Mke wangu ni HIV +, ni mjamzito na anakaribia kujifungua naomba ushauri ili nimnusuru mtoto huyo

Alikuwa hajui kama anao tulipoenda clinic ndio aligundulika ,

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hapa utaalika maswali sana. Mimi nina swali, mkeo hajasema anahisi alipata katika mazingira gani?
Najua sio lazima ngono, napia inaweza kuwa ngono lakini kamwe asikubali kusema ukweli alichepuka.

Au alijamiiana na wewe bila kupima wakati alipopata uja uzito? Mahusiano yenu yalikuwa mapya wakati unampa mimba?
 
Niliwahi kuskia kua mwanamke mjamzito anaweza akapimwa akawa v+ bila maambukizi hebu wataalam malizeni hili


Sent by iOS
Hii kesi ilishawahi kunikuta miaka 7 nyuma niliishi na mwanamke na alipopata ujauzito ndio nilipogundua ameathirika kwa namna moja nilijiuliza mara nyingi tukaenda hospt private kupima ikaonekana anao mimi sina na hapo nikiwaza nilikiwa nimemtorosha kwao basi ikabidi tufate ushauri wa Daktari.

Mpka sasa tunaishi pamoja baada mimi mwenyewe kufanya uchunguzi wangu na kugundua ulitokana na wazazi wake kipindi anazaliwa ndio alipata maambukizi ila alikuwa anaishi vyema na kwa urembo aliokua nao si rahisi mtu kugundua kua anamaambukizi ila mpka sasa mtoto wa kwanza yupo darasa la pili nilijaribu kuachana naye mwaka juzi.

ila nilipokuja kuangukia ni bora hata huyu aliyeathirkia hivyo tukarudiana tena na sasa tunaishi vizuri ikiwemo kufata ushauri wa dr kikubwa ni maelewano tu mana hata mimi huwa situmii kondomu na sina maambukizi yoyote siku zote ninazoishi naye ila nafata ushauli wa kitaalamu zaidi kikubwa nilchojifunza sio kila mschana mwenye maambukizi alifanya ngono hasa hawa waliozaliwa miaka 90
 
Kaka pole sana kwa taharuki uliyopata.

Hiyo case hata mimi nilipata baada ya kuishi na mwanamke kwa takribani mwaka moja, siku moja kwenye movements za kutoka out tukakutana na kituo cha kupima ukimwi, nasi tukakata shauri tupime maana toka tumeanza kuishi hatujawahi kupima.

Sasa baada ya kupima ikaonekana mwanamke ana HIV+ na mimi nina HIV- kumbuka huo ni mwaka mzima tunakulana kavukavu tu, kiukweli ilileta mstuko sana kwetu lakini mwanamke akasema yeye anahuhakika hana na alikataa kabisa.

Baada ya mda kidogo alikuja kupata miscarriage maana hakuna aliyejua kuwa yeye ni mjamzito sio mimi wala yeye mwenyewe. Kiukweli mimi niliamua kuendelea kula mzigo kavukavu coz nilijipa moyo kama nimeweza kupona kwa kipindi chote hicho basi sitapata tena.

Baada ya miezi kadhaa mbele binti akapata ujauzito mwingine, huo tulionote mapema na hivyo tukaenda clinic wote, kwenye vipimo ikaoneka tena kuwa yeye ni mwathirika na mimi ni mzima nahapo clinic wakampa dawa za ARVs akaanze kutumia yeye alizikataa na lakini tulilazimika kuzichukua tu, lakini alikuja kuzitupa baadaye pasipo mimi kujua.

Bahati nzuri akajifungua salama na mtoto hakuwa na maambukizo yoyote na alimnyonyesha mtoto mpka mwaka 1.5 ndipo akamuachisha na mpka sasa yeye kapima zaidi ya mara tatu hana huo ugonjwa na tukaongeza mtoto mwingine mwaka jana watoto wanaendelea vizuri wakiwa na afya zao imara.

Baada ya hiyo scenario ilibidi niingie chimbo la Google na youtube kujua what happened nilikuja kugundua mambo mengi sana kuhusu huu Ugonjwa na mambo yake.

Sasa bro na wewe fanya homework yako.

Ushauri wangu.
USIMUACHE mkeo subiri mpka ajifungue then mkacheki tena afya yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkiambiwa mwende na wenza wenu kliniki mnajiona hayawajusu, matokeo yake ndio haya sasa.
 
Braza vipi watoto walizaliwa salama ? Na je alinyonyesha? Hebu nipe data kamili maana Mimi nipo kwenye mtihani kwelikweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoto wangu mimi yupo salama alinyonyesha miezi sita baada ya hapo akamuachisha kiujumla hata mimi mwanzoni nilipata shida sana nikiwaza mambo mengi sana ila baada ya ushauli niliona ni kawaida
 
Dr. Wansegamila, Mnahangaika bure kumuandikia magazeti, hakuna mjamzito hapa. Hawa wajawazito ambao ni HIV+ huwa wanapewa care ya hali ya juu sana huko clinic. Sasa huyu anaishi dunia ya wapi hadi aje kuomba ushauri Jf eti hajui cha kufanya? Amekuja kuwachoreni tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dr. Wansegamila kama upi Dr? Ninachojua nanilichojipanga nikumzui kutonyonyesha mtoto pindi atakapozaliwa , hatoweza kunyonyeshwa nitamnunulia maziwa tu yanayo ruhusiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanaruhusiwa kunyonyesha miezi 6
Kama mama hana tatizo,umri huu mtoto huwa hana meno ya kung'ata
Na hapa mama anaendelea kutumia dawa,pia mtoto anapewa dawa muda wa miezi 3 ya mwanzo kuzuia maambukizi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnahangaika bure kumuandikia magazeti, hakuna mjamzito hapa. Hawa wajawazito ambao ni HIV+ huwa wanapewa care ya hali ya juu sana huko clinic. Sasa huyu anaishi dunia ya wapi hadi aje kuomba ushauri Jf eti hajui cha kufanya? Amekuja kuwachoreni tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee acha ujinga nipo seriously ktk hali , mke wangu anaenda lakini hakuna care zaidi ya kuchekiwa kama wajawazito wengine ndiomana naomba ushauri hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto wangu mimi yupo salama alinyonyesha miezi sita baada ya hapo akamuachisha kiujumla hata mimi mwanzoni nilipata shida sana nikiwaza mambo mengi sana ila baada ya ushauli niliona ni kawaida
Vip alijifungua kawaida au kwa opereshini? Maana na sikia akijifungua kwa operation kuna risk ndogo ya maambukizi kwa mtoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom