Mke wangu kabadilika sana.....

Mke wangu kabadilika sana.....

mjanjamjanja

Member
Joined
Feb 11, 2014
Posts
32
Reaction score
2
Habari zenu ndugu wa mmu,
Ni hivi nmebahatika kuoa na kupata babyboy moja.Nmedumu kwenye ndoa miaka 3 na mke wangu.
Nmeishi na mke wangu kwa upendo na furaha.Miezi mitatu iliyopita mke wangu alienda Kwao Mwanza,maana tangia nimuoe hajafika huko.Sasa alivyorudi amebadilika kila kitu kuanzisha furaha,upendo,hanijali tena Yaani amebadilika kabisa sio yule mke wangu wa Kwanza.mi mpaka na hisi Kwao huko wamemfanyia kitu......
Hebu ushaurini nifanye nini maana akili yangu sasa inawaza kumpiga kibuti tu.....talaka
 
Naww nenda kwenu ukirudi unabadilika unarudi home saa 9 au.asubuhi kbs...uone kama hatouliza tatizo.
 
Hapo wewe usisumbuke tafuta nyumba ndogo(mchepuko) ,Ngoma itakua draw
 
Ndoa ina stage jmn,ndo mnaingia ya pili hyo...
Kaa nae umuulize tatizo nini,kibuti sio solution
 
Hajashawishiwa?

Kaa nae chini umuulize kulikoni tangu uliporudi mwenzangu mbona umebadilika, labda anaweza kukuambia kilichomfanya abadilike
 
Hilo ni tatizo sugu kwa wanawake walio wengi (ingawa sio wote) hasa pale anapokuwa anajua kuwa amepata usajili wa kudumu (ndoa takatifu) , hakika ndio wakati amabao huwa wanaanza kutoa makucha yao ambayo waliyaficha wakati wa uchumba.
 
Pole sana jamaa kama hujatoa mahali yote hiyo nayo inaweza kuwa sababu!!!
 
Hilo ni tatizo sugu kwa wanawake walio wengi (ingawa sio wote) hasa pale anapokuwa anajua kuwa amepata usajili wa kudumu (ndoa takatifu) , hakika ndio wakati amabao huwa wanaanza kutoa makucha yao ambayo waliyaficha wakati wa uchumba.

kumbe ila huyu kazidiiii
 
Pole sana,
Muulize tatizo ni nini?
jaribu kumueleza namna alivyokuwa mwanzo na alivyo sasa...then sikiliza majibu yake kuna kitu utapata...
kuanzia hapo unaweza ku step forward...
 
Habari zenu ndugu wa mmu,
Ni hivi nmebahatika kuoa na kupata babyboy moja.Nmedumu kwenye ndoa miaka 3 na mke wangu.
Nmeishi na mke wangu kwa upendo na furaha.Miezi mitatu iliyopita mke wangu alienda Kwao Mwanza,maana tangia nimuoe hajafika huko.Sasa alivyorudi amebadilika kila kitu kuanzisha furaha,upendo,hanijali tena Yaani amebadilika kabisa sio yule mke wangu wa Kwanza.mi mpaka na hisi Kwao huko wamemfanyia kitu......
Hebu ushaurini nifanye nini maana akili yangu sasa inawaza kumpiga kibuti tu.....talaka

oh pole sana!!,naelewa unavyojisikia,njoo tuchepuke kimya kimya wala hutowaza
 
Habari zenu ndugu wa mmu,
Ni hivi nmebahatika kuoa na kupata babyboy moja.Nmedumu kwenye ndoa miaka 3 na mke wangu.
Nmeishi na mke wangu kwa upendo na furaha.Miezi mitatu iliyopita mke wangu alienda Kwao Mwanza,maana tangia nimuoe hajafika huko.Sasa alivyorudi amebadilika kila kitu kuanzisha furaha,upendo,hanijali tena Yaani amebadilika kabisa sio yule mke wangu wa Kwanza.mi mpaka na hisi Kwao huko wamemfanyia kitu......
Hebu ushaurini nifanye nini maana akili yangu sasa inawaza kumpiga kibuti tu.....talaka

Kibuti siyo suluhu kaka, unaweza ukapiga kibuti huyo likaja gubegube ukajuta na kuona heri ya uliyemuacha.

Cha kufanya, tafuta siku mkae kwa utulivu kabisa. Ikiwa mbali na nyumba yenu inweza kuwa ni nzuri sana na uongee nae kwa upendo wa hali ya juu kujua ana tatizo gani linalomfanya abadilike. Wakati mwingine inawezekana bila kujijua na wewe sehemu umebadilika kwa namna moja ama nyingine ila anashindwa kuongea hivyo na yeye kaamua kuwa kubadilika.

Kikubwa kaeni chini muyaongee, ndoa ina mapito mengi na hilo ni moja wapo tu.
 
Muulize kulikoni!? Mbona umebadilika hivyo!?
 
Hilo ni tatizo sugu kwa wanawake walio wengi (ingawa sio wote) hasa pale anapokuwa anajua kuwa amepata usajili wa kudumu (ndoa takatifu) , hakika ndio wakati amabao huwa wanaanza kutoa makucha yao ambayo waliyaficha wakati wa uchumba.

mnatupa shida sana na kashfa sie sio wife material,kwa nini wasiigize..?
 
hanijali tena Yaani amebadilika kabisa sio yule mke wangu wa Kwanza.mi mpaka na hisi Kwao huko wamemfanyia kitu......

shabash!!!!! mwanaume unalalamika hujaliwi na mke wako?

kwanini kuwe na one way communication pekee? upendo wako wewe unausafirisha nyumba ndogo, afu unataka mkeo akupepee mijasho baada ya kuhenyeka huko kwa kidubwasha chako? wewe ulishaonesha upendo wako lini? mbona unataka uhudumiwe wewe?

astakafillulah!.. hebu jifunze kwanza kusambaza upendo ndipo udai upendo, toa kibanzi kwenye jicho lako ndipo utoe kwenye jicho la mwenzio!
 
Mtwange talaka mkuu. Acha kulea nyani utavuna mabua. Mpe uhuru akakae kwao ili awe ananuna vizuri au awe na furaha maana inaonekana ww ndio unamnyima amani. Mtwange talaka mkuu.
 
Back
Top Bottom