Aisee wanaume tunatofautiana.
Katika maisha hakuna ninachokiamini kama kusudi la maisha (My purpose), kias nipo radhi kukuacha vizuri sana wewe mwanamke utakayeonyesha dalili za kunifanya nitoke nje ya kusudi langu.
Mke wangu nimekuoa, nimekuelezea malengo yangu katika maisha, kijamii, kifamilia na kiuchumi pia, halafu baada ya muda fulani unaenda against hayo malengo yaani jiandae tu mapema kuondoka.
Kama una kusudi (purpose) fulani katika maisha na unajua kusudi hilo kias kwamba upo tayari kufanya lolote kulifikia kusudi hilo bila kujali wala kumsikiliza mwingine aisee utaishi maisha ya tofauti sana.
Wife mwenyewe anaelewa na huwa narudia sana hili kwake.
Zaidi ya yote pole mkuu, japo kuna mengi katika family na hatujajua nini hasa chanzo mpka mkeo kufanya kitu kama hicho, haya mambo huwa yanaanzia mbali sana.
Ningekuwa mimi hapo nawaunganisha ili waishi wote wanipe chance ya kuishi kusudi la maisha yangu, kiukweli ni kitu ambacho ni muhimu sana katika maisha hata zaidi ya mke.