Mkenya kaniuliza swali!

Ungemwambia sisi hatubaguani kama wao. Tunafuatilia habari za EA yote ilikujifunza. Wao ukabila tu, Kenya kila kabila lina radio station. Mluo anapenda kusikia habari mbaya za mkikuyu and vice versa. Pole we kwa kutompa jibu, hana lolote ni arrogance yao tu! Kuna mluhiya aliibiwa simu ktk matatu analalamika kwa kujiamini eti lazima aliyeiba ni mkikuyu.
 

Yeye ameuliza hivyo kuonesha kwamba sisi tunafuatilia sana siasa zao, kitu ambacho ni kweli lakini sio kwa watu wote, kuna baadhi ya watu wanafuatilia mambo mengi na ndiyo jinsi walivyo.. kuna Wakenye pia wanaojua siasa zetu vizuri.. mimi ningemjibu hivi "Kutokana na machafuko yaliyotokea uchaguzi uliopita siasa za kenya zimepata umaarufu hasi na ndiyo sababu tunategea masikio siasa zenu kuona safari hii nini kitajiri"

 
just tell him sisi sio wabaguzi kama wao
ndio maana tumesita kukubali baadhi ya vipengele vya jumuia ya afrika mashariki.
TV zetu wanaonyesha news za east afrika ziwe njema au mbaya,wao hawako hivo..
 
Mbona mimi sijui mambo yao na siasa zao? Kwani mimi sio mTZ?
 
Mbona mimi sijui mambo yao na siasa zao? Kwani mimi sio mTZ?
Labda tu haufwatilii na kuangalia vyombo vyetu vya habari, vinginevyo lazima tu ungejua kwamba Wakenya wanafanya uchaguzi, ungejua wagombea Uraisi wote pamoja na vyama vyao, ungejua walikuwa na mdaharo kwa maana ulirushwa live TZ, na pia leo utajua kwamba Raisi wa Kenya yuko Tanzania kwani itatangazwa nchi nzima na kesho magazeti yote vichwa vikuu vya habari vitakuwa ziara ya Raisi wa Kenya Tanzania !
 
Jibu ni rahisi sana. Vyombo vyetu vya habari (magazeti, itv, tbccm, cnten) zinahabari za Africa mashariki, wakati wakenya vyombo vyao havina habari za 'eti Africa Mashariki)... Tumezidi kujikomba sana.
 

Unadhani vyombo vya habari vya Kenya huwa havioneshi habari za TZ? Au Kikwete akienda Kenya hawamtangazi? Kwa sababu hawako interested hawafuatilii, the same na kwangu!

Na sisi tuache kufuatilia ya wengine kwa kweli, kuna mambo mengi sana tunahitaji concentration kwa huku kwetu
 

Huwezi amini hawatangazi kabisa, na hata Bw. Kikwete akiwa kwenye ziara Nairobi hakuna mtu anajua kama raisi wa TZ yuko mjini, na isitoshe ukinunua magazeti yao wataandika lakini kurasa za ndani tena sehemu ndogo, lkn sisi leo hata mtoto mdogo ukimuuliza atakwambia Raisi Kibaki yuko Dar!

Unajua ITV unaweza kuipata Kenya, lakini huwezi ukakuta Wakenya wamekaa wanaangalia ITV kama sisi tunavyoshinda kwenye Citizen!
 

Well said.
 
Just because your friend doesn't know anything about Tz politics doesn't mean all Kenyans feel the same way. I know so many Kenyans who constantly follow closely everything that happens in Tanzania.
 
Hapo kajisifia na kujiona kuwa wao wako juu kuliko tz that's why unafuatilia siasa za kwao na yeye ana mpango na za tz.
 
Kijakazi, yaani ulishindwa hata kumwambia kuwa "SISI RAISI WETU NI HANDSOME BOY, anaendaga ulaya kila siku, anapiga picha na masupa staa, na Obama anamshobokea"?
labda ndiko asili ya obama ndo maana tunaifuatilia sana
 
Last edited by a moderator:
Tattizo ni press.Tz, watu wengi wanasoma gazeti zipi? Eti Diamond bla bla bla, freemason bla bla bla. Kenyan press ina deal na issues za jamii, ziwe nzuri au baya.hio inawafanya wageni kutonunua gazeti za kiswahili za Tz. In short, tatizo ni press sio wananchi.
 
Kuweza kumpa MwanaAfrika Mashariki mwezetu jawabu murua na lenye kutosheleza,ni vema turejee kidogo Historia ya Elimu yetu kidogo na pia harakati za ndani ya nchi yao.
1.Serikali ya Tanzania, chini ya Utawala wa awamu ya Kwanza ilitilia mkazo umuhimu wa kupandikiza hisia, fikra na mitazamo ya kizalendo kwa nchi yetu na hata kwa bara la Afrika kwa ujumla,chini ya dhana ya Pan Africanism.Tutakumbuka,kuwa, Nyerere na Nkurumah ndio waliokuwa mstari wa mbele katika harakati za kulifanya bara la na Afrika kuwa moja.
Wakisukumwa na hisia,matamanio na mitazamo ya Ki-Pan Africanism,watunga sera ,mitaala na mihustari na vitabu,katika somo uraia ,kabla yake somo la Elimu ya siasa na hata katika somo la historia walitilia maanani umuhimu wa wanafunzi kupata uelewa wakina na wa kutosha juu ya bara la Afrika.Si ajabu wanafunzi tena katika ngazi ya Elimu ya msingi ,wa miaka ya nyuma kidogo kuweza kutaja majina ya viongozi wa nchi mbalimbali katika bara la Afrika kama vile Ahmed Ben Bela wa Algeria,Robert Mugabe wa Zimbambwe, Nkurumah wa Ghana ,Kenyata na Moi ,wote wa Kenya,Mobutu wa Zaire na hata Bedel Bokasa wa CAR.Ni wazi, madhui ya somo la Elimu ya Uraia na Historia hapa nchini yamechangia Watanzania kuwa na hamasa ya kutaka kujua yanayojiri katika nchi jirani na zetu.
2.Huko nyuma,nchi ya Kenya ilifanya bidii za makusudi kuifanya radio ya KBC iweze kusikika katika nchi mbali mbali ikiwemo hapa nchini kwetu.Hatua hiyo,ilitufanya tuweze kufuatilia ,kujua na kuelewa yaliyokuwa yakijiri ndani ya nchi hiyo na hata kujua majina ya baadhi ya miji ndani ya nchi hiyo.Hata sasa,hata baada ya umaarufu wa redio hiyo kupungua,bado,tunaendelea kufuatilia na kutaka kujua yanayojiri kwao.
 

Umenikumbusha sana ndugu yangu siku moja nilitembelea Ubalozi wa Kenya, nikamkuta Kaka mmoja aliponiona alizungumza Kiinereza akionyesha dharau kuhusu elimu yetu sisi Watanzania, nikaona nimuumbue nikamuuliza jina hili la, Johnstone Wa Ngengi Kamau, ni la mtu maarufu sana nchini Kenya je alikuwa nani huyo??? Alianza kubabaika nikamwachia namba yangu ya simu ili akipata jibu anipigie anipe jibu. Alinipigia kunieleza hajui jibu lake. Nikamwambia next time asi-under-rate watu kiasi hicho. Nikamwambia ni Jomo Kenyatta, akashangaa sana na akaomba samahani kwa kutumia lugha ya dharau tena ubalozini kwao.

 
Mkuu na ww ungemuliza kwanin wanamuzik wao ha2wafaham lakin we2 wanawajua
 
ubaguzi huwa hauishii sebuleni tu huingia kila mahali,hawa watu ni wabaguzi.
 
Wako sehem yangu ya kazi, wanatabia ya ubaguzi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…