Mke wangu kanitenda, naomba ushauri

Mke wangu kanitenda, naomba ushauri

Huyu jamaa inawezekana mama yake anafahamu kinachoendelea na amekipa baraka na inawezekana hao watoto wote si wake ni wa huyo ndugu yake inawezekana jamaa hawezi tia mimba ndio mama yake akajiongeza. Maana haiingii akilini kabisa utoe talaka kwa sababu ya uzinzi mama yako amchukue wife akakae nae!!??
Kuna kilichojificha kwa mama kikubwa sana
 
Mkuu, yaani hadi umefikia kupata ushahidi then bado unakuja kutuomba ushauri...!!??
Anyway, ungekuwa karibu na mimi ningekuchapa makofi ili akili ikukae sawa.
Na kwakuwa sina la kukushauri, naomba tu nikupongeze kwa kupata mafanikio ya kwenda kuishi Europe this coming year
Na mke wake wa talaka 2 ndiye kafanikisha huo mpango.
 
Matatizo hutokea kwa sababu ya kufikiri sana bila maamuzi au kufanya maamuzi bila kufikiri.
 
Aisee kwa uvumilivu huo pepo yako mkuu mmm Sina utani na hivi viumbe mm mke wangu tuligombana tu akaniambia atatoka kingono nje ya ndoa aisee hiyo kauli tu ilitosha kumtimua a talaka juu ikafuata mahakamani na Ni ndoa ya kikristo Sasa wewe muislamu unaogopa nn au unalishwa na mama. Mchelea mwana hulia mwenyewe
 
Kwanza mshukuru Mungu kakujaalia mambo mawili, kuujua ukweli wenye ushahidi na pia kuwa na visenti...mambo haya mawili ni nguvu kubwa kabisa ya kumpiga talaka hata sita ingewezekana na wewe kuhamia upande wa pili wa kupata wa kukuliwaza kwa muda wakati ukipangilia maisha mapya yenye amani.
 
Wee jamaa utakuwa umerogwa sio akili yako, kwa mambo uliofanyiwa ila bado unataka uendelee kufanyiwa unyams na ukatili sio bure dawa bado zinafanya kazi
 
Mm hapa sina cha kukushauri maana ukweli umeujua lakn unajitoa ufahamu kwa kukumbatia matatzo.
Endelea kuyakumbatia matatzo mpaka yatakapoelemea hasa
 
Simamia maamuzi yako ya talaka mbili au ongeza moja kabisa ziwe tatu.
 
kimacho,

Mkuu, kwanza pole sana sana sana kwa unayopitia ...

Lakini, nikutie moyo na kukuondoa shaka - suala lako sio geni, ndoa kama ndoa karibia zote ni ngumu sana na ndio maana kwa sisi wafuata kristo tulishauriwa kama tunaweza kuishi katika usafi wa kiimani then tusioe kabisa.

Katika ndoa kuna vipindi vigumu na vipindi vizuri sana, I mean kuna vipindi vyote na siku zote uamuzi wa kuoa is the biggest risk a human can take so namini hata wewe hukutegemea kuwa it will be a piece of cake - huu sasa ndio muda wa kuonesha ukomavu wako na kama kweli ulistahili kuwa mume.

Ushauri wangu:

1. Kwanza, kaa chini tena, sehemu tulivu na bila jazba na dai kuujua ukweli wote

2. Jipe muda wa kutosha sana kupumzika na kulifikiria hili kwa umakini ukichukulia tayari kuna mtoto/watoto, kwa kuanzia fanya utaratibu wa kuthibitisha kama kweli first born ni wako au lah - Believe me jibu la swali hilo litarahisisha maamuzi mengine yote coz nionavyo, msingi wa yote yanayoendelea ni hilo.

3. Mwisho, ukishajua kama mtoto ni wako au lah - usisahau kuusikiliza moyo wako, maisha ni mafupi sana.
 
acha kumshauri uj8nga
Ss unataka tushaur wote jibu moja amuache??? Mapenz hayashauriki mkuu hata siku moja usije ukajidanganya hilo ,unaweza mshauri weee wakakutana wao wakapeana utam unashangaa jamaa anamwambia unajua fulani alinambia nkuache,mara ww malaya nk hujapata aibu???? Endelea kushaur mahusiano ya watu tu ipo siku utashangaa
 
Ss unataka tushaur wote jibu moja amuache??? Mapenz hayashauriki mkuu hata siku moja usije ukajidanganya hilo ,unaweza mshauri weee wakakutana wao wakapeana utam unashangaa jamaa anamwambia unajua fulani alinambia nkuache,mara ww malaya nk hujapata aibu???? Endelea kushaur mahusiano ya watu tu ipo siku utashangaa
Nakazia Pacha. Kumshauri kuachana naona sio sawa pia.
 
Back
Top Bottom