Mke wangu hataki wageni

Mke wangu hataki wageni

au aende na mtu WA kumsaidia kabisa sio mke ageuke housegirl,nishaona watu wanakuja kujifungua kwa watu akifika kila kitu apewe Hana pesa ya matumizi,hata ya usafiri kwenda hospital Hana ,mke huyo kachomoa Ana akili kama zangu
Kuna binadamu hawana aibu.....
Hadi pesa ya matumizi
Pyeeeee
 
Hata mi nisingekubali,akianza kuugua nani aanze kuhangaika?akiumwa uchungu kumpeleka hospital,kupeleka chakula hospital,akijifungua kumpikia Mara kumfulia khaaa,aende kwa wakwe zake au ndugu zake,siku hizi watu tupo busy,mkeo yupo sahihi
au kama anakuja aje na msichana wa kazi kabisa wa kukesha nae hospitali
Ubinadamu siku hizi ni wakuutafuta sana
 
Mademu hawapendani sana sasa mtu tena ni watu inavyoonekana wanakuja zaidi ya mmoja sasa hofu ni nini je, alimwambia kwamba yeye ndio atamuudumia au aje tu akae mpaka muda wa kujifungua?! Je alimwambia kwamba atakuwa tegemezi kwao?!

Kama atakuja na msaidizi na hela ya matumizi kuna tatizo gani?

Hivi nyie mademu wa jf wakati mnajifungua wakina nani waliwasaidia na wao walikuwa wanasema hivyo hivyo wakati mnawaita waje kuwasaidia?!
 
Ubinadamu siku hizi ni wakuutafuta sana

huo ubinadam malipo Ni maudhi au hujui,tatizo wanaume hawajihusishi na shughul za nyumbani,ndio maana twasema kama mume ataweza kumhudumia huyo mjamzito amlete uone kama ataweza kumfulia na kumpikia na kwenda kukesha hospital tatizo likitokea
 
Mademu hawapendani sana sasa mtu tena ni watu inavyoonekana wanakuja zaidi ya mmoja sasa hofu ni nini je, alimwambia kwamba yeye ndio atamuudumia au aje tu akae mpaka muda wa kujifungua?! Je alimwambia kwamba atakuwa tegemezi kwao?!

Kama atakuja na msaidizi na hela ya matumizi kuna tatizo gani?

Hivi nyie mademu wa jf wakati mnajifungua wakina nani waliwasaidia na wao walikuwa wanasema hivyo hivyo wakati mnawaita waje kuwasaidia?!

walitusaidia mama zetu SI mtu baki
 
Huyo mama ako anatofauti gani na wewe na mwanamke mwingine

Mbona wewe unamuona mwanamke mwezako kero na mama ako alikuona kero?

khaa nadhani hatuelewani,tatizo Ni kuanza kuhudumia mjazito au huelewi,yaan Mama yangu umfananishe na mtu baki we hujaelewa
 
khaa nadhani hatuelewani,tatizo Ni kuanza kuhudumia mjazito au huelewi,yaan Mama yangu umfananishe na mtu baki we hujaelewa
Labda sijakuelewa...ila nilifikiri ni jambo la ubinadamu ukizingatia hao jamaa ni marafiki wa muda mrefu/ndugu

Alafu mme-conclude kwamba yeye mwanamke ndio atamuhudumia ila sijaona kama kasema hivyo... Yeye kasema "wageni"...

Nadhani ni jambo ilitakiwa walijadili kwa undani... Lakini inavyoonekana hamtaki justification ya aina yyte ile...ni kwamba hatakiwi hapo... Period
 
mfano nikupe,niliwah ishi kwa dada yangu,walikua wakija hao wageni wajawazito,yaan anaumwa uchungu saa kumi usiku au saa nane usiku mnaamshwa twende hospital,mnapeleka mnarudi home,muanze kuandaa chai kupeleka hospital ,chakula cha mchana mumpikie na cha usiku yaan utatembea mpaka basi ,akijifungua mumfate mrudi nae home,afuliwe nguo zake ,aogeshewe mwanae,yaan wangapi wanaweza hudumia hivi mtu rafiki tu,Kuna kero nyingi tu
 
Sijui kwanini wanawake hawapendani... Sijui kwakweli....
Sio kwamba hatupendan kumbuka mwanaume yeye kakaribisha ila wa kumuhudumia n mkew hakuna tabu ngum kama kulea mimba ya kukaribia kujifungua na kulea mzaz ....n ngumu kuliko unavyodhan ...vyakula ..kufua...kumkanda maji..hapo kama ndio mtt wa kwanza hata kumbeba kumwogesha hajua hata mm ningechomoa ...sorry
 
Wanawake ni viumbe wenye huruma na upendo wa hali ya juu pindi wanapoonyeshwa kuthaminiwa na kuheshimiwa na vile vile ni viumbe hatari pindi wanapohisi kudharaurika au kutokuheshimiwa...
.kimsingi hili suala limekaa kibinaadamu na kiutu zaidi kuliko kushindana na kulumbana...kama vile ambavyo yeye alivyohitaji huduma bora za afya wakati akiwa mjamzito na hatimaye kujifungua salama...ndivyo na mwenzie anahitaji kujifungua swalama na kupata huduma bora za uzazi.....

Vile vile huyo ni mwanamke mwenzie angepaswa kumsitiri kimaumbile....

Vile vile kwa upande wa pili wewe jamaa nawe unahitaji lawama kwa kutomshirikisha mkeo...katika suala linalohitaji maamuzi ya kifamilia...kwa maana kwa asilimia kubwa huyo mama kijacho atakuwa anakaa na my wife wako kwa ukaribu zaidi kuliko wewe...hapo hata kama ukileta ubabe wa kiume hautaweka mambo sawa...bado muda unao wa kujadiliana na mkeo huku ukimsihi amuonee huruma mwanamke mwenzie kwani huko aliko kuna huduma duni za afya.....natumaini kwa kuwa wenzetu wamezaliwa na huruma za hali ya juu atakuelewa na mambo yatakuwa poa....

Kinacho muuma mkeo sio kwamba sio kwamba hapendi ujio wa huyo mama kijacho bali ni kuhisi kudharaulika katika mchakato mzima wa ujio wa huyo mama kijacho wakati ndiye atakayebeba majukumu yote uzazi wa huyo dada hasa ukizingatia kuwa na yeye ni mzazi na anafahamu tabu za uzazi....
 
tumia busara kumuelewesha na kumsihi tu kwa kuwa umekosea kutomshirikisha.
 
Back
Top Bottom