Mke Wangu Sharti ajue Mshahara Wangu???? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke Wangu Sharti ajue Mshahara Wangu????

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Katikomile, Jan 15, 2010.

 1. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Sina uhakika kama hili lilishajadiliwa hapa? Ila ningependa kupata maoni ya wadau hapa JF. Niekuwa nikijiuliza mara kwa mara, Mwanamke anawezakuwa anapata Shs. Mil 5 kwa mwezi, Mwanaume Shs. Mil 2, Lakini bado kila kitu utasikia, Baba nanilii, unga umeisha, mchele hakuna, Luku imeisha. Watoto wakitaka school fees ama madaftari, utasikia mwambie babayako. Mama yeye ni Salon ama kujenga kwao na samtymz bila kukwambia!

  Hii imekaaje jamani akina Chrispin, Geoff, bht, Bujibuji, carmel, FirstLady 1 , George_Porjie, JS, klorokwini, Lily Flower, MwanajamiiOne, Ngongo, Nguli, Preta, Pretty, Prodigal Son, Shishi, SMU, Soulbrother, Sumbalawinyo na wadu wengine humu JF.

  Michango yenu ni muhimu sana!!!!!!!!
   
 2. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Imeandika, mwanamke anatamwacha baba yake na mama yake, naye mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, nao wataoana na kuwa MWILI mmoja!

  Mkishaoana hakuna kubagua mali au kipato cha baba na cha mama! Ukiona hayo yanatokea basi ujue ni mojawapao kati ya mapungufu kwenye hiyo ndoa !!
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  WANAWAKE NAWAHESHIMU SANA!lakini kwenye hiloooooooo..........!well,
  ngoja kwanza...:D
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Jan 15, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sasa mbona kichwa cha habari na maelezo yanatofautiana? Au ni macho yangu mimi?( Maana leo nimekosea nikaalngalia kupatwa kwa jua with my naked eyes).
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mwanaume ndiye kichwa cha familia,
  HUPASWI KUULIZA MSHAHARA WA MKEO
  WALA HUPASWI KUMPA MAJUKUMU YA KUHUDUMIA FAMILIA..........
   
 6. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  leo ni siku ya heshima ya malediz! kuwachalenji iz noti alowed. inabidi uuchune tu. ukiwachalenji tunakuban.
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,451
  Likes Received: 22,404
  Trophy Points: 280
  WANAWAKE TEGEMEZI NI SAWA NA AKILI ZA HUYU KAKA
  [​IMG]
   
 8. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  wana kamsemo fulani wanasema "hela ya mwanamke inaishiaga kwenye lipstiki" i donti knoo how machi zis iz truu.

  on ze aza hendi! jibaba ndio ikulu ya familia. inabidi lawama zianguke kwako kama familia inalala hungry hata kama kamama nyumba kana fezwa kuliko serikali ya japani.
   
 9. GP

  GP JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  dah, mkuu hii sredi inahusika sana,
  ni moja kati ya mada nyeti sana ndani ya mahusiano.
  mi nafikiria kikubwa ni kukaa pamoja na kuangalia yale maeneo muhimu yanayaowazunguka. mjipange na kuelewana vizuri jinsi gani mtayakabili majukumu yenu ndani nyie wawili.
  kwa mfano ulioutoa hapo utakuata mwanamke ndio mwenye kipato kikubwa, kwa vyovyote vile lazima mchango wake uwe mkubwa ukilinganisha na huyo mwanaume hivyo wanatakiwa waelewane nani atafanya nini.
  back to the topic:
  yeye akiwa kama mkeo ANAPASWA KWA 100% AJUE MSHAHARA WAKO NI KIASI GANI, NA WEWE UNAPASWA PIA KUJUA ANALIPWA KIASI GANI, from there ndio itakua rahisi kujua maisha myaendeshaje.
   
 10. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #10
  Jan 15, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  MjasiriamaliShupavu kwa kawaida ndivyo ilivyojengwa na jamii yetu toka enzi za mababu zetu kuwa mwanaume atamlea mkewe na familia yake kwa nguvu zake zote. Na hii ni kwa kuwa zamani wengi wa akina mama walikuwa hawana kipato chochote kwa kuwa hawakuwa wakifanya kazi yoyote (Hii ilichangiwa na mengi including mila na desturi zilizokuwa zikimnyima mtoto wa kike elimu kwa madai kuwa atakwenda kuolewa na kulelewa na mumewe). Kutokana na hayo mke alikuwa na haki kukudai wewe kama mume hayo yote.

  Lakini kwa kadri siku zinavyokwenda mambo yanabadilika, sasa mwanamke amewezakujikomboa kwa kiasi fulani na anmeweza hata kuajiriwa, kujiajiri kwa kuwa wajasiria mali ana uwezo wa kucover some or even all the family necessities. Unfortunately wapo wale ambao wamejilemaza na ule utegemezi ambao wanauchukulia kama ni haki yao na ni wajibu wa mume kufanya hayo yote. Hawa wengi wanafanya either kwa kutokuyajua majukumu yao kama wake (zaidi ya kukupikia, fukia na kukuhudumia kimke) na kuna wale ambao wanafanya kwa makusudi kwa mtindo wa "Pesa yangu ni yangu" HAWA WANAKOSEA NA NI VEMA MKAKAA CHINI KWA UPENDO NA KUZUNGUMZA JUU YA HILI.

  Pili kuna wale wababa ambao hawakotayari kuwashirikisha wenzi wao juu ya ugumu wa maisha! Utakuta mtu analalamika kwa wwenzie kuwa haioni pesa ya mkewe pamoja na kuwa mkewe anafanya kazi lakini hayuko tayari kulizungumza na wifey. Sasa mbaba wa hivi anapofanya haya anakosea kwa sababu mke anawezaona kuwa huhitaji msaada wake kifedha kwa kuwa huulizi.

  KAA CHINI NA WIFEY MWAMBIE MUISHI KWA MALENGO.
  Mwisho wa mwezi leta mshahara wako na yeye alete wake muupangie majukumu huku ukikumbuka kila mmoja wenu kujitolea sehemu kiasi kwa ajili ya personal desires zenu.

  Kuna zile pesa nyingine ambazo mtu anawezapata nje ya mshahara mf. kwa baba amepata takrima sehemu, au dili flani au mke kapata ka allowance kwenye mkutano ambako hakuwa amekatarajia - hizi mtu anawezaamua kuitumia atakavyo yeye mf. baba kujitreat na friends/ mke friends au hata kuwela lace wigs ambazo zinakost up to laki nne e.t.c ili mradi tu amjulishe mwenzi wake asijekuwa amehongwa na demu/bosi e.t.c.


  Aksante
   
 11. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #11
  Jan 15, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Samahani kama nimeku-confyuzi MwanaJ1, ila theme ya thread yangu ilikuwa umuhimu wa Bw. kutangaza mshahara wake kama kweli inasaidia???
   
 12. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #12
  Jan 15, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  unajua salari ni siri ya jeshi....!:D
   
 13. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  ndio ni lazima aujue ..hakuna mbaya hapo Vip unaogopa?
  harafu wewe Geoff kwa nini unasita kutoa jibu hapo?
   
 14. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  ukitangaza salari ,unajichimbia kaburi! kinamama wengine wanaupigia mahesabu mshahara wa disemba kwenye mwezi wa juni . he he he!
   
 15. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  salari ni SIRI!
  SIRI YA JESHI
  akijua tu,hizo bia utazisikia bombani
  cha muhimu apate kila anachokihitaji..........
  salari hapana
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Jan 15, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  Pia inasaidia kupanga bajeti zenu hasa kama mmeamua kuwa na maendeleo katika familia !!!
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  Geoff si kweli mkeo ndio mshauri wako mkubwa sana katika sekta zote so haina haja ya kuwa na siri na salali yako ..kwani unataka uwe unafanya ufisadi mwingine na pesa hiyo????
   
 18. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Wewe fikiria unamwambia mke wangu leo hali ngumu, na hapo anakwambia LUKU imeisha, unaenda kwa mshikaji unakopa hata 20,000 ili ikuvute kidogo msikae gizani, jioni unarudi anakwambia nimenunua wa 10,000, kumi nyingine nimeedea saluni!! Na si kwamba kuna mtoko wa maana ama labda nywele zimechoka sana, sasa je akiujua mshahara hivyo vikao vitakalika kweli ama ndo Serengeti hainyweki tena?
   
 19. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ngoja nitafute ujasiri wa kumteli waifu wangu salari
   
 20. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #20
  Jan 15, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wake wengine si wa kujenga wanakukomoa! Mimi ninamfahamu rafiki yangu mmoja ambaye mumewe alisafiri kwa miaka miwili akaache mshahara wake uwe unaletwa kwa mkewe kwa ajili ya matumizi ya familia yake na kule vijijini. Na bado akawa akihangaika huku mwisho wa mwezi anatuma viEuro vya kutosha tu kwa mkewe. Baada ya miaka miwili bwana karudi nyumbani mke akamkabidhi Mil 6. from zile Euro alizokuwa anamtumia. Mume hakuamini kuwa mkewe hakuwa anatumia zile pesa- wakanunulia gari la ukumbusho. Sasa huyu mke angekuwa kama huyu unayemsimulia hapa Mjasiriamali si angenunua mtaa na kutangaza ufalme au saluni kila siku?

  Ni akili tu ya mwanamke mwenyewe
   
Loading...