Supervisor
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 559
- 208
Habari zenu wana JF.
Poleni na mihangaiko ya wiki nzima na leo hatimaye mmerejea kulijenga taifa. Jamani nimejitokeza leo kuwaeleza true story ya maisha yangu na kama kuna ushauri basi nitaupokea. Mimi nilioa kwa ndoa takatifu mwez Sept 2012. Ilipofika Nov 2012 Mke wangu alipata ujauzito na kila m2 kati yetu akawa na furaha.
Sasa ilipofikia muda wa kwenda clinic kama ilivyo ada mnatakiwa kuwa wote ili kuweza kupata nasaha na hatimaye kupima maambukizo ya HIV. Baada ya yote tukapima na yeye Mke wangu akakutwa anaishi na virus va UKIMWI na mimi niko salama kabisa. Kwel alilia sana na Nurse akapata shida sana ya kumbembeleza hatimaye akatulia na tukatoka akwa na uso wa tabasamu bandia.
Tulipofika nyumban kilio kilianza upya na mimi nikionekana usoni sina hata lepe la hofu wakati moyoni nilikuwa naumia sana. Baadae ucku akaniomba kuwa kwa sababu Kanisani tulifundishwa kuwa ndoa yaweza vunjwa kama mmoja wapo akionekana ni malaya. Ki ukwel mimi nilimkatalia nikamwambia Mi ni wake mpaka kifo kitakapo tutenganisha, wala hakuamini macho yake.
Kwa sasa anaonekana yuko at least normal ki akili na leo ameenda kazini. Yeye binafsi ni muumini mzuri na anapenda kwel kuimba na kumsifu Mungu. Naomba ushauri wenu tafadhali.
Pole sana lakini hongera kwa ujasiri wako!Ningekuuliza maswali kadhaa,ila nahisi hayana maana kwa sasa!Hapa tusubiri wadau wengine watasemaje,ila kwa mimi cha kukushauri ni ni kupigia mstari uamuzi wako wa kuendelea kuishi na mkeo wa ndoa.Maadamu mmeshajua tatizo,ni kwenu sasa kukaa chini kumlinda mtoto aliyeko tumboni,na wewe ambaye hujaambukizwa.Amini inawezekana kuishi na mwenza aliyeathirika,bila athari,ilimradi mfuate nasaha za washauri.Na mkiishi kwa furaha,haya mkeo ataishi maisha marefu....
Kwanza mlifanya kosa kufunga ndoa tena takatifu bila kupima ukimwi labda kama mlikuwa tayari mlishandoana kabla ya kufunga ndoa, kama ni hivyo hiyo haikuwa ndoa takatifu but ilikuwa ni ndoa takafujo.
Pili, huo ni mzigo wako ukubali kama ulivyoukubali.
Tatu, katafute sababu ya kwa nini wewe usiambukizwe naye? Kama una aina fulani ya damu isiyopenyesha virusi basi endelea kula tunda kwa raha zako.
Nne, akijifungua salama ndo awe mtoto wenu wa kwanza na wa mwisho-usimpe mimba tena.
Tano, akipoteza uhai wakati wa kujifungua basi oa mwanamke mwingine baada ya kuwa umeshapima mara kadhaa na kugundua kuwa hujaambukizwa. Over
pole kwa masaibu hayo makubwa
Mungu ndio amekulinda hadi leo
cha msingi mpende mkeo,mtunze vema na afuate shauri zote za kitabibu ili ajifunge mtoto asie na maambukizi
tumia kinga sasa kama condom na romance hizo acha
mpokee mkeo,usimnyanyapae au kusema kwa watu.
kama mna family doctor mtafute kwa ushauri zaidi..
Mkuu BUCHANAGANDE, hebu naomba ufafanuzi kidogo kuhusu hili.
Mkuu BUCHANAGANDE, hebu naomba ufafanuzi kidogo kuhusu hili.