Mke wangu na salon za ghali!

mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
0
Siyo siri mwenzenu nimechanganyikiwa na sielewi hatma ya ndoa yetu.
Nashindwa kumwelewa mamito wangu! [mama watoto wangu] Tuna miaka 5 ndani
ya ndoa yetu,na tumebahatika kupata 2 kids. Lakini akiaga kwenda salon tu,basi sahau
kama una mke! yaani atakaa uko from morning till down. Na kinachonisikitisha zaidi ana
penda salon za HIGH KLASS- mikocheni,masaki na mbezi ambazo nafikiri ni very expensive.
Mwenyewe kajipangia Jtano na Jpili [yaani x2 kwa wiki]. Jmatano anafanyiwa pedicure,
manicure,na full body srub. Jpili anapendelea kusukwa nywele ndogondogo hivi ndefu au wana
mshonea nywele fake za wazungu na zinakuwa kama zake original,akimaliza hapo anaingia
massage room na anafanyiwa massage. siku hizo anarudi home saa tatu hadi saa nne usiku.
kuna siku nilimshuhudia analipa billservice yake karibu tsh.laki mbili. Nikimgombeza tu anajibu
ulinikuta na maisha haya before na pesa ninazospend ni za kwangu from my job. mmmmh mwe
nzenu ndoa yangu iko matatani au mie ndiye nina matatizo? -Nawasilisha
 
roselyne1

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
1,369
0
pole.vunja ukimya ongea naye mwambie sio kuwa hupendi aende saloon,ungependa afanye hivyo ila kwa kiasi!saloon isimfanye akasahau majukumu yake mengine kama mama na mke.
fanya maombi kimya kimya muombe mungu amfungue mkeo,anasumbuliwa na pepo la ushindani...kujiona expensive...huu ni ubinafsi au kapata mwanaume mwingine?
 
Pearl

JF-Expert Member
Nov 25, 2009
3,039
1,195
Duh pole sana,pesa yote hiyo siwezi kutumia saloon tu hata nikipewa bure(zo hakuna cha bure)jaribu kuongea nae na kumueleza ugumu wa maisha kwa sasa,hata kama mna kisima cha kuchimba pesa lkn kisima hicho kinahitaji maintenance kwa jili ya pesa mo,mueleze malengo n mipango yenu mliopanga,yepi yametimia yepi hayajatimia na kwann,pangeni income and expenditure yenu,lakini ukiona hiyo pia haifanyi kazi jaribu kutafuta saloon kama hizo ananoenda yeye with te same facilities but cheaper in price mpe suprize trip huko atengenezwe na kupendezeswa as long as umeshajua siku zake za kwenda saloon,hope that will work out,pole sana.
 
Nightangale

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
265
170
nywele mara mbili kwa wiki anazifanya nini, masaji kila mara sijui ma pedikua na manikua wat for?
its a complete misuse and abuse of family income/funds.
Afu nimeshtukia kuna huduma nzuri tu unaweza kupata na kwa bei ya kawaida. Lakini hata kama mfuko unaruhusu, mara mbili kwa wiki saluni? sasa hizo nywele ndogo za nini na weave anasuka za nini? Mwambie abaki natural tu.
 
KIBE

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
943
0
Ndo maana wezenu tumeoa walimu lengo ni kuepukana na matatizo kama hayo.
Utafiti unaonyesha asilimia kubwa ndoa ambazo mwanamke ana ela zinaleta shida ndani ya nyumba heshima inakuwa haipo.
Haiwezekani mama mwenyenyumba unaondoka asubuhi hadi usiku ndo unarudi!!!! Wakati kuna majukumu ya mama kama mama anatakiwa ayafanye nyumbani?
Hebu chunguza je kwa mshahara wake anaweza kulipa hizo gharama hizo mana hapa kwa hesabu zaharaka anakwenda saloon kwa mwezi mara 8?kama matumizi hayo makubwa kuliko kipato chake anapata wapi?.na je ni kweli huo muda wote anakuwa saloon? Au ndo kapata papaaa nje?

Tatizo kuiga na ushindani wa wanawake matokeo yake wanajiingiza katika mambo ambayo siyo.
Ushindani na matumizi mabaya ya fedha yanafanya ushindwe kutekeleza majukumu ya maendeleo katika familia.
Pia hata kama una hela mwanamke unatakiwa kuwa na heshima kwa mumeo .
Ushauri hebu kaa na mkeo mwambia vitu ambavyo vinakuboakutoka kwake.
 
Msindima

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,019
1,195
pole.vunja ukimya ongea naye mwambie sio kuwa hupendi aende saloon,ungependa afanye hivyo ila kwa kiasi!saloon isimfanye akasahau majukumu yake mengine kama mama na mke.
fanya maombi kimya kimya muombe mungu amfungue mkeo,anasumbuliwa na pepo la ushindani...kujiona expensive...huu ni ubinafsi au kapata mwanaume mwingine?

Imenichekesha hii.
 
maarufu

Member
Nov 28, 2010
63
0
Kwa nini usimtegee usiku ukamnyoa upara hayo yote yataisha itabaki masaji tu ambayo hata wewe unaweza kumfanyia.
 
Msindima

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,019
1,195
and why is that?

Kilichonichekesha my dear ulipoandika kuwa anasumbuliwa na hilo pepo, nimejaribu kufikiri nikaona ni kweli kwa sababu siku za jumapili ndo siku za kukaa na familia na kupumzika ili kujiandaa na wiki inayoanza sasa inakuwaje mtu aende salon siku nzima kama sio pepo la ushindani na kujiona expensive linamsumbua ni nini zaidi?
 
semango

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
532
195
Siyo siri mwenzenu nimechanganyikiwa na sielewi hatma ya ndoa yetu.
Nashindwa kumwelewa mamito wangu! [mama watoto wangu] Tuna miaka 5 ndani
ya ndoa yetu,na tumebahatika kupata 2 kids. Lakini akiaga kwenda salon tu,basi sahau
kama una mke! yaani atakaa uko from morning till down. Na kinachonisikitisha zaidi ana
penda salon za HIGH KLASS- mikocheni,masaki na mbezi ambazo nafikiri ni very expensive.
Mwenyewe kajipangia Jtano na Jpili [yaani x2 kwa wiki]. Jmatano anafanyiwa pedicure,
manicure,na full body srub. Jpili anapendelea kusukwa nywele ndogondogo hivi ndefu au wana
mshonea nywele fake za wazungu na zinakuwa kama zake original,akimaliza hapo anaingia
massage room na anafanyiwa massage. siku hizo anarudi home saa tatu hadi saa nne usiku.
kuna siku nilimshuhudia analipa billservice yake karibu tsh.laki mbili. Nikimgombeza tu anajibu
ulinikuta na maisha haya before na pesa ninazospend ni za kwangu from my job
. mmmmh mwe
nzenu ndoa yangu iko matatani au mie ndiye nina matatizo? -Nawasilisha

ni kweli alikua hivyo kabla ya kuoana?kama alikua hivyo then it seems ulikubaliana kua na mke wa namna hiyo so itakua ngumu sana kumshape sasa hivi.but kama hakua hivyo then ndio uanze kufatilia tatizo
 
Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,146
1,250
Siyo siri mwenzenu nimechanganyikiwa na sielewi hatma ya ndoa yetu.
Nashindwa kumwelewa mamito wangu! [mama watoto wangu] Tuna miaka 5 ndani
ya ndoa yetu,na tumebahatika kupata 2 kids. Lakini akiaga kwenda salon tu,basi sahau
kama una mke! yaani atakaa uko from morning till down. Na kinachonisikitisha zaidi ana
penda salon za HIGH KLASS- mikocheni,masaki na mbezi ambazo nafikiri ni very expensive.
Mwenyewe kajipangia Jtano na Jpili [yaani x2 kwa wiki]. Jmatano anafanyiwa pedicure,
manicure,na full body srub. Jpili anapendelea kusukwa nywele ndogondogo hivi ndefu au wana
mshonea nywele fake za wazungu na zinakuwa kama zake original,akimaliza hapo anaingia
massage room na anafanyiwa massage. siku hizo anarudi home saa tatu hadi saa nne usiku.
kuna siku nilimshuhudia analipa billservice yake karibu tsh.laki mbili. Nikimgombeza tu anajibu
ulinikuta na maisha haya before na pesa ninazospend ni za kwangu from my job.
mmmmh mwe
nzenu ndoa yangu iko matatani au mie ndiye nina matatizo? -Nawasilisha
Kumbe kama ulimkuta akiwa anafanya hayo, kinachokusumbua leo ni nini? Ungetaka kumbadilisha basi ungefanya hivyo tangu kwenye uchumba. Kwa sasa ni too late. Wanaume wengi huwa ni wanafiki, ukimpenda mwanamke basi unajitahidi kuonyesha kwamba umeridhika na anayoyafanya hata kama yanakuboa, hatusemi ukweli kwa kuhofia kumkosa. Ukishampata ndo unakunjua makucha, hapo utamlaumu bure huyo mwanamke.
 
vicenttemu

Member
Nov 16, 2010
43
0
Pole man. Ask God, he 'll show u the way. He ddnt gv u a woman that would b a burden 2 u, he intends u to have a woman that 'll bring happiness to you.
 
babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
7,154
2,000
Kama anatumia pesa yote hiyo kwa salon sipati Picha bajeti yenu kwa mwezi ya köa kitu,inaelekea mko njema sana mkuu,vinginevyo naona kifo cha presha kinakunyemelea
 
Preacher

JF-Expert Member
Aug 25, 2008
327
0
sasa shida ya huyu husband ni kuwa mkewe anaenda saloon expensive au ni kuwa anakawia kurudi saloon au yote mawili yanamchanganya??

Kama ni saloon expensive - basi ndio lifestyle anayotaka huyu wife - naamini hata nguo zake ni expensive; hata nyumba wanayoishi ni expensive; hata magari waliyonayo ni expensive na wakati huyu husband anamchumbia - alikuwa ana outing expensive - na inawezekana familia hiyo ina mshiko wa kutosha - watoto wanasoma expensive school etc. - yaani ni familia ya kujirusha

kuchelewa nyumbani - labda hili ndilo tatizo lako - kama umeshaona hata akilipa - ina maana ulim-escort .......au?? Afadhali ungesikitika kuwa huyu mama hana cha sundays (kwenda kusali) au Fridays .........kama ni moslem ..........yaani ni "kuuchakachua mwili wake" kwa kwenda mbele ............. bila shaka una-muadmire na anapenda kukufurahisha wewe mumewe ...........au???

Ndio shida ya waswahili - kwani hizo fedha si angewasaidia hata watoto yatima na wajane wanaoteseka kuliko kufuja hivyo??? Ongea na mke wako na mwambie Mungu amembariki ili awe baraka kwa wengine pia - hayo maneno ni ya Mungu na yatamgusa moyoni na atabadilika.
 
mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
0
I thank all of u kwa kunipa majibu mazuri na yenye hekima zidi ya mamito wangu.
Siyo siri nakereka na vitu hivyo 2. kupoteza mda salon na kuspend mo money ever
where kwa ajiri ya mwili wake. Pia ni kweli nilimkuta ana mazoea ya kwenda salon,
lakini si salon hizi za expensive? That time alikuwa anakwenda salon za uswazi na
alirudi mapema sana home. Na kuhusu vipato vyetu -yeye ni msomi kidogo na amepata
kazi mzuri kidogo kimshahara,na mimi ni wa A'level ya kuungaunga na naendesha bias
hara zangu ma self [mjasilia mali]. Ahsanteni sana nitajaribu kukaanae tena ili nimpe
somo upya kwa manufaa ya our future.
 
TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,784
2,000
Pole sana mkuu!sijui mlipendeana nini mbaka mkaoana,lakini inavyoonekana mwanamke uliyenaye hakufai kabisa.Tafadhari jipe muda zaidi ili umchunguze zaidi!!
 
LeopoldByongje

JF-Expert Member
Apr 28, 2008
372
0
Huyo sikuwa anapenda Saloon expensive bali amelewa umaarufu na inawezekana ana mtu ambaye anamfinance na anapenda muonekanao wake. Mkuu sipendi kuingilia ndoa yako lakini inabidi ufahamu vionjo vya mkeo na pia gharama zinazoambatana na vionjo hivyo. Hata kama anakazi nzuri hawezi kumudu gharama za saloon laki moja mara bili kwa wiki mara wiki 52 za mwaka ni zaidi ya milioni kumi (100,000/= X 2 = 200000/= x 52 = 10,400.000/=). Kiasi hiki ni kikubwa sana hata kama ni asilimia moja ya mapato bado haiingii akilini. Jaribu kufuatilia usijekuwa una mwezio ambaye anatunza. Maana hayo Massage, manicure nk. Mhhhhhhhhhhhhhhh. Pole mwanakwetu.
 
afrodenzi

Platinum Member
Nov 1, 2010
18,154
2,000
mmhhh kwakweli anaraha sana ...
kweli wanawake tunapenda sana hivyo vitu ..
lakini labda usimgombeze ka ulivyosema hapo juu..
jaribu kuongea naye taratibu tu..
halafu mwambie unamwomba aiweke familia kwanza
kabla vitu hivyo..
usikate kabisa ila apunguze tuu..
maana ka amezoea kufanya hivyo vitu ni ngumu sana kuuacha..
all the best

AD
 
kasimba123

JF-Expert Member
Apr 18, 2010
1,614
2,000
hahahaha napenda lile wazo lililowahi kutolewa kuwa amuambie mkewe kuwa atatafuta nyumba ndogo ije ikae home
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom