Mke Wangu Sharti ajue Mshahara Wangu????

Sasa mbona kichwa cha habari na maelezo yanatofautiana? Au ni macho yangu mimi?( Maana leo nimekosea nikaalngalia kupatwa kwa jua with my naked eyes).

Yeah.....kidogo mtoa mada kashindwa ku-linkisha title na body......!

Anyway.....kwa ufupi zaidi ni kiaangali yale aliyoyasema kny body:

Hayo yote uliyoyasema hapo juu ni MSHAHARA wa mwanamke na compensation ya machungu anayoyapata toka kwa mume wake na familia yake kwa ujumla - Ref. kamba ya cousin Chrispin......Heshima kwa wanawake!
 
Yeah.....kidogo mtoa mada kashindwa ku-linkisha title na body......!

Anyway.....kwa ufupi zaidi ni kiaangali yale aliyoyasema kny body:

Hayo yote uliyoyasema hapo juu ni MSHAHARA wa mwanamke na compensation ya machungu anayoyapata toka kwa mume wake na familia yake kwa ujumla - Ref. kamba ya cousin Chrispin......Heshima kwa wanawake!


Dah, mkuu NL hapa tupo ukurasa mmoja kabisa! kumbe na wewe umeiona eeh? hahahahaaa
 
salari ni SIRI!
SIRI YA JESHI
akijua tu,hizo bia utazisikia bombani
cha muhimu apate kila anachokihitaji..........
salari hapana
Hapo umenena hata mimi nimekuunga mkono na miguu. Lakini sio eti unaomba pesa ya saloon, unaambiwa hana. Then unamuona yeye nikutesa na mibia everyweekend na jamaa zake ili hali hata huo mashahara huujui. Nina swali pia kwenye hili. Umekuta mume anakuficha matumizi ya hela yake, ukimuomba pesa anasema hana zote zimeishia kwenye bills. Then cku na cku ukafanikiwa kupata kazi na ww. wembe ukawa ni uleule humuonyeshi pesa zako na akiziulizia kwenye majukumu ya ndani, unamwambi na yy zimeishia saloon, wazazi wagonjwa, lipstick etc(kwenye mahitaji yako) maana ni chache huwezi kumudu majukumu ya ndani. Je ni sawa hapo!
 
Sina uhakika kama hili lilishajadiliwa hapa? Ila ningependa kupata maoni ya wadau hapa JF. Niekuwa nikijiuliza mara kwa mara, Mwanamke anawezakuwa anapata Shs. Mil 5 kwa mwezi, Mwanaume Shs. Mil 2, Lakini bado kila kitu utasikia, Baba nanilii, unga umeisha, mchele hakuna, Luku imeisha. Watoto wakitaka school fees ama madaftari, utasikia mwambie babayako. Mama yeye ni Salon ama kujenga kwao na samtymz bila kukwambia!

Hii imekaaje jamani akina Chrispin, Geoff, bht, Bujibuji, carmel, FirstLady 1 , George_Porjie, JS, klorokwini, Lily Flower, MwanajamiiOne, Ngongo, Nguli, Preta, pretty.[/FONT]html"]Pretty, Prodigal Son, Shishi, SMU, Soulbrother, Sumbalawinyo na wadu wengine humu JF.

Michango yenu ni muhimu sana!!!!!!!!

........Mnapokuwa kwenye mahusiano haswa ya ndoa hakuna siri ya pesa baina yenu.Hivyo ni vema kila mtu ajue mshahara wa mpenzi wake.

.......Mwanamke anayefanya kazi ambaye ana kipato chake naye inabidi sehemu ya mshahara wake atumie ndani ya famil. Mwanamke asiyetaka kutumia mshahara wake huyo ni selfish, mtu uwe na mshahara wako halafu kila muda kuomba omba kutoka kwa mume wala haipendezi.

.......Vile vile kuna baadhi ya wanaume hawapendi kufuatilia mishahara ya wanawake zao, mwanaume huyu atachukua kila jukumu ndani ya family kwa pesa yake mwenyewe. Wanaume hawa wanafuata ule usemi wa kwenye bible kwamba mwanaume utakula kwa jasho lake na mwanamke atazaa kwa uchungu.
 
mwanaume ndiye kichwa cha familia,
HUPASWI KUULIZA MSHAHARA WA MKEO

Hapana mkuu!

Sharti ujue hela zake zinaenda wapi!

Kama unajua kabisa kipato chake, na bado huoni/hujui zinakwenda wapi ukae kimya tu!?

No way...
 
Kutokana na ugumu wa maisha ni vizuri kujua mshahara wa mwenzako ili mpange vizuri vitu vya kufanya!!

Navyo jua chochote kinacho husu mwanamke ni chake yaani mshahara ni wake ila chochote kinacho husu mwanaume ni cha wote ndo maana wanasema vyetu cha mwanamke chake.
 
jamani inategemeana, wale wanawake wa enzi za mwalimu, inawezekana, hawa wa ari mpya na kasi mpa, akijua unaibuka na sh ngpi, umekwisha!!!!!!!!

migogoro haiishi,

mshiko ukiwa mkubwa atatka ukajenge kwao kwanza ndio umalizie kabanda kenu, ukibisha, inakuwa ishu, hata haki uliyolipia mahari hupati!!!!!!!!!

kasalari kakaiwa kadogo, basi hesabu umeumia, hata yale maji ulokuwa ukipelekewa bafuni, yanapotea, makamuzi ni mpaka mkomvisi kama unamtongoza upya na aridhie!!!!!!!!!

mkitoka droo, maumivu matupu, ubishi humo ndani, kwa shikh yahaya pana nafuu!

mimi naona inategemeana ni mwamke wa aina gani. nimewahi kuona bwana na bibi wakivburuzana kwenye ATM kisa bibi anaalika wageni wengi nyumbani wakati bwana anadai hana hela ya kutosha! ilibidi wakaprinti salio la akaunti ya mzee ili mama aelewe na abadili tabia ya kuita wageni wengi nyumbani ambao ni mzio kuwahdumia, lakini wapi, bibi alikuja juu akisisitiza kuwa mzee kapata kazi mpya lazima mshahara wake umeongezeka!

sikufuatilia zaidi walifikishana wapi na sakata lao, lakini inathihirisha kuwa huyu mchangiaj niliyemnukuu kamaliza yote!!!!!
 
mwanaume ndiye kichwa cha familia,
HUPASWI KUULIZA MSHAHARA WA MKEO
WALA HUPASWI KUMPA MAJUKUMU YA KUHUDUMIA FAMILIA..........
ni kweli unachokisema lkn pia kama mnashare mshahara mnafika mbali klk kufichana ingawaje wanawake wanahofia kulizwa baadae kuletewa mke wa pili au nyumba ndogo
 
Poleni sana wana JF! Kwa kifupi mimi mke wangu alikuwa anajua si mshahara tu, bali hata allowances nikisafiri nje na ndani ya Bongo.. Kwa kweli alikuwa hakuna anachokifahamu..Na account ilikuwa moja! Ila siku moja ilibidi nisimamishe kila kitu na sasa ni karibu 10 yrs hajui tena kitu chochote.. Kwa kifupi tulikuwa tunajenga mahali fulani, nikampa kiasi kikubwa sana cha pesa akasimamie hy kazi wakati mimi nikiwa safari.. kibaya zaidi ile pesa niliyompa na kazi iliyofanyika haviendani hata kidogo... Tangu siku hy nikasimamisha hilo zoezi.. Lakini kama wewe unaweza sio mbaya ila ipo siku utaacha.
 
kiukweli kabisa vinavyo wahusu waliooana nivema vikafahamika kwa ujumla kwa ajili ya kuu unga upendo wa dhati katika familia mbalimbali
 
Back
Top Bottom