Mke wangu wa ki-malawi (nimebaki njia panda)

Mke wangu wa ki-malawi (nimebaki njia panda)

Kama ni uamuzi wa busara ndio huo. Usimkurupukie kuhusu mtoto. tulia kama alivyokuambia. Ukifika wakati mwafaka utapata mtoto tu. Ila wahi Malawi kabla hajatwaliwa na mwingine. Tena ukifika kule acha kuchunguza chunguza; Wanasemaga; mavi ya kale hayanuki na mume ni yule aliye na mke si mwingine yeyote yule.

ni kweli najihisi mwenye bahati sana kumpata mtoto yule mbali na mswahibu yaliyomkuta akiwa shuleni lakini nimeonekana kidume sana mbele ya watoto wa banda kwani aliwatosa hata wenye fedha zao na watu mashuhuri nilipotambulishwa kwa majirani walimshangaa sana kuolewa na mtu kama mimi ambaye ni wa kawaida sana
wakati wazazi wake wanajiweza sana
 
Habari zenu wana MMU, Miaka takriban miwili na nusu iliyopita nilibahaatika kuwa na mahusiano na binti mmoja mwenyeji wa malawi ambaye baada ya kama miezi 6 ya uchumba tulifunga ndoa.
Kutokana na wazazi wa yule binti kuishi nje ya nchi (malawi) niliwaomba wazazi walezi tumalize kwanza michakato ya then ndo tupange utaratibu wa kwenda kuwaona wazazi husika kwa maana ya kujitambulisha nashukuru walikubali bila kinyongo.

Baada ya kuishi zaidi ya mwaka mmoja na nusu bila mke wangu kutokuwa na dalili zote za ujauzito ilibidi nishtuke na hatua ya kwanza niliyochukua ni kwenda kwa wataalam kwa ajili ya kunifanyia uchunguzi na matokeo yake waliambia sina tatizo lolote kwa upande wa mwenza wangu
niliporudi nyumbani nilimweleza oyte mke wangu na kumuuliza kulikoni miaka inaenda bila dalili zozote za ujauzito alichoniambia hata yeye yuko safi ila inawezekana ni wakati kwahiyo nivute subira kwani mambo mazuri hayataki harakakutokana na jibu hilo nikahisi kuna kitu si hivi hivi nikaomba ruhusa ya siku kumi na nne kazini kwa ajiri ya safari kwenda huko kwao malawi (mzuzu) kwa ajili ya mibaraka na kuonana nao ana kwa ana

Baada ya safari iliyochukua takriban masaa 18 hatimaye tulifika salama na kupokelewa kwa shangwe na vigelege vya kutosha
siku mbili baadae mama-mkwe alinichukua na kwenda kunitembeza nikaone mji na kweli kale kamji ni kadogo lakini kamepangiliawa vizuri sana na kwa sababu tulikuwa na usafiri wetu binafsi tuli-enjioy sana
tukiwa katika maongezi ya hapa na pale nilimtania mama-mkwe japo wajukuu wanasumbua katika maombi yake asilisahau na hilo kwani linampa tabu sana
Lah haula hamadi ndipo yule mama alipoanza kufunguka juu ya yule binti yake kwamba kama hakuwa na taarifa basi
hiyo ndio rasmi ni hivi binti yake kipindi anasoma alipewa mimba na mwanafunzi mwenzake na ile mimba ilimsumbua sana mpaka kupelekea kufanyiwa operesheni na bahati mbaya mtoto alikufa hivyo aliwekewa vijiti na madaktari walimshauri akae zaidi ya miaka mitatu ndo anaweza kubeba mimba
kutokana na taarifa ile ilibidi kesho yake nianze safari ya kurudi bongo huku nikimuahidi aendelee kukaa kwa mwezi mmoja zaidi ili nijipe muda wa nini cha kufanya

Wana JF tumezoea kuzibwa kwa mirija ya uzazi ili mwanamke asizae hivi inawezekana kweli mwanamke akawekewa vijiti sehemu za ukeni na asizae na wala mwanaume usijue?
na kama kweli ni kisayansi au kimitishamba mbali na hilo niegundua kuwa waifu wangu ni material wife hilo pekee yake linaweza sababisha nimuache?
kwanini amenisubilisha badala ya kuniambia ukweli?
hivo vijiti havina side effect kwenye mwili?
wakwe zangu wamekuwa wawazi na kuonyesha ushiriano mkubwa sana kwangu nafikili mila na desturi zinachangia ingekuwa hapa naona wangechuna tu hii inakuwaje?
natanguliza shukrani mawazo yanayojenga ahsanteni na tufunge mwaka kwa salama ni mi wenu KIFIMBOPLAYER

kosa ni kwamba kwanini hakuwa mkweli tangu mwanzo .
lakini mnaweza kuketi na kuongea kiutuuzima kwasababu umesema sector nyingine yuko sawa
tena shukuru mama yake ni mkweli
 
kosa ni kwamba kwanini hakuwa mkweli tangu mwanzo .
lakini mnaweza kuketi na kuongea kiutuuzima kwasababu umesema sector nyingine yuko sawa
tena shukuru mama yake ni mkweli
kutokuwa muwazi ni tatizo nadhan alihisi naweza muwacha kumbe mi nilimpenda kwa dhati ya moyo na ilikuwa ngumu nile ng"ombe mzima nishindwe malizia mkia mss neddy
 
Vijiti vinatumika sana tu kuzuia ujauzito,cha msingi hakikisha hiyo miaka mi3 inatimia kama alivyoshauriwa ndio vikatolewe.
Kama inawezekana nendeni pamoja mkapewe elimu ya uzazi wa mpango na hasa hiyo njia ya vijiti ambayo mkeo ameitumia,maswali yako yote yatajibiwa vizuri huko.
Kukuficha pia usimlaumu sana,inawezekana alihofu kuwa usingejisikia vizuri kujua ali conceive akiwa shule na katika umri mdogo.
Msamehe na muendelee na maisha

Nilitaka nikupe ushauri kama huu wa Ennie. Ufuate nina mategemeo kuwa atazaa na ndoa yako itakuwa ya furaha. Just subira tu.
 
Mkuu kamchukue mkeo ili mradi wewe umeapulisheti kuwa ni waifu material kutokusema ukweli sio sababu ya kumpiga chini.
 
Huyo dada nae inaonekana alikuwa mapepe na alikuwa hajitambue, kwa nini akubali kuwekewa vijiti ina maana ulikuwa mchezo wake kwa hiyo daktari kaona amponye kwa kumuwekea vijiti
 
mkuu mayombo kwenye mkono kuna mahusiano gani na viungo vya uzazi
hiyo ni njia ya uzazi wa mpango, hivyo vijiti viña hormone inayojimimina kwenye damu kwa lengo hilo la kuzuia mimba. Huwa vinachomekwa chini ya ngozi hasa kwenye mikono
 
Wenzetu ni wawazi ndo maana mamá mkwe alikueleza hayo, kama unapenda kweli uwe muelewa ma muendelee na maisha
 
Kuoa/kuolewa na foreigner ni ku risk; akiwa foreigner kwa ki africa ni risk zaidi (unaweza kwenda kwa wala watu)...uliamua kujilipua; hujuhi hata historia...pole; sina la kukushauri maana kuvunja ndoa yaweza ikawa dhambi kutegemea na elimu ulonayo...
 
Wenzetu ni wawazi ndo maana mamá mkwe alikueleza hayo, kama unapenda kweli uwe muelewa ma muendelee na maisha
namupenda sana na lazima tuendelee na maisha
 
Kuoa/kuolewa na foreigner ni ku risk; akiwa foreigner kwa ki africa ni risk zaidi (unaweza kwenda kwa wala watu)...uliamua kujilipua; hujuhi hata historia...pole; sina la kukushauri maana kuvunja ndoa yaweza ikawa dhambi kutegemea na elimu ulonayo...
tabia yake ilikuwa sifa kubwa ya mimi kumpenda na suala la kuvunja ndoa limefuta nisije luka mkojo nikakanyaga mavi nimesamehe bure
 
OK MKUU, kwanza usimuache mkeo maana anakupenda, hlo la kutokukuambia n weakness bt c dhambi,pili kijit huwekwa hata mkonon na kama mama hajakwambia huwezi kujua. tatu mfuate mkeo mwambie kuwa unajua kuwa y yy hapati mtoto na kisha mkapate ushaur kwenye huduma ya uzaz wa mpango,hapo uliza maswal yako yote lkn kubwa iwapo atapata mimba hawezi tena kupata matatzo? mkuu kumbuka kumbadilishia lishe kama inawezekana acha kumpa chips na kunywa maji yaliyowekewa majan ya chai,jitahd kumpa walao kwa wiki maziwa flesh na yai la kienyeji. naamin utakuja kushkru mungu kuwa mke aliokupa mungu kamwe mwanadam asiwatenganishe. mungu akutie nguvu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom