Mkuu, hizo ni kachumbari tu za mahaba. Ukiona anavaa hizo ujue anakukubali sana, anakuona ni role model wake kwa kila jambo. Furahia na zidisha mapenzi, wa kwangu singlet zangu anapenda sana, anapenda harufu ya mwili wangu, sikuhoji sana. Na hasa nikiwa safarini, ndio kabisaaa anavaa mpaka boxer, tukiongea kwa skype which we always do, ananioneshea. Kwangu ni jambo la kujivunia...cherish that mkuu, it is rare. Wapo wengi tu wanaodharau waume zao kiasi kwamba hawezi fanya lolote linalomuunganisha na mumewe na inawatesa jamaa zetu wengi sana. We furahia hilo mkuu usidanganywe