Mke wangu haachi pesa ya matumizi

Mke wangu haachi pesa ya matumizi

kwanza pole(kumbe ndio maana unaandika unakosea, kumbe sababu ni njaa. Kweli njaa mwana malegezya), ila haya ndio madhara ya kuishi pasipo kuandaa future yako, wafanyakazi wengi hamjui nini cha kufanya ili baadae ikitokea kazi kuota mbawa mpate pa kujishikiza.. Ndg nahisi utakuwa na nguvu za kutosha sasa fanya kuni-PM ili nikupe msaada wa troll la kuchotea maji maana ni kheri kujishughulisha kuliko kushinda njaa na huyo mwanamke atakuja kukutoa roho kama ukikubali kula chakula alichokupikia.. Nasisitiza ktk hili troll lang stakutoza hata100 ktk kpnd cha mwanzo, ni imara na pia madumu ya kutekea maji yapo.. karibu mkuru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaonekana Bado ni mvulana, wanaume hatuombi ushauri tunafanya maamuzi tuu
 
Naileweke: nikweli kwamba juzi niliandika uzi apa kwamba Mke wa kaka hataki kunifulia, naomba niwaweke sawa wanajamvi,
Kulingana na Hari niliyonayo sasa nimekua Mtu wakushinda nyumbani,
Juzi asubuhi nikiwa nimekaa nje hapa nyumbani Kaja kijana kiumri ni mdogo wangu lakini tumezoea kukaa pamoja na kupeana mawaiza mawili matatu kwan na yeye Hana shughuri yeyote anayofanya anaishi kwa kaka yake.
Ivo Muda mwingi tunakua pamoja, ivo juzi Kaja kuniambia shemeji yake hataki kumfulia!
Binafsi nilishangazwa Kama nyote mlivyoshangazwa, nilimuuliza Kwani huwa anakufulia? Akanijibu ndio, ndio shemeji yake huwa anafuwa nguo zoote Kwani pale Wapo watatu tu yeye, kak yake na Uyo shemeji yake, anasema baada ya kaka yake kuondoka (kasafiri takribani karibu wiki sasa) shemeji yake hamfurii tena..
Nikaona jambo ilo ni LA kustahajabisha Sana.
Japo nilimshauri aanze kujifuria ila Nikaona bora niweze kushare na nyinyi wanajamvi, ili muweze kujua kwamba Kuna familia zingine zinamambo ya ajabu ambayo kwa watu wengine unaweza kuona ni km hadithi,.
Naomba ieleweke ivyo,
Ili nililoliandika Leo ni la kwangu Sio story ya kutungunga, yeyote mwenye mashaka namkaribisha nyumbani apa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mke? Hawara? Ktk maelezo yako sijaona sehemu umeandika mlifunga ndoa huyo ni msela wako na ameshakua msela mavi cha kufanya, we hama hapo ukaanze maisha upya...sijui huko shuleni huwa mnapewa elimu gani hizi siku....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkeo yuko sawa kukunyima pesa ili akili ikukae sawa,huwezi kulia lia hapa wakati una akili na viungo vyote vya mwili,nenda kamsaidie fundi kupandisha tofali upate pesa ya kula,sio unashinda unabofyabofya tu hicho kilaptop chako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua kwann walitwa JINA LA HAWA sio watu hao ni majambazi HAWA ni washenzi HAWA mwana roho mbaya HAWA sio wa kuwaaamini hata dakika 1 HAWA tuishi nao kwa akili HAWA sio ndugu zako huwa simuamini mwanamke kwa njia yoyote ile HAWA sio damu yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mwaka wa Pili sasa tupo kwenye ndoa, nimejuananae toka tupo chuo mwaka wa kwanza.
Tuliishi pamoja ghetto hadi tunamaliza chuo, ivo namfamu vizuri Mke wangu na yeye ananifamu vizuri.

Mara baada ya kumaliza chuo nilibahatika kupata kazi kwenye kampuni moja ivi ya wachina, baada ya kufanya kazi kwa miezi kadhaa nikaona bora nimuite Mke wangu tuje tuishi Wote Kwani Wakati huo nilikua nimejitisheleza.
Wakati huo Mke wangu alikua Hana ili wala lile japo alishafanya interview nyingi tu lakini bado hakubahatika kupata kazi, kwa kipindi chote hiko Mimi nafanya kazi nilikua namtia moyo, kipindi chote hiko nafanya kazi hajawai kulala na njaa wala fashion yeyote kumpita.

Baada ya kukaa nyumbani takribani mwaka mzima bila kazi, Nakumbuka 11th mwezi 3 alifanikiwa kupata kazi kwenye taasisi moja ivi, Kwakweli turifurahi Sana hiyo siku, turimshukuru mungu kwa tusimamia na kupata kazi sote,.

Maisha yalienda tukiwa na furaha japo Kuna vitu vilinitatiza, japo Mke wangu anapokea mshaara Mkubwa Mara mbili yangu ila majukumu Yote ya kifamilia nilikua nayatekeleza Mimi, pesa yake sijui alikua anapereka wp Yaani hata gari anayotumia yeye Mimi ndie nilikua namjazia mafuta.

Kisanga kilianza baada ya mkataba wangu na wale wachina Kuisha, mwanzo mambo yalikua mepesi Mke wangu alinishauri na kunitia moyo, alikua anarudi kazini mapema japo kuna kazi nilikua nimeshazifanya km kufua, usafi wa nyumba n. K akirudi yeye kabla hata hajapumzika hunipikia chakula cha Jioni, asubuhi kabla hajaondoka huwa ananiachia kiasi cha pesa ya matumizi,,

Toka ile kazi imeisha yapata miezi minne sasa, nieleweke Sio kwamba kipindi chote hiki nimekaa tu nyumbani, nimehangaika na vyeti ofisi mbalimbali kutafuta kazi, Muda mwingi nipo na laptop yangu nafanya interviews online, kokote nikisikia Kuna nafasi za kazi mm huwa wa kwanza.

Shida kwa Mke zilianza takribani mwezi sasa, kidogo kidogo nikaanza kuona mabdiliko, akawa anachelewa kurudi, akirudi hanipikii anadai amechoka ivo ananipa pesa nikale mghawani na yeye anadai hajisikii kula, ila asubuhi lazma aache ela ya matumizi kwasababu anajua Sina ujanja wa kupata pesa.

Tumeenda ivyo mpaka majuzi Hari imeanza kuwa mbaya, akirudi hapiki wala hanipi pesa ya kwenda kula mghawani, mbaya zaidi asubuhi anaondoka aachi chochote,
Tena Jioni akirudi Hana hata Muda wa kunitazama yeye anaoga na kulala, Hataki hata kujua nimekula nini.

Naandika ivi toka Jana sijala, nyumbani Siwezi kupiga simu kuwaomba pesa kwasababu wanajua Mke wangu anafanya kazi mzuri tu.

Hari yangu mbaya Kwakweli nisaidieni hata kwa mawazo nifanyeje kwa Hari Hii niliyonayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole kashakutana na wajanja wanakusaidia anarudi mwepesi kasha maliza shuguli huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hana mapenzi ya dhati kwako, hata kama ungekua unafanya kazi bado alihitajika kuchangia matumizi ya nyumbani

Wanawake ifike mahali tubadilike, hivi una mshahara unasubiri hadi mwanaume akuwekee mafuta ya gari unayoendesha

Kimsingi mimi nikipata mshahara huwa napitiliza moja kwa moja sokoni nahakikisha chakula cha mwezi mzima ndani kipo, diapers za mwezi mzima, maziwa ya watoto na mahitaji ya ndani kiujumla na Mume wangu ameshazoea kwamba mahitaji ya ndani huwa nafanya mimi halafu yeye anahangaika na ada za watoto na kama kuna jambo la ziada huwa tunakaa tunajadiliana na tu aweka nguvu pamoja

Kifupi sijawahi kumuomba Mume wangu hela ya matumizi, huwa anaacha pesa ya kutosha bila kuombwa na pamoja na kwamba kila kitu kipo ndani lakini anaacha pesa ya matumizi,

Maana ya maidha ya ndoa ni mnasaidiana sio kumbebesha mwenzio mzigo mzitoo unamzeehsa buree

Na hakuna maisha ya raha kama ya kusaidiana na kushirikiana katika majukumu, sio maisha magumu ni mepesi na mnafurahia,



Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba nikuvulie kofia kwa heshima, hakika wewe ni mke na unastahili kuwa mke wa mtu..

Umimi kwa baadhi ya wadada ndo umefanya ndoa nyingi zisiwe na furaha..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Write your reply.. kwa kipindi chote hicho unafanya kazi hukusave pesa bank halafu utamtegemeaje mwanamke bro ... mwanamke nae anakuletea ki base unaangalia tuu kweli ww chenga ...
 
Ukiweza kunipa namba ya mkeo PM,nitakusaidia kumfunda na nikimaliza naomba na namba yako nikwambie namna ya kuishi na mke.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom