njeeseka
JF-Expert Member
- Oct 19, 2012
- 1,374
- 985
Naona awamu hii kidogo game ya siasa imepangwa kisayansi. Ni km vile hatua kwa hatua ili kupisha samaki ale chambo anase. Mpaka sasa inaonekana waliokuwa mamluki ama wafuasi watiifu wa EL wameshatimia ktk list ya kwanza bado ya pili. Ni km kuna awamu mbili zimepangwa ili wasiojua mchezo wajitumbukize ktk shimo. Tv na media zinazosapoti nazo zinamgawo na ahadi kemkem. Maskini wanainchi wasiojua mchezo unaochezwa ndio haooo fuata mkumbo kwa vile tu mtaani amepita mhamasishaji basi wanaunga tela. Siku wakiisha wale walionunuliwa mseme ili tujue sasa wanaohama ni wasafi. Bahati mbaya wanaohama kutoka upande wa ukawa hawatajwi..mifano tuliiona mwaka 2010. Kinachofanyika 2015 ni mfumo tu ulioongezewa ufanisi ili kuhadaa wananchi. Bahati mbaya sana anayepiga kura anakuwa alone ..hamna wa kumshika mkono. Hapo sasa ndo utamuona mpiga kura yupo kimyaa km anafanya mtihani vile wa kuchagua kati ya A na B ....hamadi mwisho anamkumbuka baba wa taifa.