Ok9
JF-Expert Member
- Oct 5, 2013
- 4,556
- 4,162
Ilikuwa ndani ya dakika tano tu , Munil aliingia
kwenye baa hiyo akiwa amebadili nguo. Alivaa
gauni nyeupe , refu hadi kufunika miguu wakati
awali alivaa gauni jekundu pia refu !
SASA ENDELEA MWENYEWE :
Alikuja moja kwa moja nilipokaa mimi kwenye
meza ya peke yangu, akanibusu kwanza kisha
akavuta kiti na kukaa huku akiniangalia kwa
uso uliojaa tabasamu laini. Kwa mara ya kwanza
mimi na Munil tulikaa pamoja hapo kwenye baa .
Nilianza kuhisi ni mwanamke wa tofauti sana
kwani walio wengi hawapendi kukaa baa , hasa
kwa mwonekano wake wa kiimani . Hakuwahi
kuniambia wa imani gani lakini jina lake , Munil
lilitosheleza kunijulisha yeye ni nani. Kwa hiyo
kuja kwake baa niliamini kulitokana na upendo
wake kwangu ambao ulitimilika . Nilifurahi sana
maana hata wakati anakaa hakutoa kauli ya
kuashiria kwamba hapendi kukaa baa .
SWALI LA KWANZA KWA MUNIL
Munil sikumbuki kama nimewahi kuisevu namba
yako , lakini ghafla kwenye simu yangu
imeonekana kuseviwa kwa jina la Munil One
halafu sasa Munil Only , ni nini kimetokea
mama ?
Wakati namuuliza hivyo Munil nilimkazia macho
nikiamini ataogopa kama anajua mchezo lakini
wala ! Aliniangalia kawaida na nilipomaliza
akaachia tabasamu lakini huku akisema :
Jamani, mimi ndiyo nikuulize wewe mwenye
simu lakini wewe ndiyo unaniuliza mimi. Mimi
mwenyewe mfano simu yangu, namba unaweza
kuisevu kabisa lakini ukinipigia badala ya
kutokea jina zinaonekana namba tu . Kuhusu
kusevu inawezekana ulinisevu ila umepitiwa na
kumbukumbu, mbona hilo ni suala la kawaida
sana baba.
Munil alivyoniita baba, nilifurahi sana . Nilijiona
mimi ndiyo mimi hakuna mwingine duniani .
Munil alikuwa msichana mzuri sijapata kuona
tangu nimezaliwa . Hata alipoingia pale baa
alitazamwa na kila mtu .
Kuhusu alilolisema la simu, nilikumbuka tatizo
lake hata kaka analo kwenye simu yake,
anasevu jina lakini zinatokea namba kwa hiyo
kaka kila akipigiwa simu huwa na kazi ya
kumuuliza mpigaji , nani mwenzangu? Nikaamini
kuwa huenda ni matatizo ya simu yangu.
Niliyafanya mambo hayo yawe yameisha,
akaagiza soda kama nilivyofanya mimi. Lakini
pia akataka na sambusa mbili kwa kumwambia
mhudumu. Wakati tunakunywa huku yeye
akisubiri sambusa zake , mimi nilihisi muda
umekwenda na anaweza kumaliza soda yake bila
kinywaji kuletwa kwa hiyo nikamuhimiza
mhudumu aharakishe.
Usijali baba, nitakwenda mimi mwenyewe ,
alisema Munil , mimi nikainama kuangalia meseji
kwenye simu yangu, kuinua kichwa nikaona
sambusa kwenye kisahani cha chai ,
nikashtuka. Nani kaleta ? niliuliza . Kisa cha
kuuliza ni kwa sababu kuinamisha kwangu
kichwa chini kusoma meseji na kuinua ilikuwa
ndani ya sekunde kama kumi tu, halafu
nilipoona hiyo sahani sikumwona mhudumu
akiondoka kwenye meza yetu na wala
sikumwona Munil akirudi kuja kukaa .
Kwa wakati ule haikuwa rahisi kusema yote,
lakini baada ya kuyapitia yaliyotokea ndiyo
maana nayasema haya kwani niligundua
baadaye sana kwamba nilikuwa nimepatikana
kwa mke wangu ambaye alikuwa nusu ni mtu ,
nusu ni jini kamili .
Nilipata wakati mgumu sana kuwaza kuhusu
sambusa , Munil aliniambia amezifuata yeye
lakini kusema ule ukweli hakuzileta yeye na
wala hazikuletwa na mhudumu wa baa ile .
Nilinyamaza tu lakini akili ikiendelea
kuchangamka kuwaza .
Baba, aliniita Munil baada ya kuwa kimya kwa
muda mrefu .
Niambie mama .
Utakwenda kuzika ?
Kwani mwili unakwenda kuzikwa wapi ?
Lushoto .
Itabidi niende sijui ? We unasemaje ?
Twende wote.
We utaenda?
Mimi tena , yaani ndugu halafu nikose ?!
Basi na mimi nitaongozana na wewe.
Sawasawa.
Siku hiyo baada ya kuachana na Munil
nilikwenda nyumbani. Niliwaambia majirani
kwamba nitasafiri kwenda Lushoto , Tanga kwa
mazishi . Lakini kwa sababu ya uchovu niliamua
kutokwenda msibani kulala mpaka kesho yake
ambapo ningesafiri , hata kaka nilimwambia
hivyo.
Ilikuwa usiku wa saa nne nikiwa kitandani,
nilimkumbuka Munil kwamba hatujawasiliana kwa
muda mrefu , tangu tulipoachana kule baa ,
nikachukuwa simu ili nimtwangie lakini kabla
simu haijaita , mlango mkubwa uligongwa,
nikakata simu na kuuliza .
Nani ?
Munil .
Nilishtuka , nikaguna kwanza na kujiuliza
mwenyewe:
Amepajuaje hapa au hanitafuti mimi.
Nakuja, nilisema kwa sauti nikitoka kitandani.
Nilifungua mlango, nikakutana na macho ya
Munil. Safari hii alikuwa mzuri zaidi ya wakati
wowote ule . Alizidi kuwa mweupe pee! Aliwaka
mtoto kama Mwarabu vile . Akaachia tabasamu .
Karibu Munil.
Asante, alisema akiingia ndani.
Umepajuaje hapa Munil ?
Nimeulizia .
Umeniuliziaje ? Maana sijawahi kukwambia
naitwa nani.
Si unaitwa Abigael jamani au ?
Ndiyo lakini lini nilikwambia hilo jina langu
Munil?
Na wewe bwana , hebu tuyaache hayo .
Niliamua kuyaacha kweli kama alivyotaka Munil ,
nikamkaribisha chumbani huku nikimuuliza :
Msibani umeaga unakwenda wapi ?
Je, nini kiliendelea hapo ?