Mke wangu hampendi mama yangu mzazi

Mke wangu hampendi mama yangu mzazi

Mkumbushe kuwa, mama mzazi ndie aliyekuleta duniani ndipo ukamuoa huyo mwanamke. Kama anamdharau mama yako ujue wewe anakudharau mara mbili. Mfanyie kikao ikishindikana ni "talaka ".
 
Ukitaka kujua familia ulioijenga ni imara kiasi gani mlete mama yako mzazi akae hata mwaka nyumbani.kwako!

Utaona mambo ambayo utafanyiwa ukiwa mnyonge huna ujanja akifanyiwa mama Yako mzazi!yaani kile atakachokufanyia wewe ukiwa mdhaifu na huna namna ndicho atamfanyia mama Yako hapo kwako ili aondoke!!
Ukiona hayo tambua ulifeli kutengeneza familia yako!!
 
Kata mawasiliano yao baina ya mama yako na mke wako ikitokea sherehe asiende wala kusalimia aanasana wasalimiane kwa simu siku mojamoja.
Kama waru hawaendani yanini kuwaweka karibu mtawazidishia uhasama.
Ntakataje nna watoto nae nawazazi wangu wanawapenda wakuu zao
 
Habar wakuu, mimi ni baba wa watoto wa 3, niko 35 mke 31, hapo awali miaka 4 nyuma wazazi walikua wakinambia tabia za mke ambazo ni za maneno na umbeya yaani anazungumza mambo yanayohusu wazazi wangu ndugu zake na mashost zake anazungumza maneno mabaya.

Sasa watu huhadithiana yanafika nikimuuliza anakataa. Inabidi nazungumza na namuelimisha namna maisha yalivyo.

Sasa bana kumbe tabia haikukoma, kumbe amekua akichat na ndugu zake hasa dada yake, chats za kusema wazazi wangu.

Mke wangu alishawahi kosea sms ikaja kwangu kama mara mbili sikusema chochote.

Majuzi asubuhi asubuhi nimekaa zangu kabla sijatoka home alikua anachat tu na sms zinaingia naskia anavochati

Kumbe anachat na dada yake bahati nzuri akakosea kusend sms moja ikaja kwangu akimhadithia dada yake jinsi mambo mabaya kuhusu mama yangu yaani hampendi.

Nawaza naona kama nimke ambae hanifai, alishawahi kuwekwa kikao kwa mambo haya lakini naona kama habadiliki uswahili roho mbaya vimemjaa.

Sasa mke alivyomnafiki ukimkuta na mzazi wangu wakike anavyoact kama kweli vile anamkubali.

Wakuu ushauri wenu.
Mkuu hiyo kuibadilisha ni ngumu sana. Dada yake ndie chanzo. Angekua anawatakia mema kwenye ndoa yenu angempiga stop mdogo wake na angemshauri yaliyomema.
Hakika hakika nakwambia, jiandalie makazi yako binafsi ambayo mkeo hata yajua wala ndugu zake wala watoto wenu. Kwani naamini kwa tabia yake hatataka hata watoto wako wakamtembelee bibi yao. Na wewe hutavumilia tena, utamwacha lakini utakua tayar unamakazi yako ambayo mama yako atakua huru
 
Lakini ukweli ni kwamba.....
Hakuna mwanamke ambae anapenda kukoseshwa uhuru wa ndani mwake na mwanamke mwenzie haijalishi huyo mwanamke ni nani.
Lakini pia mkeo ni mwanamke mpumbavu mkuu, hapo unashughuli pevu mbeleni.
Na mwisho, mkeo ana tabia mbaya sana kuyatoa maneno ama mambo ya ndani kwenu nje ya nyumba yenu.
Minaona huyo mke mnawe, lakini nawewe fanya namna upate maarifa ya mama yako akaishi maisha tofauti na kwako.
 
Kabla hujamweka ndani kwani ulikuwa hujui mapungufu yake,?

mna watoto wa 3 sasa hvi ndiyo umesha ona mapungufu yake...

Mvumilie mmalize ungwe ya mda mchache mliyo bakiza hapa duniani mlee watoto hao
Mda chache waliobakiza!
Wakiishi umri wa Ally Hassan Mwinyi utawakataza?
 
Mke wangu alishawahi kosea sms ikaja kwangu kama mara mbili sikusema chochote.

Majuzi asubuhi asubuhi nimekaa zangu kabla sijatoka home alikua anachat tu na sms zinaingia naskia anavochati

Kumbe anachat na dada yake bahati nzuri akakosea kusend sms moja ikaja kwangu akimhadithia dada yake jinsi mambo mabaya kuhusu mama yangu yaani hampendi.

Hajakosea, itakuwa amesave namba yako kwa jina la dada yake...
 
M
Lakini ukweli ni kwamba.....
Hakuna mwanamke ambae anapenda kukoseshwa uhuru wa ndani mwake na mwanamke mwenzie haijalishi huyo mwanamke ni nani.
Lakini pia mkeo ni mwanamke mpumbavu mkuu, hapo unashughuli pevu mbeleni.
Na mwisho, mkeo ana tabia mbaya sana kuyatoa maneno ama mambo ya ndani kwenu nje ya nyumba yenu.
Minaona huyo mke mnawe, lakini nawewe fanya namna upate maarifa ya mama yako akaishi maisha tofauti na kwako.
Mkuu hilo la kumnawa umebonyeza sana!

Kwenye mashauri ya ndoa ni mwiko kushauri hivyo.

Tushakuwa wazee, hata wakiletana na ukagundua jamaa kachapiwa, huwaga tunauma na kupulizia ila 'final solution' tunamwachia yeye ni kama riwaya, hadithi hautakiwi kuifikisha mwisho.

Kwenye issue hizi, kuna wanaume wananyanyasika sana, analalamika na mnaona kabisa madhaifu ya mke, ila wanakuja kutuangusha wakijifungia kupeana chakula cha usiku, ni aibu!

Mtu utadhani ni mgeni na hayo mambo ama kijana wa balekhe, unakuta anaungama wazi wazi na kukutaja jina lako halisi uliyeshauri waachane, yote hayo ya nini?

Piga ushauri, kunyoa au kusuka mwachie mwenyewe.
 
Habar wakuu, mimi ni baba wa watoto wa 3, niko 35 mke 31, hapo awali miaka 4 nyuma wazazi walikua wakinambia tabia za mke ambazo ni za maneno na umbeya yaani anazungumza mambo yanayohusu wazazi wangu ndugu zake na mashost zake anazungumza maneno mabaya.

Sasa watu huhadithiana yanafika nikimuuliza anakataa. Inabidi nazungumza na namuelimisha namna maisha yalivyo.

Sasa bana kumbe tabia haikukoma, kumbe amekua akichat na ndugu zake hasa dada yake, chats za kusema wazazi wangu.

Mke wangu alishawahi kosea sms ikaja kwangu kama mara mbili sikusema chochote.

Majuzi asubuhi asubuhi nimekaa zangu kabla sijatoka home alikua anachat tu na sms zinaingia naskia anavochati

Kumbe anachat na dada yake bahati nzuri akakosea kusend sms moja ikaja kwangu akimhadithia dada yake jinsi mambo mabaya kuhusu mama yangu yaani hampendi.

Nawaza naona kama nimke ambae hanifai, alishawahi kuwekwa kikao kwa mambo haya lakini naona kama habadiliki uswahili roho mbaya vimemjaa.

Sasa mke alivyomnafiki ukimkuta na mzazi wangu wakike anavyoact kama kweli vile anamkubali.

Wakuu ushauri wenu.
Ni kawaida 90% ya wanawake hawawapendi mzazi wa kike wa mwanaume kwasababu kila mtu anataka utawala ndio maana mzazi wa kiume anaweza akakaa mda mrefu kwa mwanawe ila mzazi wa kike hata mwezi hatoboi.
 
Tatizo ni kuwa hautaki kuangalia kama anachosema kuhusu wazazi wako kina ukweli. Msikilize vizuri na kama kuna ukweli tajuta njia ya kuwaambia wazazi wako ili wabadilike au mwambie avumilie tu kwa sababu hauwezi kuwabadilisha wazazi wako. Anaongea nje kwa sababu anajua hautamsikiliza. Wazazi sio malaika.

Amandla...
Sasa mkuu ww mzazi wako akashfiwe labda mfano tu labda mzazi wako aambiwe linasumbua sumbua hili libibi linaroho mbaya nalicheck tu nasura yake pasono linajiskia...unampa mtu huyo nafasi ipi yakumsikiliza
 
Kuna mstari mwembamba sana Kati ya ww na mke wako ww umeleta yake humu ila yy kachukua ya mazaako kapeleka kwa dadaake!

Ondoka kwenye hyo zone mmekusanyana wote ndugu zako na ndugu wa mkeo mtaishia kusemana tu
asipoelewa hapa basi tena, alafu wote ndio wale wale yeye kaleta JF mkewe kupeleka kwa dada ake😀😀😀.... mara nyingine analeta habari za biashara zake, mara mke mjamzito, mara mkekajifungua, mara kaishiwa damu, leo kaja msema mkewe huku ni kama mwamba flani hivi asie na maamuzi na anasumbuliwa sana na upweke nahisi ama kutokujiamini yani nyuzi zake woiiiiiiiiiiiii....... ana issues nyingiiiiiiiiiiiii
 
Sasa mkuu ww mzazi wako akashfiwe labda mfano tu labda mzazi wako aambiwe linasumbua sumbua hili libibi linaroho mbaya nalicheck tu nasura yake pasono linajiskia...unampa mtu huyo nafasi ipi yakumsikiliza
Acha kufatilia mambo ya kike mkuu we mwanaume ujue aahhhh!!
 
asipoelewa hapa basi tena, alafu wote ndio wale wale yeye kaleta JF mkewe kupeleka kwa dada ake😀😀😀.... mara nyingine analeta habari za biashara zake, mara mke mjamzito, mara mkekajifungua, mara kaishiwa damu, leo kaja msema mkewe huku ni kama mwamba flani hivi asie na maamuzi na anasumbuliwa sana na upweke nahisi ama kutokujiamini yani nyuzi zake woiiiiiiiiiiiii....... ana issues nyingiiiiiiiiiiiii
Atakua amenielewa vzr
 
Back
Top Bottom