Mke wangu mtarajiwa hataki mtoto wake aliyempata kabla hatujakutana atumie ubini wangu

Kuchna daftar yamaanisha ataki kuona jina lako kwenye jina la huyo mtoto wake.that means anampenda huyo jamaa kuliko ww ndio maana bado anataka asisahau hata jina lake.achana na uyo mwanamke ataja kukuumiza
 
Technically Mwanamke mwenzenu anajua tangia mwanzo Baba mpaka ukoo na Familia wamekataa mtoto wake, hata kama akibadili Jina kwanini uumie na kutaka ujadiliane na mtu aliyekubali kumuhudimia mwanao

If someone thinks big there wasn't a point to argue why the man changed child name

Huyu jamaa hajakosea hata kidogo
Wamemkataa Mwanamke sio mtoto.
Kuna sababu nyingi zinafanya uzae na Mwanamke lakini usimuoe, kama vile mimba za utotoni, tamaduni za koo na makabila, kutokuelewana kati ya wazazi kutokuwepo kwa upendo wa kweli n.k.
Kwa hiyo kumkataa Mama sio kumkataa mtoto na mtoto anapokuwa katika umri mdogo anabaki chini ya malezi ya Mama, Baba unapeleka matunzo, Mara nyingi wakina mama wanapokea matunzo lakini hawasemi hii ni changamoto.
 
Natarajia kuoa hivi karibuni na mke mtarajiwa ana mtoto wa miaka 5. Huyu mtoto namhudumia kwa kila kitu na namuonesha upendo wote kama baba yake mzazi.

Kuna shida imejitokeza baada ya kumpeleka mtoto aanze shule (nursery school ). Katika kujiandikisha nikampa jina langu la ukoo (Eg. Ngwengwe) madaftari full mkoba jina nimeandika Kelvin Ngwengwe.

Bhana eeh, mama yake alivyoona madaftari amechana chana, kumuuliza kisa nini mbona umechana madaftari ya mtoto?? Jibu alilonipa limeniacha hoi.

Namnukuu "Huyu mtoto baba yake yupo hai kwanini usitumie jina la ubini wa baba yake mzazi badala yake umetumia jina la ubini wa kwenu! Zaa mtoto wako umuite jina la kwenu"

Maamuzi niliyochukua ni kumpiga chini tu

MREJESHO
Jana ugomvi ulikuwa mkubwa ila nilitumia busara nilikaa kimya sikusema chochote alienda mbali zaidi akasema tuachane kimoyo moyo nikasema umeisha.

Leo asubuhi amekuja na mama yake mzazi kusuluhisha ugomvi binti amekiri kuwa amekosa zilikuwa ni hasira tu.

Maamuzi niliyochukua sikupepesa macho nilimwambia mama kuwa siwezi kuendelea na binti yako pia mahari niliyoitoa nimesahmee.
Mpaka sasa simu yangu ina missed call 80, sms 30
Inasikitisha sana kama mpaka umri huo hata wanyama wanakuzidi akili.

Hivi unaelewa utaratibu wa adaption? Hebu nenda tu kwa vituo vya watoto yatima utake kumchukuwa mtoto umfanye mwanao ndio utajiwa huna akili na huyo mchumba sijui mkeo anakuzidi akili kwa mbali sana.
 
Hivi na wewe na pumbu zako unawezaje kumpa ubini wako mtoto asiye wako bila hata kuongea na mama yake mkakubaliana,kiherehere chako cha kujilipisha ada ndo umnyang'anye mtoto haki zake
Kiufupi hata kama huyo mwanamke unamuona cheap kiasi hiko lakini na wewe ni mjinga mmoja tu
Na sioni haja ya kusitisha huo uhusiano otherwise utoto unakusumbua
 
Ni kweli hukupaswa kumuandikisha jina lako.
Ana baba yake.
Ana cheti cha kuzaliwa.

Ila mamake nae mwehu, ndo achane daftari na kukwambia zaa wako?

Hata mi ningemwacha.
 
Huyo mtoto analipiwa kila kitu na baba yake mzazi, huyo mwanamke alikuwa anakupiga.
Umefanya vyema kutaka kubadili ubini(japo umeujua ukweli) otherwise ungejutia baadae. Hapo lala mbele akitaka tia mimba leo mtoto lakini sio kuoa
 
Wewe ndo mwenye matatizo utampaje jina mtoto asiye wako kama vile sperm zako haziwezi totolesha
Hata ningekuwa mimi hakika ningemwacha, sio kwa sababu amesema mtoto atumie jina la ubini wake, ila kwa reaction ya kupayuka na kutamka maneno kama "zaa wako" aisee, nisingerudi nyuma!

Niliwahi kuwa na mchumba, nimemlipia mahari na karibu kila ndugu yake alikuwa ananifahamu (in short ilikuwa imebaki ndoa tu)

Siku moja alipata safari ya kikazi, akapitia kwa "rafiki" yake wa kiume bila kunipa taarifa, akakaa huko siku mbili, nilipompigia simu akaniambia yupo njiani anarudi, lakini sauti ilionyesha yupo ndani (mwangwi wa lodge) nikamuuliza mbona unanidanganya?

Majibu yake sasa: "Mbona unanichunga chunga ilhali hata haujanioa, usinichunge chunge hivyo, ukinioa bhana" akakata simu, aisee baada ya pale sikumtafuta tena, aliporudi Dar sikumuuliza uko wapi wala kwenda kwake!
Alipokuja kwangu nilimwambia "Usitie mguu hapa mpaka nitakapokuoa, na ufunguo nikamnyang'anya!

Aliniomba msamaha kwa kupiga simu, kuandika msg, na hata kutumia rafiki/ndugu zangu na wake, but kwa aina ile ya majibu niliona kabisa naenda kuvaa Bomu, sikurudi nyuma wala mahari sikudai!

Mpaka leo yupo tu anatoa pongezi status kila wenzake wanapoolewa!
 
I like you manhood

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Natarajia kuoa hivi karibuni na mke mtarajiwa ana mtoto wa miaka 5. Huyu mtoto namhudumia kwa kila kitu na namuonesha upendo wote kama baba yake mzazi.

Kuna shida imejitokeza baada ya kumpeleka mtoto aanze shule (nursery school ). Katika kujiandikisha nikampa jina langu la ukoo (Eg. Ngwengwe) madaftari full mkoba jina nimeandika Kelvin Ngwengwe.

Bhana eeh, mama yake alivyoona madaftari amechana chana, kumuuliza kisa nini mbona umechana madaftari ya mtoto?? Jibu alilonipa limeniacha hoi.

Namnukuu "Huyu mtoto baba yake yupo hai kwanini usitumie jina la ubini wa baba yake mzazi badala yake umetumia jina la ubini wa kwenu! Zaa mtoto wako umuite jina la kwenu"

Maamuzi niliyochukua ni kumpiga chini tu

MREJESHO
Jana ugomvi ulikuwa mkubwa ila nilitumia busara nilikaa kimya sikusema chochote alienda mbali zaidi akasema tuachane kimoyo moyo nikasema umeisha.

Leo asubuhi amekuja na mama yake mzazi kusuluhisha ugomvi binti amekiri kuwa amekosa zilikuwa ni hasira tu.

Maamuzi niliyochukua sikupepesa macho nilimwambia mama kuwa siwezi kuendelea na binti yako pia mahari niliyoitoa nimesahmee.
Mpaka sasa simu yangu ina missed call 80, sms 30
Kwani mtoto ni wako? Mbona kawaida tuu
 
Wewe na singo maza wako wote mmekosea.

Tukianza na wewe ni kweli unahudumia mtoto, ila hukupaswa kubadilisha ubini bila kukaa na mwenzio mkakubaliana. ULIKOSEA KUFANYA MAAMUZI PEKE YAKO.

Tuje kwa singo maza wako, HAJIHESHIMU NA HAKUHESHIMU, ni kweli ulimkwaza na kumkosea ila ilitakiwa akwambie bila kutumia maneno makali kama "zaa wa kwako"

Kumuacha inawezekana ni sahihi au sio sahihi, hayo majibu yake yanatia mashaka.

Kusomesha mtoto na kufanya kila kitu, FANYA KAMA UNAMLEA YATIMA NA USITARAJIE LOLOTE, UKISHINDWA KUFANYA HIVYO NI BORA UACHE KABISA MAANA UTAUMIA ZAIDI YA HAPO.

Ni mimi singo maza mstaafu.
Kumbe JF bado nzuri hivi.Naipenda J F.
 
Natarajia kuoa hivi karibuni na mke mtarajiwa ana mtoto wa miaka 5. Huyu mtoto namhudumia kwa kila kitu na namuonesha upendo wote kama baba yake mzazi.

Kuna shida imejitokeza baada ya kumpeleka mtoto aanze shule (nursery school ). Katika kujiandikisha nikampa jina langu la ukoo (Eg. Ngwengwe) madaftari full mkoba jina nimeandika Kelvin Ngwengwe.

Bhana eeh, mama yake alivyoona madaftari amechana chana, kumuuliza kisa nini mbona umechana madaftari ya mtoto?? Jibu alilonipa limeniacha hoi.

Namnukuu "Huyu mtoto baba yake yupo hai kwanini usitumie jina la ubini wa baba yake mzazi badala yake umetumia jina la ubini wa kwenu! Zaa mtoto wako umuite jina la kwenu"

Maamuzi niliyochukua ni kumpiga chini tu

MREJESHO
Jana ugomvi ulikuwa mkubwa ila nilitumia busara nilikaa kimya sikusema chochote alienda mbali zaidi akasema tuachane kimoyo moyo nikasema umeisha.

Leo asubuhi amekuja na mama yake mzazi kusuluhisha ugomvi binti amekiri kuwa amekosa zilikuwa ni hasira tu.

Maamuzi niliyochukua sikupepesa macho nilimwambia mama kuwa siwezi kuendelea na binti yako pia mahari niliyoitoa nimesahmee.
Mpaka sasa simu yangu ina missed call 80, sms 30
Ulikuwa unatafuta sababu ya kumwacha tu.
Ashakum si matusi. Yaani katika watu maboya wewe unaongoza. Unajua wazi kuwa mtoto syo wako na unakiri umemkuta, Sasa unamwandikisha kwa jina la kwenu ili iweje? Halafu hata huyo mama yake hukumshirikisha usikie atasema nini.
Hata kama ingekuwa baba mzazi wa mtoto hamhudumii bado huna uhalali wa kumwita ubin wa kwenu.
Fanya bidii umpate wako Kama alivyokushauri mama mwenye mtoto/mkeo
 
Back
Top Bottom