Mke wangu hataki niendeshe gari alilonunua. Nakereka sana

Maelezo ya mtoa mada yana viashiria vya wazi kuwa hilo gali mke amenunuliwa na mchepuko.
Hata km ni ivo!! Nyota hiyo ni ya mwanaume!!!
siku akiamua kumuacha huyo ke kwa vitimbi hivi!!

Woooote watafirisika ghafla!! Gari litakufa kibudu!! Tena bila kugongwa...mwenye nyota yake muwako kaondoka..

Heshimu na ogopa sana mtu unae nyanyuka nae kimaisha ukawa somebody siku hizi...

Kamatia ndo hirizi yako hiyo amini usiamini.....chunguza uone...uki bugie tu, ukamtema!! si rahisi tena kurudi kwa mstari mnyoofu....jaribu tu uone... Utalia lia umerogwa....hali itakuwambaya zaidi ukienda kujiagua ndo ntolee babaeeee.!!..
 
Mimi nisingegusa hiyo gari. Halafu ndani mkishaanza hiki kanunua mke ni chake basi ndoa si imara tena.
Haya ni Km yaleee!!! yalimkutaga nyarusare alisimuliaga humu jf... Aliposoma ramani akaona hkn maisha hapa...akapiga kimyaaa tu km hajui!!

Siku ya siku akaondoka km anaenda kariakoo ndo nto leee mazima!!
Kule kapiga show si kitoto!! Ana mali mara dufu!! Na ma girl mapyaa!!
 
Kosa number moja: ulikosea sana kujitenga na gari tangu hatua za mwanzoni kabisa, kwakuwa Mzee wa boda yeye kakushusha thamani yako
Ushauri wangu : gangamala ununue gari lingine hilo ndio liwe lako

Jr
La kwako liwe na ke!! Mwee!! litaburuzwa hilo na kupewa kila mtu aendeshe pale kanisani.kazini.Nk
mara utasikia mpeleke mama mchungaji.
Hkn shida!! Mara kanisa linaenda azima viti kwa Bakhresa ni gari lako litatumika kwa hasira ....
Mwaka tu!! gari lako ndembendembe!! Atalitelekeza taaatibu!! Then..

Ataanza "daaa!! Gari langu imara sana. Mpyaa nilinunua!!Angalia lako lilivo chakaa!! sijui ulipewa bureee?

Ndo maana ulitamani gari langu ukanipa mie bovu siyo?? Unanifanyia mie ujanja!! Ujanja siyo??
Haiwezekani unifanyie ivo!!

Cha msingi nunua zuri lako komaa na lako na siku ukipata migari zaidi kifo hichoooooooo!!
 
Kuna mwehu ameropoka kwa sauti hii ni awamu ya kina mama nilipomuuliza unamaanisha nini akasema nilikuwa nachungulia unachosoma Kwenye simu yako alipokuwa anachungulia nilikuwa JF nasoma thread yako mleta mada nadhani aliona thread yako
 
Pole Sana Kaka. Pole Sana kwa mkeo kuwa KERO. Wanawake wenzangu tubadilike jamani. Mume wangu siku anataka kutumia gari.... Namuomba mapema kabisa anipeleke usafiri wa bajaji unapopatikana..... naendelea na ratiba zangu kama kawaida. Nikimaliza narudi nyumbani.... Raha mustarehe... Mapenzi Mubashara😂😅. Mapenzi yana Raha Sana Wanawake wenzangu ... Haya Mambo madogo madogo haya tujifunze kuya-ignore. Tujifunze kujishusha kwenye baadhi ya mambo ambayo tunaweza kufanya na hayasumbui sana.... Kwani utapungukiwa nini? .... Pia Tunapunguza mikwaruzano inayoweza kuepukika. Gari zipo tuu. Cha muhimu Penzi na Raha ya MUME.
Mbona sioni sehemu ya ku like.
 
Kuna baadhi ya mambo ni hulka za wanawake karibu wote some ni tabia binafsi za huyo mkeo; mfano hiyo ya ukosoaji wa namna yako ya kuendesha gari is almost wanawake wengi wapo hivyo, mke wang as well hadi watoto wake hua wanamkosoa na yeye anabakia kucheka tu. Kuna binti mmoja nilikua napiga nae show mara kadhaa, nimeacha baada ya yeye kuolewa, one day nilichukua gari lake nikaenda niliko kwenda, wakati namrudishia akaniomba nimsindikize sehemu, yeye nae kama wife tu, full kukosoa kosoa na wanawake wengine wengi tu.

Kikubwa mkuu, tafuta pesa ununue gari lako, wanawake hawakuumbwa kulea mwanaume, wameumbwa kulelewa na mwanaume. Nataka kusema hivi, siku ukijaaliwa ukanunua gari lako, hiyo ya kukosolewa namna yako ya driving itaendelea, mengine anaweza kuyaacha but hiyo ya kukosolewa itaendelea tu hadi mnazeeka
 
Mke wako mshamba wa magari na limbukeni, mimi hata kama gari alinunia kwa pesa yake mimi ndiyo nitaitumia muda mwingi kuliko yeye
Wanaume wachache sana hapa watakuelewa,ila Mimi nimekuelewa vizuri sana!
 
Achana na Gari yake, ww fanya safar zako bila gari yake ila hakikisha ukirudi sifia Demu aliekupa lift kuwa ana roho ya huruma na ubinadam sana.

Wakati mwingine mwambie kuna rafiki ako wa kike atakuazima gar yake ili yeye asikose kitoka na gari yake
Point
 
Yaani gari Lina shusha thamani ya mtu

Wanawake bhana
Sema Mume nae mpole sana,mi hilo gari ningelichezea na lingekuwa haliwaki bila Mimi! Na Wanawake walivyokua wazembe hawapendi kuendesha Magari yanayosumbua, Jamaa angekua anatoa tu terminal moja kwenye betrii ya gari, alafu Mke wake akitaka kwenda kwenye shughuli zake lazima angemuomba Mumewe ndiyo am drive!!
 
acha hizo mkuu!! Ke kumnyima gari si jambo la siri hilo!! Majirani wanaona.
House girl.
watoto wako.
wageni wa nyumbani mwako wanaona.
Rafiki zako wanaona.
Asa kuna siri gani hapo

Haya sisi humu hatumjui km majirani wajuavyo huenda ni mimi ndo nafanya ivo au wewe!!
Unless otherwise hujui what is siri..

Mpe ushauri tu.dawa anunue la kwake. Lkn kuna hatari ya kuuawa mapema kwa kumjibu hivi...sababu na wewe utamnyima la kwako ataumia.
Dawa yake atakuroga tu ufe!! Hasa mtoto mkubwa akimaliza university.
Na mna mipango ya mbali, eti hadi mtoto mkubwa akimaliza university
 
hiyo ya kukosolewa namna yako ya driving itaendelea, mengine anaweza kuyaacha but hiyo ya kukosolewa itaendelea tu hadi mnazeeka

Aisee umenifurahisha sana kumbe tuko wengi kwenye hii kadhia 😂😂😂😂😂😂

Mimi mke wangu nimemfundisha gari mwenyewe alikua hajui a wala be mpaka amekua dereva na leseni nikamtafutia. Ni zaidi ya miaka mi 5 sasa tangu aanze kuendesha gari. Katika kipindi chote hicho, yeye ameshagonga gari, kukwangua, kupasua taa, vioo, kugonga miti, mageti, nk mara zisizohesabika. Mimi sijawahi kugonga hata inzi!

Cha ajabu sasa nikiwa naendesha mimi utasikia "eh, punguza mwendo bana unakimbia sana" (hapo niko speed 30), "ongeza mwendo, we huoni hilo semetrela nyuma..? Au paki kwanza lipite!", "hii kona umekatia mbali sana", "unaona hiyo gari mbele, unaona..?", "washa indiketa tunaingia pale...", "mpigie honi huyo bodaboda utamvaa", "washa full bana mimi sioni mbele..", "mbona umeovatekia karibu hivyo?"... yaani mi hua saa nyingine naishia kucheka tuu..🤣🤣🤣🤣
 
Mke wako mshamba wa magari na limbukeni, mimi hata kama gari alinunia kwa pesa yake mimi ndiyo nitaitumia muda mwingi kuliko yeye
Tufafanulie zaidi hapa na sisi wa Ke .... Tukuelewe Mkuu🙈🙊
 
Tufafanulie zaidi hapa na sisi wa Ke .... Tukuelewe Mkuu🙈🙊
Baba ni kichwa cha familia, mnapofanya miradi au mipango lazima awe kinara wa kuisimamia, Mfano Ke.. akinunua gari hilo ni la familia na mume hivyo hivyo..kiongozi wa familia ni Me.
 
Back
Top Bottom