Tunaongea kitu kimoja mkuu, mimi nimeelewa kama wewe ulivyoelewa, instagram ni app ambayo iko kwenye simu, na ni kweli inapoteza sana muda!
Sasa
MO11 alichosema ni kwamba, kama jamaa ameshajua mchepuko wa mke wake ni instagram, basi amfumanie mke na huyo instagram na amshushie kipondo instagram ili aache kumchukulia mke wake!
Hizi ni lugha za fasihi, in other sense ni kwamba kama umeshajua tatizo ni nini, piga marufuku matumizi ya hiyo kitu inayoleta tatizo.
Ninasikitika sana na huu utumiaji wa maneno ya kashfa kwa mtu unayekuwa umeshindwa kuelewa naye, kwa nini usimweleweshe mtu bila kumtusi ndugu? Ukumbuke, tunaishi humu kwa majina ya bandia lakini hisia ni zile zile, tusiifanye JF kuwa sehemu ya kutukanana, mpaka mtu anaogopa kuchangia hoja, matusi waachie kina Mkapa ndugu.