Mke wangu hana nidhamu?

Mweeeeeeeee! Hata mie nimechoka kabisa kuhusu kumkaribisha mtu maji ya kuoga! Labda hilo la chakula naweza kuelewa lakini kuoga? Yaani maji yanatoka bafuni nikukaribishe kuoga? Ha ha haaaaaa! Mila nazo sometimes zinatuponza!

Choka tu, kuna wenzako watakusaidia halafu uje na mada hapa ya mumeo anatoka nje. Mlidhani ndoa ni part time business, eti?

Na msijikengeue, suala linaloonekana hapa si kuyabeba maji bali ukaribu na mawasiliano. Mwanamke lazima ajue nafasi yake katika ndoa. Baadhi yenu hamjui hata mume aliondoka saa ngapi asubuhi
 
Mweeeeeeeee! Hata mie nimechoka kabisa kuhusu kumkaribisha mtu maji ya kuoga! Labda hilo la chakula naweza kuelewa lakini kuoga? Yaani maji yanatoka bafuni nikukaribishe kuoga? Ha ha haaaaaa! Mila nazo sometimes zinatuponza!
tatizo nyie mnavoishi mnadhani wote ndivo tunavoishi...wengie hatuna mabomba huko bafuni. maji yanachotwa kwa jirni ndo yanaingizwa bafuni..kwa nini nisiambiwe hata lugha tamu ya karbu mme wangu maji yako tayari bafuni?
 
sawa kabisa ila kosa lake kwa nini asimwambie kuhusu tabia yake na je naye akiwa na kasoro kidogo mke naye atafute wa kando? mawasiliano ni muhumu sana katika ndoa

Ukimsoma mleta mada vizuri,utaona huwa anamwambia mke wake kukerwa na hiyo tabia.Hapo kwenye red mkuu,yeyote kwenye ndoa anaweza kuingia kwenye vishawishi na kusaliti ndoa yake kwa kusababishwa na mwenza wake.Ndiyo maana nimeongelea sababu mojawapo ikiwa mawasiliano ambayo hata wewe umekubaliana nayo.
 
nakuunga mikono,miguu na kichwa mamii.
 
Hahaha! Nimechekaje! Wanaume bwana. Zee zima mwaka 2013 anataka abembelezwe kuuosha mwili wake mwenyewe. Ana bahati hadi maji anatengewa!
Snipper inabidi uinvest nguvu zako kuweka mabomba ndani ya nyumba kuliko ku overanalyze mke wako. Kazi nyingi za nyumbani mpaka kubembeleza zee zima, that's too much. Wewe ulishawahi kumwekea maji bafuni na kumbembeleza aje kuoga? Au ni jukumu la upande mmoja? Ndoa ni ya watu wawili baba. Ongoza kwa mifano.

wanaume bwana mnaboajeeee
utajijuuuu and u wil keri uaself we huwezi kuweka??kama ameshindwa kukwambia jiambie mwenyewe kimoyomoyo
 
Last edited by a moderator:
hana matawi yoyote..yaani kama ni kuwa juu mi ndo niko juu kwa kila kitu sema tu ni mambo ya kuoana ambayo huwezi kumwambia mwenzako ulikomtoa maana atajihisi kuwa unamnyanyasa ukimkumbusha ya nyuma!
Kweli mzee, hawa wanawake tunaowaokota barabarani ni pasua kichwa
 
hapo wanamama ndo huwa mnakosea....wewe unaujua uchumi wake<?? au unafikiri what u can do can be done by everyone? we mdada vipi...?

Pole, jaribu kuongea nae tena kama haelewi atakuja juta ukipata wakukukaribisha
 
hapo wanamama ndo huwa mnakosea....wewe unaujua uchumi wake<?? au unafikiri what u can do can be done by everyone? we mdada vipi...?

yaani kwa kweli hata mimi nawashangaa wanawake...nilishasema naishi nyumba ya kupanga na bafu ni la ne na maji lazima uyachote kwa jirani ujaze ndoo then ndio uweke bafuni..halafu naambiwa niweke shower! hivi humu JF kwani wote ni mambo safi?
 
wanaume bwana mnaboajeeee
utajijuuuu and u wil keri uaself we huwezi kuweka??kama ameshindwa kukwambia jiambie mwenyewe kimoyomoyo

kwa nilivyomuelewa mimi,ishu sio kuweka maji,ishu ni kukaribishwa!ule ukarimu wa kukaribishwa umekosekana,na ndio upendo wenyewe!haya endelea kutoa maoni yako Amu baada ya kukudadavulia.

n.b snipper,kama nimekosea ufafanuzi nirekebishe tafadhali
 
Hiyo haina habari ya makabila ni tabia tuu ya mtu!
 
hapo wanamama ndo huwa mnakosea....wewe unaujua uchumi wake<?? au unafikiri what u can do can be done by everyone? we mdada vipi...?

hivi mkuu umsoma vzr post yangu??

mm nimempa option mbili na nikaaanza na ile ambayo inawezekana kwa kila mtu, je kutoa alternative nyingine ni mbaya??
hata kwenye EIA project alternative inaruhusiwa so kama wewe huelewi uulize na sio kuzodoa as if umepata
 
Pole kwa jinsi umejisikia,kwanza mkeo ana adabu ndo maana hata anakuwekea maji bafuni,,labda useme mke wako hayuko sweet ila unaweza ukamfanyia vile unataka ufanyiwe nae atajifunza taratibu,kikubwa usikate tamaa
 
Wakinisaidia si itakuwa ujinga wake mwenyewe? Wala hutakaa unisome humu nalalamika kuhusu hilo. Humu hakuna wa kunifundisha kuhusu ndoa.
 
tatizo nyie mnavoishi mnadhani wote ndivo tunavoishi...wengie hatuna mabomba huko bafuni. maji yanachotwa kwa jirni ndo yanaingizwa bafuni..kwa nini nisiambiwe hata lugha tamu ya karbu mme wangu maji yako tayari bafuni?

Endapo unatumia lugha nzuri na ya upendo kwangu kwanini nami nisirudishe huo upendo/lugha nzuri? Tatizo baadhi ya wanaume wanadhani ni wao tu ndio wanaostahili kupendwa na kubembelezwa. Tenda kwa mapenzi uone kama hutotendewa kwa mapenzi na hata zaidi. Watu wamabakia kukimbilia mila. These are diffent times!
 
mtafutie makungwi wamfundishe
 
Alifanyiwa kitchen party huyo sasa inabidi umrudishe kwao wamfanyie UNYAGO, ataelimika na kuing'arisha ndoa yenu. Mbona utabebwa juu juu hadi bafuni kwi kwi kwi kwiiii

Sent from Samsung tablet
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…