Mke wangu hampendi mama yangu mzazi

Lakini ukweli ni kwamba.....
Hakuna mwanamke ambae anapenda kukoseshwa uhuru wa ndani mwake na mwanamke mwenzie haijalishi huyo mwanamke ni nani.
Lakini pia mkeo ni mwanamke mpumbavu mkuu, hapo unashughuli pevu mbeleni.
Na mwisho, mkeo ana tabia mbaya sana kuyatoa maneno ama mambo ya ndani kwenu nje ya nyumba yenu.
Minaona huyo mke mnawe, lakini nawewe fanya namna upate maarifa ya mama yako akaishi maisha tofauti na kwako.
Mama sikai nae tuko mbali mbali mji mmoja
 
Ndio sijakata ndio maana nimesema kwasababu kila mtu anataka utawala mwingine juu ya mtoto wake mwingine juu ya mume wake.
Hili bifu ni natural hata kwenye maandiko lipo..... Nadhani ni wivu kila mtu anauhitaji upendo wa mwanaume na kila mtu anaona ana haki 100%
Msiumize vichwa wala
 
Sometimes sijui ni fikra za kimaskini au ni nini. Sijui kilichopita baina ya hao wawili, na simtetei dada hapo, lakin familia za kiAfrica zina kash kash sana. Kuna muda mtu unajaribu kuwa vizuri tu lakin unaishia kuwa slapped in the face na kudhihakiwa. Kuna wanawake walishajitahidi kuwa wema ukweni lakin bado mambo yakaback fire. Sasa huwa nahisi ni fikra za kimaskini tu. Kuna msemo unasema strong people dont revenge rather do ignore. Naamin mkeo akianza kujishughulisha na ya kwenu meaning wewe, watoto na yeye mwenyewe basi hizi kasumba zitaisha.

Ningepewa nafasi ya kumshaur binti leo ningemwambia "unapoingia kwenye familia za watu cheza kwa step. Kuwa na kiasi, usisomeke...hii ni ili kuilinda afya yako ya akili. Usijifanye mjuaji sana, msomi sana, mmbea sana. Wakikaa kujadili yao katafute hata kuni huko porini. Kamwe usimseme yeyote ukishirikiana nao, kitakuramb hutaamin. Usiwe mzigo ukweni, usiwe kihongwe vilevile. Masuala ya umbea na mama wakwe, mawifi koma!!! Fanya kazi kwa bidii, ukipata chochote na kwa upendo mtumie mama mkwe mara moja moja kiroho safi. Zaidi sana jifunze kuongea na Mungu juu ya hiyo familia. Ukiwa busy na mambo yako hakuna atakae kujua wala kukuzoea na kutakuwa na mipaka so sio rahisi wao kuingia anga zako na wewe kuingia anga zao".

Migogoro mingi sana inaletwa na ufahamu mdogo wa the female gender. Lakin pia kuna namna tunakoseaga pale ambapo tunaruhusu third parties kwenye familia zetu. Mungu hakukosea alivyosema Ndoa na iheshimiwe na watu wote na na malazi yawe safi meaning kila mtu ana wajibu wa kuiheshimu including walioko ndani. Sawa sometimes sisi vifua vimetujaa tunataman kucheua ili tupone basi nenda kwa asiyewafahamu ili awashaur akiwa neutral zone. Anyways hizi changamoto naamin kabisa zinatatulika kwa msaada wa Mungu. May God give you wisdom....
 
Sasa mkuu ww mzazi wako akashfiwe labda mfano tu labda mzazi wako aambiwe linasumbua sumbua hili libibi linaroho mbaya nalicheck tu nasura yake pasono linajiskia...unampa mtu huyo nafasi ipi yakumsikiliza
Kwa kuuliza anasumbuliwa vipi na kwa nini anasema libibi lina roho mbaya. Lazima kuna sababu. Ni kwa kumsikiliza tu ndio utajua tatizo wapi. Kama tatizo liko kwake atakuheshimu kwa kumsikiliza na kumtendea haki. Kama wazazi wako ndio wenye matatizo, atakuheshimu kwa vile atajua kuwa unamjali. Kwa namna hii, badala ya kukimbilia kwa mashoga na ndugu zake tatizo likitokea, atakuja kwako kwa sababu atajua kuwa wewe ni mtu wa haki.

Amandla...
 
Mtu anayependa kuongea pembeni tafasiri yake ni kuwa ana mambo anayotaka kusema ila hajapata masikio ya kumsikiliza katika nyumba yake. Na jambo lingine inaonekana mkeo hajakuamini kiasi kwamba anapata shida kukwambia yale yanayomsibu.

Mama yako ni binadamu pia huenda ana mapungufu yake ambayo mkeo ameyaona na ametaka kuyajadili na wewe ila sababu ya namna utapokea vibaya ameona akae kimya ila amekwenda kuongelea nje.

Keti chini na mkeo tena sehemu ya faragha sana halafu mbembeleze akwambie yanayomsibu. Mkeo ni nusu yako ya pili, hutakiwi kuiacha itetereke huku wewe ukiwa upo comfortable tu.
 
Naam mu hali gani ndugu watazamaji naona humu kumeanza kuchangamka tupo livee bila chenga tunakwenda kumuhoji mke wa mleta mada nikuubie tu siri mke wa mleta mada ni mchawi ninakwenda kumuhoji na akileta ushenzi namlatua makofi livee bila chenga!
 
Back
Top Bottom