Mke wangu hataki niendeshe gari alilonunua. Nakereka sana

Bulichekah

Member
Jan 12, 2014
68
185
Mimi ni mwanaume wa kawaida, nimejaaliwa kipato cha wastani tu kinachotokana na juhudi za kujihusisha na hiki na kile kwa kupitia kujiajiri.

Mke wangu pia ni mchakarikaji na anaitumikia biashara ya vyombo vya ndani na mapambo ya ndani ambayo kwa pamoja tuliifungua na inafanya vizuri sana.

Tumejaaliwa kuwa na gari moja Suzuki modeli mpya ambayo kiukweli aliinunua yeye mwaka Jana January. Kwasasa mimi ni fundi wa mashine za aina mbalimbali ikiwemo majenereta, magreda, kreni n.k. Na kwa kuwa mishe zangu za kiufundi hazihusishi sana matumizi ya gari ya kutembelea kwahyo huwa naitumia mara chache sana.

Baada ya kumfundisha mke wangu kuendesha akawa nayo kuanzia hapo. Mie Nina pikipiki ambayo hunipeleka huku na kule na kunifanikishia mishughukiko yangu yote bila tashwishi. Ninapohitaji gari kwa ajili ya matumizi ya hapa na pale au ninapoonyesha dalili ya kwamba nitatumia gari siku hiyo, papo hapo mke wangu huanza kujiskia karaha na ataanza kuongea maneno ambayo yanatoa ishara kwamba hataki nitumie gari.

Ukweli sipendezwi na hali hiyo maana inaudhi sana. Kwakuwa nimeshamjulia huwa nampuuza afu nachukua gari naenda kwenye kusudi nililolenga lkn furaha yake hutoweka kwa siku hiyo na hukereka kiukweli. Ingawa mie ndo niliyemfundisha kuendesha lkn pia haniamini napoendesha gari na hapendi nimuendeshe na kila wakati anasikika akinikosoa ninapoendesha, yani huwa dereva namba moja wakati aliyeshika usukani ni mimi.

Na kwa vile ameshajua pia nampuuza katika hilo, mara nyingi mke wangu huamua kukaa siti ya nyuma kwa vile haamini udereva wangu na huona kama nitamsababishia ajali akikaa mbele.

Kwa ufupi hapendezwi ninvyoendesha gari na hili jambo linanikera sana.

NAOMBENI USHAURI WENU WA KUNIJENGA KATIKA HILI.
 
Pole kijana ila maisha ndo yalivyo.

Wewe ulimfundisha kuendesha gari hukuchangia kununua gari kwahiyo uwe mpole mpaka utakaponunua gari lako hapo mtakuwa salama.

Kuhusu kumpuuza huwezi kujua anakwazika kiasi gani na hajali haina kinga ipo siku utachukua gari akiwa hataki utalibamiza na huo ndio utakuwa mwisho wa ndoa yenu.

Je wakati anajiandaa kununua ulishirikishwa hatua zote?

Je una uhakika pesa alonunulia gari zilitokana na biashara yenu?

Ukinijibu nitaendelea kukushauri.
 
Pole Sana Kaka. Pole Sana kwa mkeo kuwa KERO. Wanawake wenzangu tubadilike jamani. Mume wangu siku anataka kutumia gari.... Namuomba mapema kabisa anipeleke usafiri wa bajaji unapopatikana..... naendelea na ratiba zangu kama kawaida. Nikimaliza narudi nyumbani.... Raha mustarehe... Mapenzi Mubashara😂😅.

Mapenzi yana Raha Sana Wanawake wenzangu ... Haya Mambo madogo madogo haya tujifunze kuya-ignore. Tujifunze kujishusha kwenye baadhi ya mambo ambayo tunaweza kufanya na hayasumbui sana.... Kwani utapungukiwa nini? .... Pia Tunapunguza mikwaruzano inayoweza kuepukika. Gari zipo tuu. Cha muhimu Penzi na Raha ya MUME.
 
Nimejikuta nawachukia sana watu wanaotoa siri za wapenzi wao hadharani, hivi unadhani nani anajali? inatusaidia nini>? Jifunze kumheshimu mke au mume wako, social media kamwe haiwezi kukusaidia matatizo yako zaidi utaishia kupata majanga zaidi
 
Mimi ni mwanaume wa kawaida, nimejaaliwa kipato cha wastani tu kinachotokana na juhudi za kujihusisha na hiki na kile kwa kupitia kujiajiri. Mke wangu pia ni mchakarikaji na anaitumikia biashara ya vyombo vya ndani na mapambo ya ndani ambayo kwa pamoja tuliifungua na inafanya vzr sana. Tumejaaliwa kuwa na gari moja Suzuki modeli mpya ambayo kiukweli aliinunua yeye mwaka Jana January. Kwasasa mimi ni fundi wa mashine za aina

Pole mkuu..hilo gari sio lake..yeye ni kivuli tu cha alionalo,atakua kuna mtu aliweka fungu lake kubwa ili amfanikishie anunue hilo gari ndo maana anaona jau ukiwa unataka kuliendesha usijepishana na mwenye nalo..yeye kukaa nyuma anahifia mkionwa pamoja..maana ukionwa wewe pekeako anaweza sema wewe ni mfanyakazi wao alikutuma..

Kama si hivyo nnavyofikiria tofauti na hapo huyo mwanamke ana roho ya uchoyo sana..


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anzisha ligi kila akitaka kwenda na gali ukasilike hadi aliuze ndoa yenu ibaki na amani
Mimi ni mwanaume wa kawaida, nimejaaliwa kipato cha wastani tu kinachotokana na juhudi za kujihusisha na hiki na kile kwa kupitia kujiajiri. Mke wangu pia ni mchakarikaji na anaitumikia biashara ya vyombo vya ndani na mapambo ya ndani ambayo kwa pamoja tuliifungua na inafanya vzr sana. Tumejaaliwa kuwa na gari moja Suzuki modeli mpya ambayo kiukweli aliinunua yeye mwaka Jana January. Kwasasa mimi ni fundi wa mashine za aina mbalimbali ikiwemo majenereta, magreda, kreni n.k. Na kwa kuwa mishe zangu za kiufundi hazihusishi sana matumizi ya gari ya kutembelea kwahyo
 
Pole kijana ila maisha ndo yalivyo.
Wewe ulimfundisha kuendesha gari hukuchangia kununua gari kwahiyo uwe mpole mpaka utakaponunua gari lako apo mtakuwa salama.
Kuhusu kumpuuza huwezi kujua anakwazika kiasi gani na hajari haina kinga ipo siku utachukua gari akiwa hataki utalibamiza na uo ndio utakuwa mwisho wa ndoa yenu.
Je wakati anajiandaa kununua ulishirikishwa hatua zote?
Je una uhakika pesa alonunulia gari zilitokana na biashara yenu?
Ukinijibu nitaendelea kukushauri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wangu, kila hatua alinihusisha na ninataka nikuhakikishie kwamba pesa za manunuzi zilitokana na biashara na hiyo biashara ni yetu. Naiita ni yetu kwa mantiki mimi ndiye mtoa mtaji kwa 100% na nikamkabidhi kama ajira yake lkn kitega uchumi cha familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Achana na Gari yake, ww fanya safar zako bila gari yake ila hakikisha ukirudi sifia Demu aliekupa lift kuwa ana roho ya huruma na ubinadam sana.

Wakati mwingine mwambie kuna rafiki ako wa kike atakuazima gar yake ili yeye asikose kitoka na gari yake
 
Nimejikuta nawachukia sana watu wanaotoa siri za wapenzi wao hadharani, hivi unadhani nani anajali? inatusaidia nini>? Jifunze kumheshimu mke au mume wako, social media kamwe haiwezi kukusaidia matatizo yako zaidi utaishia kupata majanga zaidi
mkuu kunywa maji relax, ingekuw wote tuwe na usiri na mambo yawe ya ndan au ya nje sidhan kama ungepata hata thread ya kufungua usome. hata jf isingedumu. NOT EVERYTHING IS FOR EVERYONE. kitu kama hakikuvutii unaskip tu unaendelea na mambo mengne

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom