Suppose NCCR - Mageuzi kweli ikawa Chama kikuu cha upinzani, nini itakuwa nafuu ya CCM?

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Siasa za awamu hii tangu Rais John P. Magufuli ashike hatamu ya uongozi wa taifa hili zimekuwa pasua kichwa kwelikweli....

Ndiyo kipindi ambacho siasa za wazi kwa vyama vyote halali kujiimarisha kwa njia ya mikutano ya ndani na hadhara ili kutangaza itikadi na sera zao kwa wananchi na kupanua mitandao yao imekuwa ya upande mmoja (chama kinachoongoza serikali - CCM) huku vyama vingine vikiogelea ktk marufuku iliyo kinyume cha sheria na katiba pasipo kuchukua hatua yoyote madhubuti kupingana na marufuku hiyo batili....

Hilo likiwa hivyo, kwa upande mwingine tunashuhudia makumi ya viongozi hususani wabunge na madiwani wa vyama pinzani na CCM wakihama kwa mbwembwe kuhamia CCM, chama kinachoongoza serikali inayosimamia haya....!

Hawa wahama vyama ukiwatazama namna wanavyoongea wanapokuwa wanajitangaza kuhama vyama vyao, utagundua mara moja kuwa lugha ya miili yao, matamshi yao ya midomo na mioyo yao haviwiañi, yaani ni kama mashariki ilivyo mbali na magharibi zisivyowiana....

Mwanzoni wengi wa wahamaji hawa walikuwa wanapendelea kuhamia chama kinachoongoza serikali, yaani CCM...

Sina hakika, kumetokea nini hata kutokea mgeuko wa ghafla (sudden twist) na sasa wanakimbilia chama kingine kilicho nje ya serikali, NCCR - Mageuzi....

Anyway, labda inaweza kuwa ni kubadili "mkakati" ili nia ovu iliyo nyuma ya mkakati huu isije kugundulika kirahisi na wananchi wa kawaida japo werevu tunaweza kujua kwa urahisi nia na lengo la mkakati huu... Yaani kulinda madhaifu makubwa ya serikali na kiongozi wake mkuu....

Kila mtu anaelewa na kufahamu kuwa, kwa vyama vilivyo nje ya serikali, vyenye majina na nguvu na ushawishi ingalau kwa sasa ni viwili; CHADEMA na ACT - Wazalendo....

Pamoja na kwamba chama cha siasa ni ITIKADI na MALENGO yake kwa kile kinachoamini, lakini uimara wa chama na msambao wake ni added advantage kwa mwanasiasa yeyote makini...

Hivyo, kwa mwanasiasa wa kweli, anayeitazama na kutaka kuilinda kesho yake njema ya kisiasa ni ngumu sana kuhamia chama cha siasa dhaifu kama kilivyo TLP ya Mrema, ama NCCR - Mageuzi ya Mbatia, ama UDP ya John Cheyo na vingine unless kuwe kuna kitu maalumu....

Aidha tangu mfumo wa vyama Vingi uingie Tanzania mwaka 1992, historia inaonesha kuwa ni mwanasiasa mmoja tu mwenye nguvu ya ushawishi aliyehama chama chake kilichomlea, chenye nguvu na ushawishi akaenda alikoenda akabaki na umaarufu wake...

Aidha huyu, si kuhama tu bali badala ya kuhamia chama kingine cha siasa kuendeleza harakati zake za kisiasa, alianzisha chama kipya kabisa, kikasimama na kikawa na nguvu kwelikweli na hivyo umaarufu wake kuendelea....

Huyu si mwingine ni Zito Z.R. Kabwe.

Lakini hiki tunachokiona leo kwa wanasiasa wa "kileo" wakati mwingine na kwa mara moja kundi zima kama vile walikaa wakapanga na kuelewana, binafsi nayaona kama maigizo ambayo hayatawapa matunda yoyote ya kisiasa popote waendalo huko mbeleni....

Nina hakika hata wao wanajua kuwa, mchezo wao hautawanufaisha kwa chochote na kwa lolote kisiasa si kesho wala keshokutwa isipokuwa kama ni biashara ya fedha ( maarufu kununuliwa), ndiyo faida pekee waliyokwisha ipata tayari...

Na kwa wengine kama kina Waitara, Dr Mollel, Dr Slaa, Abdallah Mtolea, Julius Mtatiro, Dr Kitila Mkumbo, Patrobas Katambi, David Kafulila na wengine; nao faida pekee waliyoipata ni zawadi ya vyeo hivyo vya uteuzi walivyopata lakini baada ya hapo hawataonekana mahali.....!!

Sasa kuna hawa kina mama wawili ambao leo tarehe 22/5/2020 strategically na kimitego tego wametumia njia ileile aliyotumia Antony Komu ama Lijuakali kutangaza kuwa wanajitoa CHADEMA na baabaye watajiunga na NCCR - Mageuzi mwingine akiomba kazi ya kufagia ofisini kwa Spika....

Hili halijaja wala kufanyika kwa bahati mbaya. Ni mpango maalumu unaoratibiwa sehemu na wataalamu wa propaganda wa serikali na chama tawala wakiwa na bajeti maalumu ya fedha kwa lengo la kusababisha taharuki upande unaoshambuliwa na ili CCM ipate uhalali na sababu kumwaga mashambulizi yake dhidi ya wapinzani wake kisiasa...

Mwisho kabisa nikajiuliza maswali kadhaa ambayo ndiye yawe msingi wa mjadala huu, kwamba;

1. Tuchukulie kuwa NCCR - Mageuzi kweli ikawa "main opposition party" kama inavyotangazwa sasa kwa kasi na waratibu wa mkakati huu ambao ni wana - propaganda wa CCM na Serikali kwa kupata kura nyingi za Urais, wabunge wengi, madiwani wengi nk; je, CCM itakuwa na nafuu yoyote kwa kuwa sasa si CHADEMA wala ACT - Wazalendo?

2. Kwamba, kama watu waliokuwa CHADEMA, ACT - Wazalendo, CHAUMA nk yaani kina John Heche, Freeman Mbowe, Zito Kabwe, Maalim Seif Shariff Hamad, John Mnyika, Halima Mdee kwa kutaja wachache; itokee wote wakaua vyama vyao na kuhamia NCCR - Mageuzi, CCM ya Magufuli itaweza kupata nafuu yoyote?

Tujiulize tena, ni kwa nini isiwaue watu wenyewe maana vyama ni kama gari tu, likiharibika unapanda lingine unaendelea na safari yako na kufika uendako?

3. Tujiulize pia swali hili kuwa, hivi CCM na Rais Magufuli wanadhani tatizo lao hasa liko wapi? Ndani ya vyama vya upinzani kwa majina au ndani ya CCM na Serikali yenyewe kwa ujumla?

4. Je, wanadhani tatizo lao ni uwepo wa jina la chama cha siasa chenye jina la CHADEMA au ACT - Wazalendo na kwa hiyo wakifuta majina hayo na hayo wanayodhani ni matatizo yao yanakuwa yamekwisha?

I personally don't get it. Maana chama (CCM) chenye dhamana ya kuhakikisha ustawi wa nchi na wananchi hata kupewa mamlaka ya kuunda serikali, badala ya kuwekeza MUDA na RASRIMALI za nchi kupanda ustawi huo, sasa kimewekeza kwenye biashara ya watu na propaganda kwa kila jambo....

Kwa mwenendo huu, nchi kama ya kwetu kupata maendeleo ya kiuchumi na kijamii inaweza kuchukua miaka mingi sana kama mambo haya hayatabadilika haraka....!!
 
Itakawa nafuu ya CCM kwa kuwa lengo lao la kukifanya chama cha NCCR kuwa CCM-B litakuwa limetimia
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Tanzania inahitaji maendeleo na kuondoa umaskini uliotukuka sio kila siku kusifiana na kuhama vyama. Hata ikibaki ccm itapata changamoto tu za kukosolewa. Siku nchi umaskini ukiisha ndo tusherekee sio upumbavu wa watu kutaka madaraka basi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania tuna tatizo la watu, hatuna tatizo la vyama, kwa mantiki hiyo CCM haijawahi kuwa tatizo bali mtu moja mmoja anaweza kuwa. Kwa kuwa tuna watu wengi wenye matatizo katika jamii yetu; wakikushanyika pamoja matokeo yake yanaweza kutabirika na hicho ndicho kinachotokea.

Zaidi ya hapo ni stori kufurahisha genge.
 
Zitto hakuanzisha ACT. Rudia historia na jielimishe alafu urudi.

Nisaidie historia ya ACT - Wazalendo, ilianzishwa lini mwanzilishi ama waanzilishi wake....

Hakuna ubaya wowote wewe kufanya hivyo. Ndiyo maana ya mjadala....

Inawezekana mimi nimepitiwa, sijui ama nimesahau...
 
Tanzania tuna tatizo la watu, hatuna tatizo la vyama, kwa mantiki hiyo CCM haijawahi kuwa tatizo bali mtu moja mmoja anaweza kuwa. Kwa kuwa tuna watu wengi wenye matatizo katika jamii yetu; wakikushanyika pamoja matokeo yake yanaweza kutabirika na hicho ndicho kinachotokea.

Zaidi ya hapo ni stori kufurahisha genge.

Asante, nami ndivyo ninavyoamini...

Watu wakibadilika, mazingira na hali zetu za kimaisha itabadilika...

CCM haina tatizo, watu waliomo humo na mifumo waliyojijengea kujilinda ndiyo tatizo kuanzia viongozi down to the members...

Vivyo hivyo CHADEMA, ama ACT - Wazalendo ama NCCR - Mageuzi nk tatizo siyo chama kwa jina bali ni watu, kuanzia viongozi bottom to the members...
 
Nimewasikiliza hao akina mama wawili nikabaini kwamba na wao wanalalamikia kunyanyaswa kingono na kijinsia. Haya yamekuwa ni madai ya muda mrefu watu, hasa wabaya wa CHADEMA, wamekuwa wakisema kwamba ndani ya CHADEMA viti maalumu kwa akina mama hutolewa kama zawadi baada ya kufanya na kuendelea kufanya kazi maalumu.

Haya madai sasa yamepata kasi mpya, zamani walikuwa ni washabiki wa CCM ndio walikuwa wakiyasema haya na tukawa tunayapuuza, ila sasa hawa waliokuwa wakiambiwa kwamba wanapewa viti maaamu baada ya kufanya na kuendelea kufanya kazi maalumu wanajitokeza na kuthibitisha hilo.

Alianza Gekul na sasa hawa sijui Sokombi ma Masele. Gekul alienda mbali zaidi na kusema walikuwa wanataka kuendelea kuutweza utu wake kwa maana kwamba alishatwezwa na sasa kulikuwa na juhudi za kuendelea kumtweza. Huyu alikuwa si wa viti maalumu lakini utu wake ulitwezwa, je hawa wa viti maalumu si ndio kabisa!

Kama madai haya ni sahihi pamoja na ya matumizi yasiyoelezwa ya pesa za michango basi ni dhahiri shairi kwamba kuna shida ndani ya CHADEMA; CHADEMA wanatweza wanachama wao!
 
mambo ya kususia bunge kama wanawake yatapungua kwa kiasi kikubwa sana, sababu nccr wana amini katika umoja wa kujenga nchi kwa ncjia ya kuosoana sio kususa.
 
Wahuni watakuwa wametimiza lengo lao la KUIUA Chadema. Kwani wanajua fika kwamba Chadema iko mioyoni mwa Watanzania walio wengi na kwenye Uchaguzi huru na wa haki Chadema itaibuka kidedea na ushindi wa TSUNAMI Nchi nzima.

NCCR ni chama LEGELEGE wataingia bungeni ili kujaza matumbo yao na wala si kusimamia maslahi ya Watanzania.
 
Umeongea vizuri ila kuna pahali umechemka kidogo mkuu.

Nguvu ya ACT haitokani na ZItto, nguvu ya ACT inatokana na Maalim na kundi lake, Kabla ya ujio wa Maalim ACT ilikuepo kigoma tu. Maalim kaingia ACT na zaidi ya asilimia 80% ya wafuasi wa CUF. Ngome zote zilizokua za CUF zimegeuka kuwa za ACT.
 
Nafuu yao watakuwa relaxed, hawatakuwa wanakimbizwa mchaka mchaka bungeni na hoja nzito za wapinzani.

Kinyago ulichikichonga hakiwezi kukutisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa za awamu hii tangu Rais John P. Magufuli ashike hatamu ya uongozi wa taifa hili zimekuwa pasua kichwa kwelikweli....

Ndiyo kipindi ambacho siasa za wazi kwa vyama vyote halali kujiimarisha kwa njia ya mikutano ya ndani na hadhara ili kutangaza itikadi na sera zao kwa wananchi na kupanua mitandao yao imekuwa ya upande mmoja (chama kinachoongoza serikali - CCM) huku vyama vingine vikiogelea ktk marufuku iliyo kinyume cha sheria na katiba pasipo kuchukua hatua yoyote madhubuti kupingana na marufuku hiyo batili....

Hilo likiwa hivyo, kwa upande mwingine tunashuhudia makumi ya viongozi hususani wabunge na madiwani wa vyama pinzani na CCM wakihama kwa mbwembwe kuhamia CCM, chama kinachoongoza serikali inayosimamia haya....!

Hawa wahama vyama ukiwatazama namna wanavyoongea wanapokuwa wanajitangaza kuhama vyama vyao, utagundua mara moja kuwa lugha ya miili yao, matamshi yao ya midomo na mioyo yao haviwiañi, yaani ni kama mashariki ilivyo mbali na magharibi zisivyowiana....

Mwanzoni wengi wa wahamaji hawa walikuwa wanapendelea kuhamia chama kinachoongoza serikali, yaani CCM...

Sina hakika, kumetokea nini hata kutokea mgeuko wa ghafla (sudden twist) na sasa wanakimbilia chama kingine kilicho nje ya serikali, NCCR - Mageuzi....

Anyway, labda inaweza kuwa ni kubadili "mkakati" ili nia ovu iliyo nyuma ya mkakati huu isije kugundulika kirahisi na wananchi wa kawaida japo werevu tunaweza kujua kwa urahisi nia na lengo la mkakati huu... Yaani kulinda madhaifu makubwa ya serikali na kiongozi wake mkuu....

Kila mtu anaelewa na kufahamu kuwa, kwa vyama vilivyo nje ya serikali, vyenye majina na nguvu na ushawishi ingalau kwa sasa ni viwili; CHADEMA na ACT - Wazalendo....

Pamoja na kwamba chama cha siasa ni ITIKADI na MALENGO yake kwa kile kinachoamini, lakini uimara wa chama na msambao wake ni added advantage kwa mwanasiasa yeyote makini...

Hivyo, kwa mwanasiasa wa kweli, anayeitazama na kutaka kuilinda kesho yake njema ya kisiasa ni ngumu sana kuhamia chama cha siasa dhaifu kama kilivyo TLP ya Mrema, ama NCCR - Mageuzi ya Mbatia, ama UDP ya John Cheyo na vingine unless kuwe kuna kitu maalumu....

Aidha tangu mfumo wa vyama Vingi uingie Tanzania mwaka 1992, historia inaonesha kuwa ni mwanasiasa mmoja tu mwenye nguvu ya ushawishi aliyehama chama chake kilichomlea, chenye nguvu na ushawishi akaenda alikoenda akabaki na umaarufu wake...

Aidha huyu, si kuhama tu bali badala ya kuhamia chama kingine cha siasa kuendeleza harakati zake za kisiasa, alianzisha chama kipya kabisa, kikasimama na kikawa na nguvu kwelikweli na hivyo umaarufu wake kuendelea....

Huyu si mwingine ni Zito Z.R. Kabwe.

Lakini hiki tunachokiona leo kwa wanasiasa wa "kileo" wakati mwingine na kwa mara moja kundi zima kama vile walikaa wakapanga na kuelewana, binafsi nayaona kama maigizo ambayo hayatawapa matunda yoyote ya kisiasa popote waendalo huko mbeleni....

Nina hakika hata wao wanajua kuwa, mchezo wao hautawanufaisha kwa chochote na kwa lolote kisiasa si kesho wala keshokutwa isipokuwa kama ni biashara ya fedha ( maarufu kununuliwa), ndiyo faida pekee waliyokwisha ipata tayari...

Na kwa wengine kama kina Waitara, Dr Mollel, Dr Slaa, Abdallah Mtolea, Julius Mtatiro, Dr Kitila Mkumbo, Patrobas Katambi, David Kafulila na wengine; nao faida pekee waliyoipata ni zawadi ya vyeo hivyo vya uteuzi walivyopata lakini baada ya hapo hawataonekana mahali.....!!

Sasa kuna hawa kina mama wawili ambao leo tarehe 22/5/2020 strategically na kimitego tego wametumia njia ileile aliyotumia Antony Komu ama Lijuakali kutangaza kuwa wanajitoa CHADEMA na baabaye watajiunga na NCCR - Mageuzi mwingine akiomba kazi ya kufagia ofisini kwa Spika....

Hili halijaja wala kufanyika kwa bahati mbaya. Ni mpango maalumu unaoratibiwa sehemu na wataalamu wa propaganda wa serikali na chama tawala wakiwa na bajeti maalumu ya fedha kwa lengo la kusababisha taharuki upande unaoshambuliwa na ili CCM ipate uhalali na sababu kumwaga mashambulizi yake dhidi ya wapinzani wake kisiasa...

Mwisho kabisa nikajiuliza maswali kadhaa ambayo ndiye yawe msingi wa mjadala huu, kwamba;

1. Tuchukulie kuwa NCCR - Mageuzi kweli ikawa "main opposition party" kama inavyotangazwa sasa kwa kasi na waratibu wa mkakati huu ambao ni wana - propaganda wa CCM na Serikali kwa kupata kura nyingi za Urais, wabunge wengi, madiwani wengi nk; je, CCM itakuwa na nafuu yoyote kwa kuwa sasa si CHADEMA wala ACT - Wazalendo?

2. Kwamba, kama watu waliokuwa CHADEMA, ACT - Wazalendo, CHAUMA nk yaani kina John Heche, Freeman Mbowe, Zito Kabwe, Maalim Seif Shariff Hamad, John Mnyika, Halima Mdee kwa kutaja wachache; itokee wote wakaua vyama vyao na kuhamia NCCR - Mageuzi, CCM ya Magufuli itaweza kupata nafuu yoyote?

Tujiulize tena, ni kwa nini isiwaue watu wenyewe maana vyama ni kama gari tu, likiharibika unapanda lingine unaendelea na safari yako na kufika uendako?

3. Tujiulize pia swali hili kuwa, hivi CCM na Rais Magufuli wanadhani tatizo lao hasa liko wapi? Ndani ya vyama vya upinzani kwa majina au ndani ya CCM na Serikali yenyewe kwa ujumla?

4. Je, wanadhani tatizo lao ni uwepo wa jina la chama cha siasa chenye jina la CHADEMA au ACT - Wazalendo na kwa hiyo wakifuta majina hayo na hayo wanayodhani ni matatizo yao yanakuwa yamekwisha?

I personally don't get it. Maana chama (CCM) chenye dhamana ya kuhakikisha ustawi wa nchi na wananchi hata kupewa mamlaka ya kuunda serikali, badala ya kuwekeza MUDA na RASRIMALI za nchi kupanda ustawi huo, sasa kimewekeza kwenye biashara ya watu na propaganda kwa kila jambo....

Kwa mwenendo huu, nchi kama ya kwetu kupata maendeleo ya kiuchumi na kijamii inaweza kuchukua miaka mingi sana kama mambo haya hayatabadilika haraka....!!
Mimi nashangaa nguvu ccm inayotumia kuua upinzani kila kukicha. Kuna uoga mkubwa sana kwa CDM ambao nafikiri jiwe anaota kila siku HIVI CDM IKATOKEA KUCHUKUA NCHI ITAKUWAJE, NITAKIMBILIA WAPI LEO MBOWE AKIWA RAIS AU HATA MTU MWINGINE TU NDANI YA CDM? Jambo hili linawakosesha usingizi sana jiwe na kundi lake.
 
Back
Top Bottom