wiseboy.
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 2,932
- 4,534
Wakuu Habari Hii Ni Kweli Kabisa Nami Nimeamua Kuileta Kwenu Kama Nilivyoambiwa Na Rafiki Yangu Ambaye Kila Siku Analia Na Amekata Tamaa Kabisa.Mara Ya Kwanza Nilipoambiwa Kuwa Mke Wangu Ni Mchawi Sikuamini Hata Kidogo Ila Kila Sehemu Habari Zilitapakaa Kuwa Ninaishi Na Mchawi,niliamua Kwenda Congo Sehemu Inaitwa Kalemii Ambako Ili Kupata Dawa Kwa Mganga Wa Jadi Huko Nilichanjwa Mwili Mzima Na Kupewa Dawa Ya Kupaka Machoni Inayoona Wachawi,niliporudi Nyumbani Niliiweka Machoni Hiyo Dawa Usiku Wa Manane Na Ndipo Niliposhuhudia Kwa Mara Ya Kwanza Jambo Ambalo Sitalisahau Maisha Mwangu,pale Kitandani Nikidhani Usiku Wote Ule Nilikuwa Namkumbatia Mke Wangu Kumbe Haikuwa Hivyo,fisi Mkubwa Ajabu Alikuwa Pale Kalala Nilipiga Kelele Kwa Hofu Wanangu Wakaamka Wote Sekunde Ile Ile Fisi Yule Akatoweka Na Mke Wangu Sikumuona Hadi Saa Kumi Alfajiri Nilipomuona Akirudi Akiwa Uchi Mwilini Kajipaka Dawa Nyeusi Alipogundua Nimembaini Akasema Lazima Nife,ndugu Zangu Nifanyeje? Dawa Niliyochanjwa Congo Ndo Inanilinda Sasa.