Mke wangu hataki wageni

Mke wangu hataki wageni

Cassava

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2010
Posts
282
Reaction score
36
Wakuu,

Kisa chenyewe ni hiki;

Mwenzenu mke wangu hasomeki. Mimi nina rafiki yangu tangu enzi hizo tuko primary. Huyu jamaa yangu, binti yake kaolewa na sasa ni mjamzito. Kama mnavyojua ujauzito wa mtoto wake wa kwanza huyu rafiki yangu kapagawa kushinda Mkwe wake.

Wanaishi bush, sasa ameniomba binti take aje akae kwangu ili ajisubilishe kujifungua katika hospital nzuri town.Ombi lake lilikuwa la maongezi kwa njia ya simu, mimi kwa haraka haraka bila kumshtua/kumwambia mke wangu nikakubàli.

Nilipofika nyumbani nikamweleza ujio wa wageni hawa. Aisee sikutegemea, mke wangu aliwaka kama Mbogo, na kuanza kuniambia wewe mimba unaijua?

Akakomaa kuwa hataki kuwaona hapa.

Sasa wakuu, wenye wapenzi hii issue ni i handle namna gani? Manake jamaa nimeshamuahidi, sasa kumwambia asije naona soo.

Nipeni mawazo wandugu
 
ww inaonekana mke wako anakucontrol..so hao wageni bora wasikae kwako,wife anaweza kukutia aibu mbele ya hao wageni ..ukizingatia kuwa ujio wao yy hajaupenda
 
Tell them kuwa wife hatakuwepo home kwa muda so hakuna mtu wa karibu wa kumhudumia huyo mjamzito
 
Mwambie asije kwa sababu huyo wife wako hachewi kumtoa mimba Ohoo!
 
Haina uhusiano na kupendana....
Alipaswa azungumze na mkewe ajue je yupo tayari kumhudumia mzazi?????
Hapo ni kuacha kazi na kufanya kazi........

Kumbuka wema usizidi uwezo

Sijui kwanini wanawake hawapendani... Sijui kwakweli....


Na hapo bado mume wa binti wake na wageni wengine watakaokuja kumuona mzazi
 
Heri wewe umeliona hili


anajua matatizo ya kulea mzazi ndio maana kachomoa.
huwa wanadeka haooo!!
tena anapiga mahesabu ya kuhangaika na mtoto wa rafiki yako, mwenye mume na wakwe zake!!
huyo jamaa yako naye hajielewi kabisa.
 
Fanya maamuzi yoyote magumu tu. inaonekana wife anakucontol

wewe nyumba ni ya familia na pia kama mkewe anamcontrol wats the problem bora ata huyu ni wife sio bibi mwitu...
ifike mahala tutambue nafasi ya kila mmoja ktk familia na kila mtu ashiriki ktk maamuzi haswaa kama ni mke na mume. hamna cha kushikana maskio kwe ndoa…
 
mwambie jamaa waje na mtu mzima wa kumhudumia. wife asifanye chochote labda ishu ndogondogo. akichomoa tena mchomeke kwa nguvu. hata ungemwambia kabla na angekataa bado ingekuwa soo kumwambia rafiki yako
 
Tell them kuwa wife hatakuwepo home kwa muda so hakuna mtu wa karibu wa kumhudumia huyo mjamzito
Watu wasiokuwa na haya watamfungasha huyo mjamzito na shangazi yake wakamlee huyo mwanamkr wakati wa kujifungua nyumbani kwa jamaa!
 
Akijifungua kwa operation God forbid unalo maana hawezi kusafiri kwa muda. Mbona utampikia supu wewe shemeji yake kama wife kachomoa
 
Cassava

Umekosea kutoa maamuzi bila kumshirikia mkeo.Kumbuka usumbuf wote wa kumuangalia mzazi ataupata yeye.Jadiliana na mkeo mshauriane umjibu vp rafiki ako
 
Last edited by a moderator:
Ongea na wife vizuri kama sio tabia yako kuchepuka atakuelewa tu
 
Back
Top Bottom