Mke wangu ameambiwa damu yake ni ndogo sana

switch Off

Member
Oct 30, 2019
48
186
Mke wangu ni mjamzito wa miezi 6 kuelekea 7. Jana ameenda kupima damu majibu yamekuja ana damu 7.5 na wakasema ni ndogo sana ni hatari kwa maisha yake. Leo amepeleka majibu hayo cliniki, kwanza wameshangaa kuona ana damu 7.5 na hawajaamini kabisa Mwisho wamemuambia akapime sehemu nyingine ili alinganishe majibu ya kipimo hicho. Kama itatokea majibu yamefanana basi ni hatari, na wamemtishia na kumwambia anaweza kupoteza maisha.

Nahitaji kumsaidia jamani. Naombeni ushauri nifanye kitu gani au nimpeleke hospitari gani ili Damu iongezeke kwa haraka.

NB: Kwa sasa ameshaanza kutumia juice ya viazi kwa ajili ya kuongeza damu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama dakitari ndo katumia neno ndogo akimaanisha chache ama chini ya ujazo wa kawaida hakika tumekwisha..
 
Kiwango cha chini ni 8.5 ikipungua hapo ni hatari
Haemoglobin inatakiwa iwe 12 kama sikosei kwa normal person. Below that especially kwa mama mjamzito ndio yuko at risk zaidi. Mi kwa mwanangu nilimkazania na juice ya Rozella, matembele, maini na pia hospital wanatoaga Iron supplements. Mkazanie sana jamani aongeze hiyo damu before afike 9 months. All the best

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana ndugu jitahidi ale sana mchicha na matembele ili kuongeza damu pia ukiweza mtengeneze juice ya tembele awe anakunywa ni fasta tu anakuwa nayo nyingi
 
switch Off,
Anaweza akahitaji kuongezewa damu ili walau Hb ifike 9 na kuendelea ndio anaweza akaruhusiwa kujifungua. Otherwise anaweza akableed to death wakati wa kujifungua na damu tayari ni chache.

Halafu kwa uchache huo wa damu hata maendeleo ya mtoto yataathiriwa. Vidonge vinaongeza wingi wa damu lakini taratibu sana
 
Mke wangu ni mjamzito wa miezi 6 kuelekea 7. Jana ameenda kupima damu majibu yamekuja ana damu 7.5 na wakasema ni ndogo sana ni hatari kwa maisha yake. Leo amepeleka majibu hayo cliniki, kwanza wameshangaa kuona ana damu 7.5 na hawajaamini kabisa Mwisho wamemuambia akapime sehemu nyingine ili alinganishe majibu ya kipimo hicho. Kama itatokea majibu yamefanana basi ni hatari, na wamemtishia na kumwambia anaweza kupoteza maisha.

Nahitaji kumsaidia jamani. Naombeni ushauri nifanye kitu gani au nimpeleke hospitari gani ili Damu iongezeke kwa haraka.

NB: Kwa sasa ameshaanza kutumia juice ya viazi kwa ajili ya kuongeza damu

Sent using Jamii Forums mobile app

Mawazo tu sio DR

1. Akapuime choo kama kina damu. Kama kina damu wataangalia rangi lakini watafanya kipimo cha colonoscopy wajue inatokea wapi. Kama ana damu kwenye choo inawezekana ni vidonda vya tumbo (kama hamuioni kwa macho lakini choo ni cheusi sana) lakini kama mnaona damu kwenye choo na macho nyekundu inawezekana ni tuma kwenye utumbo mkubwa. Wakiona damu kwenye choo nashauri ufanye colonoscopy .
2. Inawezekana ana madini kidogo mwelini ya chuma ambayo ndiyo yanatengeneza damu mwilini. Hivyo nashauri

Hivi anza na kupima choo na wakati huohuo aende pharmacy kukunua dawa ya vitamins hasa za madini ya iron .chuma
Kama ana mimba itakuwa kwasababu ya madini ya chuma hivyo atumia hizi dawa na kula mboga kwa wingi
 
Mke wangu ni mjamzito wa miezi 6 kuelekea 7. Jana ameenda kupima damu majibu yamekuja ana damu 7.5 na wakasema ni ndogo sana ni hatari kwa maisha yake. Leo amepeleka majibu hayo cliniki, kwanza wameshangaa kuona ana damu 7.5 na hawajaamini kabisa Mwisho wamemuambia akapime sehemu nyingine ili alinganishe majibu ya kipimo hicho. Kama itatokea majibu yamefanana basi ni hatari, na wamemtishia na kumwambia anaweza kupoteza maisha.

Nahitaji kumsaidia jamani. Naombeni ushauri nifanye kitu gani au nimpeleke hospitari gani ili Damu iongezeke kwa haraka.

NB: Kwa sasa ameshaanza kutumia juice ya viazi kwa ajili ya kuongeza damu

Sent using Jamii Forums mobile app
Tumia juisi ya Kiazi cha Beet Root awe anakunywa kwa siku mara 2 asubuhi na usiku kila siku damu itaongezeka haraka.
FAIDA YA BEET ROOT.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom