Mke wangu kachachamaa anataka tuachane!

Mke wangu kachachamaa anataka tuachane!

Tegelezeni

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2009
Posts
268
Reaction score
124
Eti ni kwa sababu kikao cha ukoo kilichokaa juzi kimeamua nimrithi mke wa marehemu kaka yangu aliyefariki mwezi uliopita kwa ajali ya gari.

Kwa mila na desturi zetu inaruhusu mdogo mtu au kaka mtu kumrithi mke wa ndugu yake pale anapofariki. Sasa namshangaa mke wangu kanuna wiki sasa anataka talaka yake aondoke.

Hivi hapa nimechanganyikiwa sijui nifanye nini maana mke wangu nampenda lakini pia nisingependa damu ya kaka yangu ipotee. Lazima mila iheshimiwe...
 
kwa hiyo wewe unataka kumrithi huyo mwanamke au unasemaje.. chengine wewe utakuwa na mambo ya ajabu kumfikiria mke wa marehemu..
 
Jamani!!!! Khaaaaaaaaaaaaaaa!!! hivi haya mambo bado yapo!!! Maweeeeeeeeeeee!!! jamani na magonjwa yoooote hayo lakini binadamu hatuoni, kwani kaka uko upande gani wa utandawazi , maana hizo ni mila potofu ambazo zinazidisha maambukizi ya Ukimwi. Lakini wewe unataka kurithi mke, kwa nn usirithi watoto ukawasomesha? mpk na mama yao? mh! ama kweli ukishangaa ya firauni.
 
hicho kikao cha familia na wewe uliyeridhia hovyoooooo

au mnataka mali za marehemu? Maana kama mna nia ya dhati mnaweza kumsaidia shemeji yako bila kumridhi... Tena kamati nzima ya ukoo mmeshindwa kuja na njia endelevu ya kusaidia zaidi ya hiyo?

Na huyo mwanamke kakubali umridhi? Au mlikuwa mnatamaniana kabla mumewe hajafa?

Anyway najiuliza tu
 
ilitukusaidie vilivyo:- tupe desturi za mila yenu (kabila,Ukoo) na umri wako na umri wa shemeji yako....
ilituweze kusavu ndoa yako A na usipoteze B.
Good luck mume mwema.
 
Aaaaaaaaaaahhhhh!Kwa mfano wewe ndiyo ungekuwa mwanamke, halafu mumeo anataka kurithi mke wa kaka yako ungekubali?
Hapa mie naona unaendekeza njaa.Hizi mila zingine bwana, kwanini usichukue tu jukumu la kusaidia kui-support hiyo familia bila kumuoa huyo mwanamke?
Kwani mungu alipomchukua hakujua kama damu yake itapotea.
wewe sema tu ulimtamani shemeji yako tangu siku nyingi na ulikuwa unasubiri wakati muafaka.
ila kama umedhamiria, bora umpe mkeo talaka akaanze maisha mapya salama kabla haujamletea maradhi kutoka huko unakoenda kurithi.
 
Mkuu mila zetu zinasema hivyo, na mimi siwezi kukataa kwani nitaachiwa laana na wazee kwa kwenda kinyume na mila na desturi za kabila letu
 
Jamani!!!! Khaaaaaaaaaaaaaaa!!! hivi haya mambo bado yapo!!! Maweeeeeeeeeeee!!! jamani na magonjwa yoooote hayo lakini binadamu hatuoni, kwani kaka uko upande gani wa utandawazi , maana hizo ni mila potofu ambazo zinazidisha maambukizi ya Ukimwi. Lakini wewe unataka kurithi mke, kwa nn usirithi watoto ukawasomesha? mpk na mama yao? mh! ama kweli ukishangaa ya firauni.
Ni nani kakwambia kwamba kaka yangu kafa kwa ukimwi?
Nishasema kafa kwa ajali mwezi uliopita
 
Eti ni kwa sababu kikao cha ukoo kilichokaa juzi kimeamua nimrithi mke wa marehemu kaka yangu aliyefariki mwezi uliopita kwa ajali ya gari.

Kwa mila na desturi zetu inaruhusu mdogo mtu au kaka mtu kumrithi mke wa ndugu yake pale anapofariki. Sasa namshangaa mke wangu kanuna wiki sasa anataka talaka yake aondoke.

Hivi hapa nimechanganyikiwa sijui nifanye nini maana mke wangu nampenda lakini pia nisingependa damu ya kaka yangu ipotee. Lazima mila iheshimiwe...

Kwa maamuzi ya kikao cha familia na wewe umelipokea bila kuonna athari zake bora akuache tu maana unaonekana elimu yako haijakukomboa na kukustarabisha!
 
hicho kikao cha familia na wewe uliyeridhia hovyoooooo

au mnataka mali za marehemu? Maana kama mna nia ya dhati mnaweza kumsaidia shemeji yako bila kumridhi... Tena kamati nzima ya ukoo mmeshindwa kuja na njia endelevu ya kusaidia zaidi ya hiyo?

Na huyo mwanamke kakubali umridhi? Au mlikuwa mnatamaniana kabla mumewe hajafa?

Anyway najiuliza tu
Huyo kaka yangu hakuwa na mali wala nini, mimi ndio naonekana kwetu kuwa nina nafuu hivyo nimetakiwa kumrithi mke wa kaka yangu ili nimsaidie kulea watoto na kumtunza huyo mjane
 
ilitukusaidie vilivyo:- tupe desturi za mila yenu (kabila,Ukoo) na umri wako na umri wa shemeji yako....
ilituweze kusavu ndoa yako A na usipoteze B.
Good luck mume mwema.
Mimi ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga.
Ukoo na mwengine sitakueleza
 
Jamani!!!! Khaaaaaaaaaaaaaaa!!! hivi haya mambo bado yapo!!! Maweeeeeeeeeeee!!! jamani na magonjwa yoooote hayo lakini binadamu hatuoni, kwani kaka uko upande gani wa utandawazi , maana hizo ni mila potofu ambazo zinazidisha maambukizi ya Ukimwi. Lakini wewe unataka kurithi mke, kwa nn usirithi watoto ukawasomesha? mpk na mama yao? mh! ama kweli ukishangaa ya firauni.
Kuna kabila moja huku kwenye visiwa vya ziwa victoria, wana tabia ya "KUWATAKASA WAJANE".eti kila mwanamke anayefiwa na mumewe, ili aweze kuolewa na mwanamme mwingine lazima "ATAKASWE", kwa maana kwamba kuna mwanaume(MTAKASAJI) ameteuliwa kwa kazi hii ya kuwatakasa(KUWAGEGEDA) wajane kabla hawajaolewa tena ili wasipate mikosi kwenye ndoa zao.
Sijajua kama huyu mtakasaji ameoa, na kama ameoa, mkewe anajisikiaje wanapoletwa wajane pale kwake kwa ajili ya kutakaswa?
 
Eti ni kwa sababu kikao cha ukoo kilichokaa juzi kimeamua nimrithi mke wa marehemu kaka yangu aliyefariki mwezi uliopita kwa ajali ya gari.

Kwa mila na desturi zetu inaruhusu mdogo mtu au kaka mtu kumrithi mke wa ndugu yake pale anapofariki. Sasa namshangaa mke wangu kanuna wiki sasa anataka talaka yake aondoke.

Hivi hapa nimechanganyikiwa sijui nifanye nini maana mke wangu nampenda lakini pia nisingependa damu ya kaka yangu ipotee. Lazima mila iheshimiwe...

Hivi mpaka sasa kwenye dunia hii kuna watu wenye akili hizi?tena mtu mwenye kujua even kuingia kwa mitandao ya Internet?
I wonder TAMAA zinakusumbua tu wewe!!
 
Aaaaaaaaaaahhhhh!Kwa mfano wewe ndiyo ungekuwa mwanamke, halafu mumeo anataka kurithi mke wa kaka yako ungekubali?
Hapa mie naona unaendekeza njaa.Hizi mila zingine bwana, kwanini usichukue tu jukumu la kusaidia kui-support hiyo familia bila kumuoa huyo mwanamke?
Kwani mungu alipomchukua hakujua kama damu yake itapotea.
wewe sema tu ulimtamani shemeji yako tangu siku nyingi na ulikuwa unasubiri wakati muafaka.
ila kama umedhamiria, bora umpe mkeo talaka akaanze maisha mapya salama kabla haujamletea maradhi kutoka huko unakoenda kurithi.
Wewe wasema, lakini mimi ninafuata mila zetu, hayo mengine hayanihusu, hata mke wangu wakati namuoa alikuwa aanajua kuhusu mila zetu maana kwetu hata shangazi yangu alirithiwa na mdogo wa mumewe aliyefariki mwaka 1985
 
Eti ni kwa sababu kikao cha ukoo kilichokaa juzi kimeamua nimrithi mke wa marehemu kaka yangu aliyefariki mwezi uliopita kwa ajali ya gari.

Kwa mila na desturi zetu inaruhusu mdogo mtu au kaka mtu kumrithi mke wa ndugu yake pale anapofariki. Sasa namshangaa mke wangu kanuna wiki sasa anataka talaka yake aondoke.

Hivi hapa nimechanganyikiwa sijui nifanye nini maana mke wangu nampenda lakini pia nisingependa damu ya kaka yangu ipotee. Lazima mila iheshimiwe...

Mpe talaka yake aende zake kwa amani na MUNGU amjalie huko aendako afanikiwe wala asikukumbuke tena ubaki na mjane wako, unataka kumuua mwenzio na virus. Bado watu badala ya kutafuta hela mnakaa vikao vya uzinzi.

Umejuaje kama huyo mke wa kaka yako anakupenda? Unahisi watoto wake watajisikiaje wakikuona unalala kitanda cha baba yao? Ingekuwa ni mama yako anatembea na baba yako mdogo ungejisikiaje?

Inaelekea ulikuwa unamtamani toka kaka yako akiwa hai!
 
Eti ni kwa sababu kikao cha ukoo kilichokaa juzi kimeamua nimrithi mke wa marehemu kaka yangu aliyefariki mwezi uliopita kwa ajali ya gari.

Kwa mila na desturi zetu inaruhusu mdogo mtu au kaka mtu kumrithi mke wa ndugu yake pale anapofariki. Sasa namshangaa mke wangu kanuna wiki sasa anataka talaka yake aondoke.

Hivi hapa nimechanganyikiwa sijui nifanye nini maana mke wangu nampenda lakini pia nisingependa damu ya kaka yangu ipotee. Lazima mila iheshimiwe...

Mm nilifikiri haya mambo hayapo tena kumbe bado yapo........ahsante kwa kunikumbusha, mpe mkeo talaka aende zake we endelea kurithi upotofu!!!!!
 
Ni nani kakwambia kwamba kaka yangu kafa kwa ukimwi?
Nishasema kafa kwa ajali mwezi uliopita
Msamehe mkeo, mpe talaka aepuka balaa hili unalolikimbilia. ukimwi, Hepatitis B and c havipimwi kwa macho.
 
kaka hayo ni mambo ya zamani sana ni nisawa na kumkeketa mwanamke,niheri ya kuwa na nyumba ndogo kuliko umrithi mke wa kaka yako.kwanza wajuwa kaka mkubwa ni sawa na baba mzazi!kama walijuwa hilo nisawa na kumlithi mzazi samahani kwa kauri hiyo kwani najaribu kukuweka ktk jamii ya sasa siyo hiyo uliyo nayo.sawa mila ni muhimu bali same time tunatakiwa kuwa out nazile mbovu,kwanza tambua kuna maladhi mengi kwa sasa katika hii dunia.tafakari kwanza kaka.
 
Back
Top Bottom