Mke wangu askari Polisi bado anawasiliana na mzazi mwenzie ambae pia ni askari Polisi

Niliwahi kusikia katika wanawake hupaswi hata kujihusisha nao katika ndoa ni askari (iwe polisi au jeshi) sikupewa sababu ila baada ya utafiti wangu nikapata majibu wanatafunana sana
Ishu mezani ni single mama, kazi ya uaskari kama yupo single unaweza kufuata process ukapiga chini akatafuta kazi nyingine
 
Mwanamke akishakuwa na mtoto halafu umwambie huyu mtoto wako akakae kwa bibi yake ili kupunguza ukaribu na mzazi mwenza wa mke hapo ndio matatizo yatakapo anza.

Kwanza mwanamke atahisi wewe haumpendi mtoto wake ndio maana unaleta sababu hizo kumbuka kuwa hata kama wewe ungezaa naye huyo mtoto basi jua kuwa mapenzi ya mama yangehamia kwa mtoto wenu.

Hivyo sikushauri uruhusu mtoto aende kuishi na bibi cha msingi kama bado na wewe haujazaa na huyo mke wako ongeza mashambulizi ili nawe uzae naye ili kupunguza kumkumbuka sana huyo jamaa kwa sababu ndiye pekee aliyemuwezesha kwenda wodi ya uzazi.

Namalizia kwa kuandika kuwa usihofie cheo cha huyo polisi kwa sababu linapokuja jambo la mahusiano na mapenzi kila kiumbe kinakuwa dhaifu bila kujali ukomavu wake katika nafasi aliyo nayo.
 
Na wewe ni askari ama raia
Habari zenu wanajamvi wenzangu...
Nimeoa askari polisi miaka miwili iliyopita, japo nilimkuta mwenzangu akiwa na mtoto wa kiume..
Kutokana na maelezo yake Baba wa mtoto wake ni Police tena mwenye cheo kikubwa tu ..
Walishawai kuishi nae ila alimiacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine na kupelekea kuachana ..
Ila uko alipooa hakuwai kupata mtoto mwingine ..
Hivyo basi jamaa uyo amekuwa busy na kumfatilia mtoto kulipa ada na garama za mavazi ...
Sina wivu ila najaribu kutaka ushauri kwenu nyie wakubwa zangu mlionizidi kwa kila kitu kuhusu haya mahusiano ...
Vile vile sina tatizo na mke wangu..
Tunaheshimiana Tunapendana lakini mwisho wa siku nahitaji kupata ushauri wa tahadhari ili baadae yasinikute ...Naomba kuwasilisha ..
 
Askari,askari,kombati nini jesh,!
Nimekumbuka hako kawimbo wakati tukiwa depo kuleee! Kj 828,kwa askari hakuna kuachana,kama jamaa ni afisaa mkeo anaweza kukuambia anaingia shift kumbe wanaenda lala na jamaa mpaka monie,jamaa linapewa papuch mguu mpaka dirishani,
fikiri hii,kwa nini askari wengi hawapendi kuoa askari wenzao? Yanayofanyika huko,yajayo hayanogi.
Nimecheka kwa sauti
 
Kwa hiyo umeoa single mother?
Wakati mwingine vijana matatizo tunajitakia wenyewe. Wewe umejiunga familia ya mkeo, hujaanzisha familia yako. Hivi uliyafikiria haya kabla hujaoa? Yaani as if hukuyajua haya before.

Shauri yako mwenyewe.
 
Kabla ya kumuoa huyo mwanamke au kabla ya kufunga naye NDOA haukupata muda WA kutafakari kuhusiana NA suala hili unaloomba ushauri??? Unaambiwa fikiri kabla ya kutenda, wewe umefanya kinyume chake. Hivi ni KWA nini Wanaume wengi WA siku hizi wapo namna hii??

Suala LA kuoa au kuolewa ni jambo nyeti sana ktk maisha ya binadamu, hivyo basi, kabla ya MTU yeyote yule hajaamua kuingia kwenye NDOA ni lazima kwanza afanye upembuzi yakinifu wa kina kabisa ili kujiridhisha juu ya utayari wake. NDOA siyo jambo LA kukurupuka, hasa unapoamua kumuoa mwanamke ambaye tayari ana mtoto au watoto aliozaa NA mwanaume mwingine.

Kazi kwako, ,"UKILIKOROGA LAZIMA ULINYWE"

"Kalagabao NA ubwenzi wako !!"
Mkuu najarubu kutafakari ushauri wako ..
inamaana Mwanamke mwenye mtoto afai kuolewa tena...
Istoshe mke wangu huyu hajawai kuwa na ndoa na uyo Mzazi mwenza..
Swala la kuchunguza mpaka kufunga na ndoa halikuwa ni swala la siku moja ..
Vingi nilichunguza na nikajiridhisha ..
Wasiwasi wangu ni kwamba isifike mahali nikaanza kununua magunia ya mkaa ilhali sina jiko la mkaa ...!!
Uwo ndio wasi wasi wangu ..
Nikiamini kwamba kunawahenga wenzangu waliputia changamoto kama hizi na wakafanikiwa ...
 
"Kutokana na maelezo yake".

Kumbe ni maelezo ya Mkeo.

Kwanini na wewe usifanye Uchunguzi wako ili upate kujua anachosema Mkeo ni cha kweli, au si cha kweli.

Kwa KAULI yako hii "Kutokana na maelezo yake", inaonesha fika ya kuwa wewe mwenyewe nusu unakiamini anachokisema Mkeo, na nusu hukiamini.

Hapa kuna UTATA
Mkuu ukweli ni kwamba hakuna mtu mbea kama mke wangu...
Hata akinyonga mtu nahakika ataniambia tu ..
Hivyo basi sina shaka sana na alichoniambia ...
Alaf mimi sio mtu wakufatilia sana Mwanamke maana mwisho wa siku nitajiumiza
tu na kuacha kufanya mamho ya msingi ..
Furaha usipoitafuta mwenyewe mkuu basi ni nani huyo wakiitafutia ...
ukianza kuchunguza kiundani kila Mwanamke utaekutana nae basi naamini hata Mama angu mzazi asingeolewa na Baba angu ...
Sijui kama tunaenda sambamba mkuu..!!?
 
Mbea kama lusu??

Au humjui lusu??
 
Pole na hiyo changamoto, wanaume tumeumbiwa mateso na kuhangaika ila kuyapunguza ni juhudi zetu wenyewe.

Kuoa mwanamke aliyezalishwa na kuachwa wala sio kosa bali ni upendo wa dhati japo changamoto huwa ni masaibu na hao wazazi wenza kutaka kuyala matapishi yao sometimes.

Cha kufanya hapo na ni cha lazima na ilibidi ufanye mapema kabisa kabla hata ya ndoa: ni mtoto kupelekwa kwa baba yake, baba yake ataamua akae naye ampeleke kwa wazazi wake na kama inashindikana kabisa basi mkeo ampeleke kwa wazazi wake na mahitaji na mawasiliano yote yafanyike moja kwa moja kwa anayekaa na mtoto na sio kupitia kwa mama mtoto wala baba mtoto. Huwa wanapasha viporo na wanaweza kutaka kurudiana kutokana na uhitaji wa kuzaa tena mtoto/watoto na kuna uwezekano mkubwa ukadhurika hata uhai wako.

Usikae na mtoto wa mtu mwingine. Mimi nilizalia sehemu mke wangu alileta ushirikiano mzuri sana kuwa tuchukue mtoto amlee mwenyewe kama mtoto wake. So kwa namna nyingine alisaidia matumizi bora ya fedha na pia kuzuia mawasiliano yangu na huyo mzazi mwenzangu.
 
Kushirikiana simu sio hoja. Watu wanaandika na kufuta sms za mahabati. Jipange KUDUKUA uthibitishe.

Bazazi
Mkuu kabla ya kuingia kwenye Ndoa nilifundishwa Ndoa ni uvumilivu na kusameheana ...
Histoshe ndoa ya kikristo ni moja tu mpaka kufa ...
Sikatai ushauri wako wa kudukua mawasiliano ila nikishapata ninachokitaka alaf nifanyaje sasa...
mimi naona ukimchunguza bata sana hakika uwezi kumla so ivyo vitu vyakuaribu sipendelei sana kuvifatilia maana mwisho wa siku nitabomoa nyumba tu na istoshe hakuna Mwanamke asiyekuwa na kasoro...
 
Nimependa kitu kimoja tu kutoka kwako kaka mkubwa ni busara unazotumia kuuliza swali kama bado mama yake uyo mkeo yuko hai mwambie ampeleke mtoto akae kwa bibi yake au aende kwa uyo babake mkuu mbeleni watarudiana na itakukost sana mkuu
Noted
 
Mkuu kabla ya kuingia kwenye Ndoa nilifundishwa Ndoa ni uvumilivu na kusameheana ...
Histoshe ndoa ya kikristo ni moja tu mpaka kufa ...
Sikatai ushauri wako wa kudukua mawasiliano ila nikishapata ninachokitaka alaf nifanyaje sasa...
mimi naona ukimchunguza bata sana hakika uwezi kumla so ivyo vitu vyakuaribu sipendelei sana kuvifatilia maana mwisho wa siku nitabomoa nyumba tu na istoshe hakuna Mwanamke asiyekuwa na kasoro...
Ok
 
Kwa hiyo umeoa single mother?
Wakati mwingine vijana matatizo tunajitakia wenyewe. Wewe umejiunga familia ya mkeo, hujaanzisha familia yako. Hivi uliyafikiria haya kabla hujaoa? Yaani as if hukuyajua haya before.

Shauri yako mwenyewe.
Hahahaha aisee mkuu umepiga jiwe la maana,
Eti amejiunga na familia ya mkewe
 
Mnaambiwa msioe single mother bado mnajifanya mnaongozwa na mihemko na hisia pambana na Hali yako

Hivi mkuu wanawake waliishaga au?
Mkuu wangu asante kwa Ushauri ila bado siamini kuoa mwanamke mwenye mtoto kama ni dhambi...
Kwa sisi ambao tumepevuka kiakili sidhani kama naweza kusumbuana na vitoto vya kidacho cha 4 ...
Mimi niliangalia mwanamke ambae tutaelekezana tutakatazana na kuambiana ukweli...
Mwanamke ambae anajua Mume ni nini...
Maisha inatakiwaje...
Huyo ndio mwamamke niliekuwa namtafuta...
Wengi wenye watoto akili zinakuwa zimepevuka na kutambua majukumu yao ....
 
Pole na hiyo changamoto, wanaume tumeumbiwa mateso na kuhangaika ila kuyapunguza ni juhudi zetu wenyewe.

Kuoa mwanamke aliyezalishwa na kuachwa wala sio kosa bali ni upendo wa dhati japo changamoto huwa ni masaibu na hao wazazi wenza kutaka kuyala matapishi yao sometimes.

Cha kufanya hapo na ni cha lazima na ilibidi ufanye mapema kabisa kabla hata ya ndoa: ni mtoto kupelekwa kwa baba yake, baba yake ataamua akae naye ampeleke kwa wazazi wake na kama inashindikana kabisa basi mkeo ampeleke kwa wazazi wake na mahitaji na mawasiliano yote yafanyike moja kwa moja kwa anayekaa na mtoto na sio kupitia kwa mama mtoto wala baba mtoto. Huwa wanapasha viporo na wanaweza kutaka kurudiana kutokana na uhitaji wa kuzaa tena mtoto/watoto na kuna uwezekano mkubwa ukadhurika hata uhai wako.

Usikae na mtoto wa mtu mwingine. Mimi nilizalia sehemu mke wangu alileta ushirikiano mzuri sana kuwa tuchukue mtoto amlee mwenyewe kama mtoto wake. So kwa namna nyingine alisaidia matumizi bora ya fedha na pia kuzuia mawasiliano yangu na huyo mzazi mwenzangu.
COPY
Thanks alot
 
Back
Top Bottom