Mke wangu nimemtimua leo

Mke wangu nimemtimua leo

Wazee wa zamani walinena 'kuchapiwa ni siri ya ndani' , ungemezea tu. Ila la kuanza kumpenda Mama yako mzazi sijaelewa... ulikuwa humpendi au unataka kumpa mapendo gani zaidi wakati upendo wa mzazi upo tu kiasili...!!!
 
Una balaa kubwa wewe,unahamishia mapenzi yako kwa mama yako? Dunia bye bye
 
Niligundua amenisaliti kwa kiwango cha hali ya juu sasa baada ya kuthibitisha aliyekuwa anamdanganya na yeye ameoa yupo na mke nimeamua nimuache nione kama ataweza kuwaoa wote wawili.
Dah..Kwanini na wewe usimchapie bana? Huu ni udhaifu..🙂
Sina mapenzi tena na mwanamke wacha niamishie mapenzi yangu kwa mama yangu

Dah...dadeki..🙄
 
Ndiyo maana amekusaliti, Wanaume kama ninyi Wanawake huwa aidha wanawamwaga au wanakusaliti kama alivyokufanyia, kwa maana hakuheshimu, Mwanamke anapenda Mwanaume strong na siyo lege lege, sasa tabia uliyoonyesha ya kuleta hapa malalamiko ya Mke wako kumegwa, inaonyesha wewe ni lege lege na ndiyo maana alikudharau na kutembea nje!

Kwa kukusaidia tu jaribu kubadilika na uwe mwanumeme imara ili siku nyingine ukipata mwingine akuheshimu, tatua matatizo na siyo kulia lia, Mwanamke anashindwa kuona tofauti yako na yake na hatimaye kupoteza heshima kwako na kukumwaga!
Siyo Pointi, kama hulidhiki na mwenza wako ni bora kuvunja ndoa kuliko kuzini nje ya ndoa.. Kosa hili ghalama yake ni kubwa sana.
 
Ni uamuzi tu ila ulihakikisha kuwa anakusaliti? Usije Kujutia baadae
 
Mke wangu niliyekaa naye kwa muda wa miezi 7 kwenye ndoa sasa nimeamua kuachana naye moja kwa moja.

Nimemwambia aondoke kwangu baada ya kumpa uthibitisho wa kunisaliti na yeye kuukataa bahati nzuri sijazaa naye na Jana niliamua kuenda naye kufanya pregnant test baada ya kukuta hana mimba nimeamua kuachana naye.

Niligundua amenisaliti kwa kiwango cha hali ya juu, sasa baada ya kuthibitisha aliyekuwa anamdanganya na yeye ameoa yupo na mke nimeamua nimuache nione kama ataweza kuwaoa wote wawili.

Nilimwamini sana nilimpa kila kitu mpaka nikamfundisha kupanda ndege, kutumia baadhi ya vifaa vya ndani kwani alikuwa hana uelewa wa baadhi ya matumizi ya vifaa alivyokuta ndani kwangu.

Sina mapenzi tena na mwanamke wacha niamishie mapenzi yangu kwa mama yangu. Kwa sasa sitaki mwanamke wa aina yeyote niacheni nitulie nikichoka nitakuwa nikienda kwa mama yangu na ananifariji.
Ungekuwa haun shida naye usingeanzisha uzi.
 
Pole sana,jipe moyo mkuu hauko peke yako.Uvumilivu kwenye ndoa ni zaidi ya ushujaa wa vita kuu ya pili ya dunia.
 
Kila kitu ulichokuwa unapewa na mke wako utapewa na mama yako? Pengine na yeye aliona unamapenzi na mama ndiyo maana akatafuta na yeye wa kumpa mapenzi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom