Heri wewe umeliona hili
Wakuu,
Kisa chenyewe ni hiki;
Mwenzenu mke wangu hasomeki. Mimi nina rafiki yangu tangu enzi hizo tuko primary. Huyu jamaa yangu, binti yake kaolewa na sasa ni mjamzito. Kama mnavyojua ujauzito wa mtoto wake wa kwanza huyu rafiki yangu kapagawa kushinda Mkwe wake.
Wanaishi bush, sasa ameniomba binti take aje akae kwangu ili ajisubilishe kujifungua katika hospital nzuri town.Ombi lake lilikuwa la maongezi kwa njia ya simu, mimi kwa haraka haraka bila kumshtua/kumwambia mke wangu nikakubàli.
Nilipofika nyumbani nikamweleza ujio wa wageni hawa. Aisee sikutegemea, mke wangu aliwaka kama Mbogo, na kuanza kuniambia wewe mimba unaijua?
Akakomaa kuwa hataki kuwaona hapa.
Sasa wakuu, wenye wapenzi hii issue ni i handle namna gani? Manake jamaa nimeshamuahidi, sasa kumwambia asije naona soo.
Nipeni mawazo wandugu
Sijui kwanini wanawake hawapendani... Sijui kwakweli....
Sijui kwanini wanawake hawapendani... Sijui kwakweli....
tunapendana sana ila mkee wa jamaa hajiamini tena ni mchoyo anazani mjamzito atamaliza chakula. Tena baada ya kujifungu atamlisha ugari na makande mpaka akome so wajiongeze.
mimi siwezi kumlazinisha mke wangu kubeba majukumu ya mke wa mtu mwenye wazazi, wakwe, wifi zake na wake wenzie.
huo utakuwa ni upuuzi naufanya.
mwisho wa siku mtakuja kulipwa majungu tu.
mke wangu atahudumia ndugu zangu tu tena sio kwa kumlazimisha.
hivi umewahi kuzaa au kuhudumia mzazi? ndio maana wanapendaga watu wazima wawepo nyumbani kwani kazi zingine ni busara na hekima ndio inawaongoza
Pole sana. Kumbe umeolewa.... kwanini bado wajiita miss miss nuru??Mmh mkuu inataka moyo sana, niliwah kukaa na jamaa yake Mume Wangu alivyojifungua hizo kaz nilizokuwa nafanya za mzazi ni shida, kufua nguo za mzazi alizochafua leba ,nikisema hiv wazaz wananielewa, halafu yule bint alikuwa anakula viporo bas ile nguo ilikuja na m... ,karud home habadilish ped mpaka mnguo zinachafuka, kiufup alikuwa mchafu, mvivu, mwez mzima namfanyia kila kitu ,