wenye rasilimali, misaada tunayopata ni kidogo sasa kulingana rasilimali zinazochotwa, kupitia katiba mpya tutahakikisha mirija hiyo inakatwa.

Mwigamba: Elimu ya msingi itakuwa kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne na itakuwa bure, baada ya hapo wanafunzi waliofaulu vizuri watapewa scholarship na ambao hawajafanya vizuri watapata mikopo. Serikali inakusanya asilimia 11 tu kama kodi kwenye pato la taifa.
Jacob: Tutatoaje elimu bure, lazima wananchi wafanye kazi ili pato likue na serikali ikusanye pesa zaidi kurudisha kwenye elimu.

Rajab: Usimamizi mzuri wa rasilimali itawez kutoa elimu bure msingi mpaka sekondari, mabadiliko ni lazima chagueni UPDP.

Kigangwala: Wanachokiahidi wenzetu ni kwa pupa, mabadiliko ni hatua, tulianza na msingi tunakaweza na sasa tunahamia sekondari. Mtu leo anaibuka na kusema elimu itakua bure bila kusema pesa zitatoka wapi, huwezi kuanza na elimu kabla hujawapa watu chakula

Swali; Elimu bora ni msingi wa maisha bora, asilimia 30 darasa la sababu hawawezi kufanya hesabu wala kusoma kwa kiwango cha darasa la pili. Nini sera zenu?

Kingwangala: Ni lazima tuongeze walimu, vitabu na maslahi ya walimu, huwezi kufikia hilo bila rasilimali fedha, serikali ya chama cha mapinduzi

Ndelakindo: Tunapoingiza darasa la kwanza, akifika miaka saba lazima aanze wakati tunajua kuna watoto wengi wamedumaa, hio ni dhambi kubwa, mfumo tulionao ni ule tulioachiwa na mkoloni.

Mwigamba: Hata ufaulu wa sekondari umeshuka mpaka viwango vimebadilishwa, tutahahakikisha tunaongeza motisha katika sekta ya elimu kuvutia watu na waliopo wabaki kwenye sekta ya elimu.

Jacob: ADC sera zinaeleza wazi, tatizo lilipo ni viongozi wanaosimamia elimu si wabunifu mpaka tunapata mashaka juu ya elimu zao, mwanafunzi wa darasa la kwanza anapokuwa na masomo kumi atawezaje kuyaelewa haya masomo kumi, msingi mbovu unaleta matokeo mabovu.

Swali kutoka kwa mdau wa JamiiForums; Miaka 50 hamna uhakika wa lugha gani inayofaa, mnadhani lugha gani inafaa kufundishia?

Ndelakindo; Asili ya binadamu huwezi kuheshimika bila kutambua lugha yake. Kiswahili ndio lugha inayotutambulisha dunia hivyo lugha ya msingi itaanza na Kiswahilki na baadae tutaongeza kiingereza kama somo.

Mwigamba; Tungependa watanzania wamudu lugha zote mbili na baadae watanzania ndio wachague, tumekuwa wanyonge kwenye lugha ya kiingireza, lazima tuboreshe ufahamu kwenye lugha ya kiingereza.

Jacob; Tumesaini mkataba wa dunia kama kijiji na lugha kubwa inayotumika ni kiingereza, tunawaogopa wakenya kwa ajili ya lugha, napendekeza kuendelea na kiingereza wakati Kiswahli kinakua

Rajab; China wanatumia lugha yao lakini wameendelea, kiingereza itakua somo maalum.


Kigangwala; Ukizungumzia lugha unazungumzia utamaduni wa watu, lugha hii imekuwa na faida katika kutuunganisha, tutaendelea kukipa kipaumbele Kiswahili, hatuwezi kukitupa Kiswahili.

Kwa 'LIVE' updates zaidi tembelea JF Twitter account - https://twitter.com/JamiiForums
 
Habari wakuu. Tupime HOJA zao na kuzijadili kwa mapana.


Kipindi kipo Live StarTv muda huu.


----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------


Mpaka sasa kuna wawakilishi wafuatao na vyama wanavyotoka.


1.Mrs. Ndelakindo Kessy (NCCR/UKAWA)

2.Samson Mwigamba ( ACT Wazalendo)

3.Hamis Kigwangala (CCM)


4.Jacob Joel Samwel ( ADC )

5. Jacob Hoza ( UPDP)
 
Hamis Kigwangala anasema Upinzani wanataka mabadiliko kwa pupa.

teh teh teh teh
 
Tunahitaji wagombea Uraisi , hawa naona kama ni maigizo tuu kwanza sioni mvuto wowote.
 
swali.ni mikakati ipi mmeiandaa ili kuweza kuwaajiri moja kwa moja wanafunz waomaliza vyuo mbalimbali hapa nchini??
 
Back
Top Bottom