Mke wangu ni HIV +, ni mjamzito na anakaribia kujifungua naomba ushauri ili nimnusuru mtoto huyo

Si anahudhuria clinic? Afuate maelekezo yote anayopewa na wataalamu wa afya huko clinic.

Kama unataka kumsaidia zaidi ni vyema ukaa unaambatana nae huko clinic ili uweze kusikiliza vizuri huo ushauri ili ukiona anakosea uwe unamkumbusha, pia wewe kama mume na baba mtarajiwa kuna masharti utatakiwa uyafuate katika kuchangia mtoto azaliwe bila maambukizi.

Asilimia kubwa ya wamama wenye maambukizi ya VVU siku hizi wanajifungua bila watoto wao kupata maambukizi, isipokua asilimia chache tu kati yao ambao ukifuatilia unakuta hawakufuata ushauri waliokua wanaambiwa clinic.

cordoba
 
Ushauri kama upi Dr? Ninachojua nanilichojipanga nikumzui kutonyonyesha mtoto pindi atakapozaliwa , hatoweza kunyonyeshwa nitamnunulia maxiwa tu yanayo ruhusiwa ,

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu cordoba huo ushauri wa kutonyonyesha umeutoa wapi?

Ndo maana mimi nakwambia ni muhimu sana sana mkuu uwe unahudhuria clinic na mwenzako mkuu, sisi wanaume huwa ni wakorofi sana katika hili, hatutaki kuhudhuria clinic na wenza wetu,halafu tunaokota okota taarifa huko na kuanza kulazimisha wenza weru waende kinyume na maelekezo waliyopewa clinic, na hapo ndo tunachangia sasa mtoto kupata maambukizi.

Mama ananyonyesha vizuri tuu mkuu, bila shida na wala mtoto hatapata maambukizi. Maelekezo ynahitaji madarasa endelevu, ndio maana mimi nimekushauri uende na mwenzio clinic mkuu.

Hiyo hela uliyojipanga kununua maziwa ya formula, ichote kiasi uende na mwenzio hata kwenye private clinic aonwe na daktari bingwa wa wanawake umsikie kwa masikio yako atakachoshauri (this is not necessary,ila nimekushauri hivi kwa jinsi ninavyokuona wewe unapta ugumu wa kuongozana na mwenzio clinic-labda unakwepa msongamano au unaona aibu kwenye hizi clinic za public).

Baadhi ya maelekezo ni haya:
1.Mama mjamzito kutumia dawa za ARV baada tu ya kugundulika,na kuzitumia kwa usahihi bila kumiss dose.

2.Mama atatakiwa kumnyonyesha mtoto wake BILA KUMPA KITU KINGINE CHOCHOTE KILE KWA MUDA WA MIEZI SITA YA KWANZA (mtoto anyonye tuu,asipewe hata maji-muhimu sana).

3.Baba nae apime VVU, na kama ana maambukizi aanze dawa pia,na atumie condom kushirikiana na mama mjamzito kimapenzi-kuepusha baba kumpa virusi vipya mama.

4.mtoto akifikisha miezi sita, aendelee kunyonya na aanze kupewa vyakula vingine,anyonye hadi anapofikisha mwaka mmoja,kisha aachishwe kunyonya (muhimu sana).

5.Na maelekeoz mengine mengi, mkuu NENDA CLINIC NA MKEO KAMA KWELI UNAJALI AFYA YA MKEO NA YA MTOTO WAKO MTARAJIWA.
 
Mkuu naungana na waliouliza swali
Je ameupataje?

Hapa possibility kubwa ni alikua nao na alijua ila hakumwambia msela. Na kama alijua inamaana alikua tayari kweny dozi kwa siri. Wanasema mtu anaetumia dawa kwa kuzingatia anauwezkano mdogo wa kuambukiza mwenzake.

Nadhani inategemea na romance zinazotangulia kabla ya tendo kuanza. Sina uwelewa sana lakini ni maelezo ambayo nimekua nikisia lakni pia hta kauli ya waziri wa afya aliwahi kutaja kweny hotuba zake siku moja
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom